Mimi ndiye niliyeanzisha msemo wa jipu kabla ya Rais Magufuli

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kwa ajili ya Record to Ningependa Kusema Mimi Ndiye ambaye Nilitumia Msemo wa JIPU, (Sisemi Kuwa Magufuli anafanya Vibaya Kulitumia, Nimesema tu kwa kuwa Nasikia Limevuma huko bongo Kila mahali Jipu, Majipu. Sina Ugomvi Kabisa na Rais Magufuli wala sina nia ya kumfanyia ufidhuli Magufuli kwa Hilo) Wakati Nikipiga Kampeni sana Kwa Kuwanadi Ukawa, Pamoja na kua Nilimpenda sana Magufuli na Nikaweka wazi. Bado Niliamini na Ninaamini Kuwa CCM ni Kidonda, imeoza Kupiliza uwezo Na Hakuna Kiongozi Yeyote kutoka CCM atakayeweza Kuleta Mabadiliko ya Kweli Tanzania akiwa CCM Kama ilivyo sasa. CCM Ni Sikio La Kufa. CCM NI DONDA NDUGU.

Ushahidi wa Nilivyoanzisha Msemo wa Jipu!

Pia Nililaumiwa Kwa Kumtuhumu Magufuli Kuichukua kwa nguvu na Kuitumia Nembo ya Chadema ya M4C Na Kuitumia. Ukweli Nilijua Nilikuwa Tu Nikitumia Mbinu ya Maarufu ya Kisiasa Kutumia Maneno au Makosa ya Mpinzani wako kumpunguzia Makali. Sio Kuwa Niliamini Kuwa Magufuli ni Mwizi la hasha.



Ushahidi Wa Nivyomheshimu Magufuli, Katikati ya kupigia Kampeni Ukawa

Ukweli Mimi Tangu, 2006 Nilikuwa Nikirudi Nyumbani Kutoka Kazi zangu Nilikuwa (1) Naoga, Nakaa sebuleni Naangalia Habari za Dunia, CNN, na MSNBC, na FOX News, Halafu nafanya Tathmini yangu Mwenyewe. Kisha Naingia Kwenye Komputer, Nasoma Magezeti, ya Tanzania IPP Media, Mwananchi, Mtanzania na Kisha Nafanya Tafsiri yangu Mwenyewe. Kisha Naingia Mtandaoni Kutaka kujua MAGUFULI anaendeleaje, Nikafanya hivi mpaka 2015 Nikatibuliwa na CCM Kufanya Uonevu kwa Lowassa. Na Mizengwe ya Kinafiki. Na Mimi Mtu akionewa nisione, Najisikia kama natapika Roho!

 
Duh, hii dunia kuna vituko!

Ama kweli zaliwa uyaone maajabu ya dunia!

Hawa ndiyo wanaojiita kwenye mitandao USA baby, USA baby!

Mwl. Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema upumbavu ni kipaji kama ufupi na urefu.

Kutojua si jambo la kuhukumiwa. Ni motisha wa kuishi.

Mjinga akishaambiwa, inakwisha. Ujinga ni kutojua.

Huyu USA baby, USA baby anahitaji elimu ili aelimike kuhusu siasa za Tanzania!

Watu wa USA baby, USA baby sijui wanakula maharage ya wapi?
 
Sawa mkuu kwahyo Magu kaiba log yako? Kumbuka jamaa anatumia ilani ya Ukawa mwache ayatumbue tuu hayo majipu tutaona mwsho wake
 
Hii ni Tovuti ya Mijadala na Maswala Mbali mbali ya Jamii ikiwemo Siasa, Sasa Hii Kutuna inaonyesha nini? Jibu hoja ya Mtu kama Unalakumpinga toa hoja halafu Ukimtukana ajue umempa sababu. Ika kama utaamua Kuonyesha dharau kwa wengine Ni Haki yako, ya Kujidhalilisha!
 
Hakuna dhihaka hapo, ni ushauri wa bure.

Bandiko lako linaashiria kila dalili za mtu mwenye bawasiri.

Watu wenye akili wanatoa madai, kisha wanasema, N this is why,(Wanatoa sababu) Sasa Ili Nisije na mimi nikawaza u miongoni mwa wale waliodondokewa na Nazi Kichwani wakiwa watoto, kwa Kuepukaa gharama zisizo la lazima Daktari akashona-shona fuvu bila kurudishia Ubongo! labda nikuombe unipe sababu. Kama Umevaa Miganda ya Kijani Usinipe sababu nshaijua!
 
Hii ni Tovuti ya Mijadala na Maswala Mbali mbali ya Jamii ikiwemo Siasa, Sasa Hii Kutuna inaonyesha nini? Jibu hoja ya Mtu kama Unalakumpinga toa hoja halafu Ukimtukana ajue umempa sababu. Ika kama utaamua Kuonyesha dharau kwa wengine Ni Haki yako, ya Kujidhalilisha!
Muache na yeye atumbue jipu la ukweli..
 
Ni vizuri kuumiza kichwa kusaka pesa kwa ajili yako na jamii kwa ujumla kuliko kuumiza kichwa kutafuta sifa ya watu wajue mimi ndiye.....sijui ni lini Tanzania tutapata watu wa kututoa sehemu moja kwenda nyingine kwa michango yenye tija na kuibadilisha jamii
 
Una haki miliki ya hilo neno?
No Na wala Sisemi Kuwa Magufuli anafanya Vibaya Kulitumia, Nimesema tu kwa kuwa Nasikia Limevuma huko bongo Kila mahali Jipu, Majipu. Sina Ugomvi Kabisa soma kama Umeona Nikimfidhuli Magufuli kwa Hilo
 
Sijui na mimi nitafute nini la kusema nipate kiki kypitia Mh. Magufuli.

Ungenyamaza tu hii kujitetea unachemsha. So hauna kitu kingine cha kuandika sasa unataka nini, ulipwe fidia? maana ni wewe tu umetumia maneno ...jipu... na Mh. Raisi alikusikia akakuibia

Aaagh na mimi nashindwa kuandika nazunguka tu maana bado nafikiria utalipwa shilingi ngapi unayoitamani au cheo gani unataka. Yaani duh
 
Back
Top Bottom