Mimi ni CCM damu, kwangu mimi chama kwanza, maendeleo ya nchi na familia yangu baadae

mkezwag

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
3,245
1,080
Wanajamvi mimi ni mwanachama na nimeendelea kuwa mwanachama mtiifu na mwaminifu kwa chama cha Mapinduzi toka nilipojiunga nacho ccm miaka ya tisini.Chama hiki kilinipeleka shule ya wanafunzi wenye vipaji maluum pale mkoani morogoro,shule iliyokuwa inamilikiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 100% yaani Mzumbe Sekondari na ambayo ilikuwa inaendeshwa na kodi za wadanganyika wakulima na wafanyakazi.Pamoja na Mzumbe kulikuwa na shule nyingine nzuri za umma zilizokuwa na hadhi sawa na mzumbe kama vile Iliboru-Arusha,Msalato-dodoma,Kilakala-Morogoro,Tabora boys na girls za Tabora ambayo watoto wa wadanganyika masikini walipata elimu bora hapo.

Wakati huo watoto wa masikini na matajiri wa nchi hii tulibanana kwenye shule hizo,tulihudumiwa vizuri(Kiukweli pale Mzumbe wali kuku ilikuwa chakula chetu cha kawaida kabisa),tulikuwa na maktaba iliyojaa vitabu,kila mwanafunzi alikuwa na kitabu chake si cha hisabati,biology or physics,Tulikuwa na walimu wazuri-Mr.Mkomboti(Mungu amuweke mahali pema peponi)na wengineo viwembe.Kiukweli tuliinjoy kuwepo mzumbe for our six years.Makoteo yakitoka si ya form four or form six tulikuwa tunaangalia nani kafeli,maana sisi kufaulu kwa point 3 for form six au point 7 kwa form four was not an issue.Ada kubwa niliyolipa ilikuwa shilingi elfu 60 mwaka wangu wa mwisho-form six.Nilikuwa nikilipa hiyo ada ndogo wakati nchi hii ikimiliki mgodi mmoja tu -Mwadui mambo ya Almasi yale.

Sasa hivi mambo yamebadirika sana,mawaziri wetu ndiyo wanafanya biashara ya shule,waziri mmoja ambaye sh.milioni 10 za KiTZ ni pesa ya Mboga anakili kupewa 1.6B kuwekeza kwenye shule yake,Vigogo wengi wa nchi wana shule zao,Lini watawekeza kwenye shule za umma kama Mzumbe,Kibaha,Tabora boys nk.Je wakiwekeza kwenye shule hizo zikawa kama ile mzumbe niliyosoma mimi nani atasoma hizo shule zao?biashara yao itakuwa imekufa nani atakubari biashara yake ife kirahisi?

Pamoja na Shule zetu kufa na wanangu kukosa matumaini mimi nitaendelea kuwa mwaminifu kwa ccm na kuipa ccm kura yangu maana kwangu mimi ushindi wa chama changu ni muhimu kuliko future ya watoto wangu,watoto wa ndugu zangu na wajukuu zangu.by the way kila mtoto anazaliwa na riziki yake,ye RIZ1 alizaliwa awe waziri,mwanangu alizaliwa awe boda boda

Sera ya elimu bure hadi kidato ya nne mr.hapa kazi tu anakuja kuisimamia,ninahakika mwanangu hatafeli si darasa la nne wala la saba na hivyo form four atafika na kupata cheti akimaliza hata kama hatakuwa na kitu kichwani lakini cheti si atakuwa nacho?Ndiyo sasa Mungu anipe nini?

Mimi ccm kwanza future yangu na ya watoto wangu baadae
 
Hhaahahahhaahahah...Mkuu umenikumbusha mimi maisha ya Pale Ilboru

Lakini kwa sasa waeiua ile Shule
 
Ni wachache sana watakaokuelewa falsafa ya andiko lako hili....na maana nzito iliyobebwa humu.
 
Sera ya elimu bure hadi kidato ya nne mr.hapa kazi tu anakuja kuisimamia,ninahakika mwanangu hatafeli si darasa la nne wala la saba na hivyo form four atafika na kupata cheti akimaliza hata kama hatakuwa na kitu kichwani lakini cheti si atakuwa nacho?Ndiyo sasa Mungu anipe nini?

Mimi ccm kwanza future yangu na ya watoto wangu baadae

Kama akifeli, cheti cha form four hapati ndugu au labda leaving certificate lakini si CSEE
 
sawa tumekusikia kua uliwahi kusoma mzumbe...lakini vile vile , tungependa kujua hili taifa limefaidika vipi kutokana na elimu au kipaji chako, kwani fedha zetu za kodi zilitumika kukupatia wewe hiyo wali kuku ambayo unaaiita sio issue.
 
Hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nimekusoma nikakumbuka comedy za Anne Kansiime!!
Pamoja na kusoma shule ya watoto wenye vipaji maalumu hicho ulichokiandika hapo ndicho ulichofundishwa huko shuleni?
Je wewe kwa sasa riziki yako ni ipi nikiamini cheti ulipata!?

Pole sana kama ulichanjiwa CCM hiyo miaka ya tisini ukiwa haujielewi bado!!
 
Back
Top Bottom