Mimi ni fundi Simu, natafuta kazi

Mimi ni fundi Simu, natafuta kazi

Wazo lako ni zuri sana kama ukipata mtu mwenye duka la kuuza spare za simu, wewe unabadilisha vifaa na kurepair wote mnapata...
 
Mkuu hapo Kariakoo nafasi zipo za kuweka meza?
Huwa wanalipa kodi?
Kama wanalipa Ni kiasi gani?
Kwa muda gani?
kwa uzoefu wangu kwa sehemu nyingi wanaoweka meza pembezoni mwa barabara zinazoingia mitaa ya kariakoo hawalipi chochote ndio maana mgambo wanawandama.

Ila kuna zile parking za magari, unaongea na wale wanaotoza ushuru wa parking anakumegea nafasi mtakubaliana labda kwa siku umtoe buku...lkn bado mgambo watakuandama ni wewe uwaungishe.
 
Apo itabidi blower niwe navaa shingoni ili nikianza kutimua mbio nisiache kitu
Blower ya kazi gani wakati 90% ya watu wenye vimeza karikoo awana umeme kazi yako kubwa wewe itakuwa kubadilisha vioo ukiwa na kipengele cha kuchoma utaingia ndani kwa mafundi wenzako
 
Ufundi simu unachukuliwa easy sana mimi ni fundi simu niko dodoma kuna mshikaji namuamini sana kwenye kutengeneza iPhone ni best dodoma hii juzi nilikuta analipia dollar 800 kujifunza kutengeneza face id full course online
 
Ufundi simu unachukuliwa easy sana mimi ni fundi simu niko dodoma kuna mshikaji namuamini sana kwenye kutengeneza iPhone ni best dodoma hii juzi nilikuta analipia dollar 800 kujifunza kutengeneza face id full course online
YouTube mbona watu wanafundisha bure,hiyo Dola 800 karibia m2 kabisa....hiyo ananunua mavifaa kibao,mi naona YouTube Ni chuo Ada Ni bando.
 
Blower ya kazi gani wakati 90% ya watu wenye vimeza karikoo awana umeme kazi yako kubwa wewe itakuwa kubadilisha vioo ukiwa na kipengele cha kuchoma utaingia ndani kwa mafundi wenzako
Hapo unakuwa dalali,ukitaka sehemu yenye Moto unapata?
 
meza ni nyepesi na ndogo sana, mgambo wakija unanyanyua na mkono mmoja na mwingine umeshika benchi lako na mwavuli 😄
Hii nilionaga miaka ya 2012....jamaa walikuwa wanauza saa,chaja,na urembo Sasa wakuja mgambo unaona jamaa wanakimbia na meza mkononi,na kule posta pale maeneo ya ofisi ya posta na JB Belmont hotel walikuwepo wakina mama wanauza maandazi wakija mgambo wanapakia maandazi yote kwenye Gari Lao.
Unaamka asubuhi kwenda kukimbizana na mgambo.....sema hapo Kariakoo udalali mwingi.
 
Nahitaji msaada wakuu ili niondoe ili tatizo inaonekana simu ilikuwa flashed
images.jpeg
,Nina Samsung mpya A12 ila nikiiwasha bootloader imeshakuwa tiyari unlocked , na inaleta maandishi error yafuatayo
👇👇

1."The phone is not running Samsung’s official software. You may have problems with features or security. And you won’t be able to install software updates."

2."This phone’s bootloader is unlocked and the software integrity can’t be verified. Any data on this phone may be vulnerable to attackers. Don’t store any important or sensitive information on the phone."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom