"Mimi ni gamba, tena nene"

"Mimi ni gamba, tena nene"

Mi nadhani huyu ana akili sana. Sema labda kujua kuwa ana akili nako kunahitajili akili. HAPO HPJA YAKO ITAKUWA SAHIHI.
 
Uandishi wa hii thread unanikumbusha uandishi wa Richard Mabala na safu zake za 'Makengeza' na 'Mabala wa Mabalaa!'
 
Hoja imefika kwa mwenye kujua hoja. Hoja ni kali mno, ilihitaji kupakwa mafuta kidogo ili wenye ngozi laini waweze kugusa. Vinginevyo hoja imefika, ingawa inauma kama sindano PPF.
 
Wow! I like it!

Kuna mmoja wetu hapa anashauri mwandishi angepeleka ushahidi mahakamani kama anao. Niulize tu, nani anapeleka ushaidi wa 'detainee' Rwakatare mahakamani? Magampi yameonekana wazi lakini magamba na vyombo vyake ummebana hamtaki yaende mahakamani?

Hata kama ushahidi ungekuwepo nini cha maana kingefanyika? Yuko wapi Balali? hukumu gani ingetolewa kwa marehemu muaji Dito? Hukumu gani ilitolewa kwa muaji Chenge? Nayule wa wizi za ujenzi wa majengo pacha?

Mnnn...hivi ktk nchi ya utawala wa sheria Kinana angekuwa huru? Siyo EL angekuwa ametaifishwa mali zake zote?....

Wakati namaliza elimu yangu...vijana wengi niliokuwa nao nilisikia wanasema kuwa magamba ili watajirike haraka...baadhi yao ni magamba na wametajirika haraka.

Ni mfanyakazi gamba pekee anayeweza kuwa na utajiri mkubwa pasipo kuhojiwa utajiri wake.
 
Ndiyo maana mimi nilisema"UKITAKA KUNIVUA GAMBA HAKIKISHA NIMEKUFA KWANZA",Gamba langu haliwezi kuvuka nikaendelea kupumua.
 

Attachments

  • Mangula.jpg
    Mangula.jpg
    10.5 KB · Views: 72
  • Mangula2.jpg
    Mangula2.jpg
    9.3 KB · Views: 71
  • Mangula3.jpg
    Mangula3.jpg
    9.6 KB · Views: 70
  • Mangula4.jpg
    Mangula4.jpg
    10.2 KB · Views: 72
Lakini mleta mada naona kwenye uandishi wake amejaza kebehi za kutosha as if on earth everything is perfect except CCM and its government.

Dhana ya watanzania kujiuliza tumeifanyia nini nchi yetu ndio inakuja hapa, je, mleta mada kama haya ya wizi unayajua, umechukua hatua gani madhubuti mbali na hii ya kuja kulia lia humu JF?

Kama una vielelezo vyote vya kubaini wahusika wa matukio uliyo yaeleza, kwanini hamtaki kuviwasilisha mahala stahiki? Na sio pengine, ni polisi.

"KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI, KIDUMU CHAMA TAWALA."

Ungerudia tena kusoma story yake!!!, Hajaiponda ccm kuwa ina mapungufu ila amesifia maradufu juu ya utendaji wake mzuri hasa katika matumizi ya mali za umma na ametoa mpaka mifano kadhaa ya uzuri wa kuwa gamba, ndio maana naye anaenda kuungana nao.

Kwenye ishu ya kuwa na vithibitisho na kuwatia nguvuni sio shida yake ndio maana kakwambia ishu ya Dowans, Rich, kagoda na ishu ya mtondooo kwa kina... yote hayo yameshindikana kwa ajili Gamba!!!!. Na kuonyesha usahihi wa hayo kuna ripoti yeyote ya ufisadi huo ilishawahi kuwa wazi? ndio maana kakwambia kaugonjwa cha kupayuka.

Na kwa staili hiyo kitadumu chama cha mapinduzi.
 
Back
Top Bottom