Natafuta kazi: Mimi ni dereva pia nina uzoefu wa biashara ya gesi

Kyawanjubu

JF-Expert Member
May 13, 2017
2,436
2,156
Ndugu zangu habari zenu. mimi ni kijana wa miaka 32, ni baba wa watoto wawili.

Nilikua nafanya kazi kwa ndugu kama dereva na mtu wa mauzo kwenye biashara ya mitungi ya ges anauza jumla. Tulikuja tofautiana aliponiona naanza kuwa na maendeleo kidogo.

Maana nilianza kujenga msingi wa nyumba kijijini ili nimjengee mama akaniletea visa mpaka akanipeleka police kwamba nimemuibia. Mwisho wa siku ikaonekana sikuiba ikawa ndo mwisho wa kuacha kazi.

Nikarudi mtaani nikafungua biashara ya gesi maana ndo nilikuwa na uzoefu nayo baada ya miaka miwili biashara yangu ilikua sana lakini daaa inauma sana siku naamka asubuhi kwenda kufungua kazi nilikuta pamevunjwa.

Na tairi za gari inaonyesha watu walikuja na gari wamebeba mzigo wote. Nilienda kwenye vicoba nikakopa mil 2 nikaanza tena biashara ya viatu vya mtumba.

Ni mwaka jana mwezi wa 8 nikiwa nimeamka asubuhi sa 11 nafata viatu moshi nilete arusha nilikutana na vibaka wenye bodaboda wakanipora hela yote na kunikata na panga sana mikononi. Sasa hivi nimepona.

Naomba mtu yoyote mwenye kazi anisaidie maana nimekaa sana nyumbani. Wife kapambana sana juu yangu lakini naona saizi kaanza kuchoka. Kazi ninayoweza ni udereva na biashara yoyote.
View attachment 1703312
 
Duh all the best, japo maelezo yako yanaleta maswali mengi sana.

Anyway, watakuja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom