Mimi ni mtu wa aina gani?

pascal luoga

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
232
257
Habari wana jamii forums.

Twende moja kwa moja kwnye mada.

Mimi ni kijana wa rika fulani 20-30 ni mfanya biashara.

Sababu zilzonifanya niandike huu uzi ni kutokana na maisha ninayoyaishi mpaka muda mwingine najikuta najishangaa na kujiona ni kama mtu wa ajabu

Iko hivi kwa kipindi changu chote huwa sinaga marafiki, watu wangu wa karbu especially ninaoishi nao mtaa mmoja wanajitaidi sana kujenga urafiki na mimi kwa kuja nyumbani na kunijulia hali mara nyngi ila mimi binafsi sinaga hali hiyo ya kusema niende kwa rafiki kumtembelea hata kama yuko karbu na mm. Mpaka sasa nina marafiki wawili tu ambao niko based nao kwa upande wa nyumban yaani mtaani ambao naweza kwenda mahala pao ama kuspend some areas with them ila wengine ote waliobaki ni kuwasalimia kwa salamu tu njiani bac

In short ni kwamba sina tabia ya kujichanganya na watu yaani marafiki ,niko radhi nikae ndani kutwa nzima.

Sabubu ambazo nimejaribu kuchunguza na kuziona kwangu ni kwamba. ''huwa napenda sana kukaa mahala tulivu especially alone'' pia huwa najikuta mtu ambaye nakua interested naye ni yule ambaye namuona anakitu ambacho kinaweza kuwa na mchango kwangu kwa kifupi ambaye ni mfanya biashara pia.

Sifuatilii KITU CHOCHOTE .
Sifuatilii mpira
Sifuatili ngumi, kuogelea ,basket wala mchezo wowote ule katika huu ulimwengu.

Kilichinileta humu ni mnisaidie niweze kujitambua kwamb mimi ni mtu wa aina gani? Huenda labda bdo cijajitambua bado wapendwa
Naombeni msaada wapendwa huenda siko sahihi kwa haya maisha ninayoishi....
 
Kama hilo jina ndio lako halisi, basi tatizo linaanzia hapo kwenye umri....unawezaje kuwa na utoto na utu uzima kwa pamoja? 20 - 30 years of age sio?
 
Sio ajabu sana. Utakuwa mtu mwenye akili zaidi kupita watu wa kawaida, na akili yako imepangiliwa sana, yaani upo objective zaidi na unapenda mpangilio wa mambo, au unapenda kila kitu kiwe na maelezo mazuri (logic) la sivyo hakifanyi maana kwako. Ni mtu mwenye kuvutiwa zaidi na mantiki kuliko hisia.

Pia ni mstaarabu na mpenda haki. Hizi ni baadhi tu ya tabia zako nzuri. Kadiri unavyokuwa mkubwa utajigundua zaidi na utajimudu na utaweza kuwa mtu wa kuaminika sana.

Elekeza nguvu zako zaidi kwenye kuwasaidia watu kwani unaweza mengi ambayo wengi hawayawezi. Kwa namna hii utafungua mlango kwa wengine na pia utakuwa sehemu muhimu ya jamii kwa kujumuika na jamii kupitia vipaji vyako.
 
Binafsi mimi naona huna tatizo mkuu binadanamu tumeumbwa na hulka tofauti tofauti ambazo huwa zingine ni za kuzaliwa nazo zingine ni kutokana na mazingira uliyoishi tokea utotoni,,,,hivo ndo inatufanya tuwe tofaut ingawa muda mwingine hulka ya namna kama yako ikizid sana inaweza kukuletea msongo wa mawazo na kishindwa kutatua matatizo na kutengeneza fursa za mafanikio.

Ila ukiamua kubadilika inawezekana pale utapoamua mfano hufatilii mpira unaweza kusema sasa nataka nifatilie mpira,,,,unape nda kukaa ndani unaweza kuwa na ratiba yako ya siku nzima kwamba muda flani ntaenda sehemu fulan au kumtembelea flani hivo ukiona hiyo hali huitak unaoweza kabisa kuifundisha akili yako wewe nini unataka baada ya muda utabadika kabisa!!
 
Shukran ndugu

Nashukuru ndugu
Sio ajabu sana. Utakuwa mtu mwenye akili zaidi kupita watu wa kawaida, na akili yako imepangiliwa sana, yaani upo objective zaidi na unapenda mpangilio wa mambo, au unapenda kila kitu kiwe na maelezo mazuri (logic) la sivyo hakifanyi maana kwako. Ni mtu mwenye kuvutiwa zaidi na mantiki kuliko hisia. Pia ni mstaarabu na mpenda haki. Hizi ni baadhi tu ya tabia zako nzuri. Kadiri unavyokuwa mkubwa utajigundua zaidi na utajimudu na utaweza kuwa mtu wa kuaminika sana. Elekeza nguvu zako zaidi kwenye kuwasaidia watu kwani unaweza mengi ambayo wengi hawayawezi. Kwa namna hii utafungua mlango kwa wengine na pia utakuwa sehemu muhimu ya jamii kwa kujumuika na jamii kupitia vipaji vyako.
 
Back
Top Bottom