Mimi na wewe... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimi na wewe...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Aug 16, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Leo asubuhi nilikua nafikiria kitu nikajikuta naangalia mahusiano na ndoa kwa namna ambayo sikuwahi kabla. Mimi na wewe ni kama vipande vya puzzle ....you've got your share and I have got mine.Ukiviweka pamoja either unapata picha/umbo kamili ama hupati.

  [​IMG]
  kila mmoja ana shape na size tofauti.Inapotokea wewe kama puzzle umemchagua mtu ambae yeye kama puzzle hana shape zinazoendana na vipande ulivyonavyo ndipo matatizo na migongano inapoanza.Utajitahidi kunoa na kuongeza zile sehemu zisizofit vizuri kwako au kwake ila mwishoni unashangaa pamoja na jitihada zako zile sehemu zinapwaya na ukiendelea kulazimisha zinavunjika na kuvunjika.

  So jambo la muhimu hapa ni kutafuta vile vipande ambavyo vinaendana na vyako_One that is complementary to yours....one that accomodates your needs.
  [​IMG]
  Linapokuja swala la ndoa ndo kabisa umakini wa hali ya juu unahitajika.Hapa kinachofanyika ni kuvishikanisha vipande vyako na vya mwenzako kwa glue.Hata kama haviendani at first havitakua na jeuri juu ya glue....ila baada ya muda utashangaa huku kunameguka...na vikianguka tu vinavunjika vunjika.Ila kama vitakua vinaendana ni rahisi kustahimili mitikisiko na mianguko.Hata sehemu ikimeguka ni rahisi kuirudishia.Kwahiyo kuweni waangalifu....usichukue tu vipande ni vipande...
  [​IMG]
  ....bali tafuta vile vinavyokufaa!!

  Mchana mwema!!
   
 2. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Aika mae sema wakati mwingine hivi vipande kabla ya kufungiwa huwa vinaonekana kuganda pamoja,lakini vikifungiwa tu huwa sielewi labda joto la chumba huyeyusha gundi iliyopo.
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  thax lizzy maana siku hzi kuna na vya kichina kinaeza kufit siku moja kumbe feki.
   
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kweli hapa ni kwa Great Thinkers. Nimeifurahia hii .... sijui mi nitapata anayefit au nitapata asiyekuwa na gundi ya kunifanya ninate kwake?
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Its true its all about compatibility......

  Na ni vema ujaribu kubadilisha piece yako ya puzzle (yaani wewe) kuliko hujaribu kumbadilisha yeye (au kujipa moyo kwamba atabadilika..)

  A Zebra Can Never Change Its Stripes.....,
   
 6. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Naendelea kutafakari tutakutana mbeleni....
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lizzy Mdogo wangu,

  Hii dunia ingekuwa na huruma kidogo tu labda tungekuwa tunaweza kutabiri mazuri au mabaya yanayotusubiri mbele yetu.

  Kuna watu vipande vinakuwa na perfect fit utadhani vilitegenezwa baada ya kuwa vimepimwa tena kwa special order...Ila huwezi kuamini kwamba vinashindwa kuhimili mitikisiko na kuvunjika vunjika kabla ya kufika nyumbani. Na kuna vingine ni so irregular kiasi kwamba hata kuvilazimisha vigundishwe inakuwa nje ya uwezo wetu wa kufiriki..Ila mtu unashangaa jinsi miujiza inavyojitokeza na kuvifanya viishe pamoja utadhani nilikuwa pacha toka day zero.

  Maisha yaachwe tu yawe hivyo kwani hata kinyonga ana nafuu!
   
 8. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Lizzy mie kama chauro alicosema pande langu lilifiti vizuri sana nafikiri ile elninyo iliyoleta mafuriko ilipanuka ikawa hafiti nikawahi kulikausha na jua, usemavyo ni kweli, kabisa ila sijui ninnini huwa kinakuja kutokea
   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Unavyodhani NDIVYO - SIVYO. (Rejea wimbo wa Profesa J) Uko sawa ndugu yangu.
   
