Mimi ni mpish mwenye uzoefu wa kupika vyakula mbalimbali, natafuta kazi

Imphuvyi

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
224
151
Habari, husika na cha habari hapo juu.

Mpishi anatafuta kazi, jinsia (Me).

Sifa:
Ana uzoefu wa kupika vyakula mbalimbali vya ndani na nje, michemsho ya kila aina hadi ya mamba! ni mpishi mzuri wa bites, na ni mzoefu wa BBQ, sekera na shawarma.

Nb, hana vyeti, kazi zote hizo amejifunza kwa vitendo sehemu mbali mbali alizopita pita. Sasa anahitaji ajira. Anaomba msaada wenu tafadhali

Mawasiliano 0769636666.
 
Bado nina uhitaji ndugu zangu.

Mim ni mpishi mzuri mno ktk sekta mbali mbali naombeni kazi.

Lkn pia niwashukuru wote mliyoonesha nia ya kunipa kibarua kutoka mikoani,na niwatake radhi maana mimi nipo dar es salaam, nina miaka 31,na nina Familia. Hivyo kwa kazi ya muda (temporary) Siwezi kusafiri. Lkn kama itakuwa ni kazi walau ya mkataba hata wa mwaka mmoja, nipo tayari kwenda popote. Asanteni.
 
Wakuu mimi pia ni driver, nina leseni ya Kuanzia class c1, pia ni IT Ngazi ya cheti. Hivyo wenye hotel naamini naweza kuwafaa kwa namna fulani ktk shughuli zao. Naombe ajira.
 
Siku hizi wanaangalia magamba bwa shehe kwenye mihotel ya maana na migahawa mikubwa, labda mitaani ndo najua kupika vyakula vyote ya maneno.
 
Nimekupigia, sijakupata, una uzoefu wa muda gani, uko wapi? mfano sehemu kama kigamboni unaweza kufanya kazi,
Maswali ni mengi kwenye simu ndio vema zaidi.
 
Habari za jioni wakuu...
Nashukuru sana kwa mara nyingine kwa wote mliyoonesha nia ya kunisapoti (kuniajiri, kunipatia kibarua). Mbarikiwe sana.

Nimefanikiwa kupata nafasi sehemu japo ni ya muda (not permanent) lkn kutokana na kwamba wamenikuta mkweli, (maelezo ya Ujuzi wangu yameendana na uhalisia) namshukuru Mungu wananilipa vizuri sana japo ni kwa siku (daily payment).

Hivyo kwa sasa sipatikani tena ( simaanishi kutopatikana kwa simu). Lakini ikiwa kuna Atakae nihitaji kwa ajili ya kazi ya mkataba, nitakuwa tayari.

Nawashukuru sana, moja ikiwa ni kwa sababu kwa wote tulifanikiwa kukutana kwa ajili mahojiano, tulikwenda vizuri.

Asanteni sana.
 
Pamoja mzee..
 
Back
Top Bottom