Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,157
- 4,457
Kabla sijaoa kwa nyakati tofautitofauti nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasichana wadogo, mmoja alikuwa Secondary form three, mwingine alikuwa form four, na kwa Mara ya mwisho nilitembea na mtoto wa form Six hii ilikuwa ni katika harakati za kukidhi mahitaji yangu ya kimwili hasa ikichukuliwa kwa kipindi kile ilikuwa ngumu sana kwa mimi kumiliki mwanamke serious.
Kutokana na hali niliyokuwa nayo kimaisha(Kiuchumi) ilibidi nijikite katika kutafuta mtu ninayeweza kumdanganya kwa vichips mayai vya hapa na pale na ilikuwa ngumu kwangu kufikilia kuoa maana nilikuwa naishi katika mazingira ya Gheto (chumba kimoja mnashea watu kadhaa) huku kila kukicha tukihangaika kusambaza barua za kuomba kazi, nadhani wengi wetu tumepitia hili baada ya kumaliza vyuo.
Lakini Baada ya kuoa kutulia na ndoa yangu na Mungu kunijaalia Katoto kazuuri ka Kike na baadaye katoto kengine kazuuri ka kiume, achilia mbali kwamba nilishaacha kabisa hayo Mambo, lakini huwa naumia sana nikiona mtu mzima ana mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa shule awe wa Kike au wa kiume hata kama yupo Chuo kikuu, roho inaniuma sana na naichukia sana hii tabia ya kuchukua mtoto wa shule maana naona ni uharibifu, hii imekaaje? Je mimi ni mbinafsi? Maana hii hali imenikuta miaka ya hivi karibuni baada ya Muumba kunipatia watoto, je hii hali imewakuta na wanaume wenzangu?