 10. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuna wakati miracles happen na watu hubadilika.., lakini sio vema kuingia uhusiano na mtu kwa kusema kwamba atabadilika au utambadirisha tabia zake..., mara nyingi hapo ni kuleta mfarakano..., na sio fair kutaka kumbadilisha mtu tabia kuendana na unavyotaka wewe (hapo ni kutaka mtu afanye sacrifice...)

  Kumbuka tofauti zina-depend (sababu kama hupendi mtu anaekunywa au kuvuta sigara basi ni dhahiri kwamba itakuwa karaha kupata mtu anaekunywa..., au kama una wivu sana itakuwa karaha kupenda mtu outgoing na mcheshi na anaejichangaya).., Kama hupendi kelele itakuwa karaha kuwa na mtu mwongeaji and vice versa...


  Ni bora kupata mtu ambae mna-fit in more ways than one, kwahiyo inamaanisha bond yenu ni kubwa kuliko Bond ambayo imeunganishwa na vitu vichache hapo shida zikitokea ni rahisi kuachana....
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Babu DC nimekusoma.

  Nnavyoona mimi ni hivi: wale wanaona puzzle zao zinafit na baadae hazifit na wale wanaoona hazifit na baadae wanashangaa sio kama ni miujiza au bahati mbaya vinakua vimewatokea.Bali ni matokeo ya kutumia puzzle za MATAKWA yao kutafuta kile WANACHOHITAJI!!!

  Kwahiyo wale wanaopata zinazofit wanakua wamepata kile wanachokitaka...ila baada ya muda mabadiliko yanakuja!Wanagundua kwamba walichotaka na kukipata sicho wanachohitaji!Hivyo hivyo kwa wale wanaodhani wamebahatika kuona muujiza mbele ya macho yao...mtu anakua ametumia puzzle za matakwa na kuona kwamba haziendani na za mwenzake.Ila kumbe zinaendana na mahitaji yake ambayo ni muhimu kuliko matakwa.

  Na tatizo hapa ni kwamba wengi hua tunafikiria na kujua ni nini tunachotaka bila kujishughulisha kufahamu tunayohitaji!!!Ndio maana unakuta mtu aliwahi kukupa sifa za atakae kua mke wake baadae ila siku ikifika akakutambulisha unajiliza kama amesahau sifa zake zile au la!Sio kama anakua hajawaona wenye sifa alizotaka awali. Na wkati mwingine unakuta mtu anatamba sana mwanzoni kwamba mwenzangu ana kila NNACHOTAKA ila muda sio mrefu unashangaa akisema yule hakua size yangu au hakunifaa!Ukiangalia sifa zote alizotoa mwanzo kama ni uzuri/pesa/ndoa/ n.k bado viko pale pale!!

  Au labda ndio mambo ya za mchina kama Chauro alivyosema!! lolzzz!!!
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahhhaa...Bebii asante kwa kunifurahisha!!Alafu nikakosea kusema Chauro ndo kaongelea za mchina!
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo kilichobaki ni kuendelea kuangaza macho..
   
 14. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  aika mbee!
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Gaga afadhali uligundua kwamba yalikua matatizo ya kiufundi tu ukakomaa...ungezitupa saa hizi ungekua unajutia!!
   
 16. S

  SMART1 Senior Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Liz,
  Mungu akubariki kwa ujumbe wako wa leo....
  Kweli watu tunaangalia juu juu tunapochagua mates..... na matokeo yake ni kuumizana na kuharibiana maisha....
  Right mate is comming from God!!!

  Umenifanya nikupennde... enjoy ur day
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante SMART....nawe ubariliwe pia!!!
   
 18. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Lizzy hapa umepatia more than 100%. Your statemets are more than correct and to me they mean TIMING IS EVERYTHING AND ONLY TIME WILL TELL!

   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ngwana ni kweli unayosema kwamba timing is everything ila huo msemo wa “time will tell“ sijui kwanini siupendi sana.
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  . . . . . tukumbushane umuhimu wa kuchagua mwenzi sahihi badala ya kudanganyika na vitu ambavyo kiukweli sivyo tunavyohitaji kwenye mahusiano.
   
Loading...