Mimi na mwenza wangu tunatarajia kutafuta mtoto wa kike, tunataka awe Giniasi tunaomba muongozo wenu

U giniasi wa mtoto hutokana na makuzi (malezi) unayompa katika ukuaji wake naweza kukupa mfano wa tofauti ya watoto wangu wawili hawa wa mwanzo, mmoja ana miaka mi 5 mwingine mi 2 na miezi mi 5 ila mambo anayoyafanya huyu wa miaka mi 2/5Months ni tofauti sana na kaka yake wa miaka mi 5 ambaye tulimlea kama yai (kama ujuavyo mtoto wa kwanza) ikamuwia vigumu hadi shule ubongo ulikua unalala lala kama malezi tuliyompa,lakini huyu kijana mdogo 2/5months mpaka sasa anaweza kuhesabu mpaka 10 bila kukosea,anaweza kuandika (japo vingi havieleweki) ,anahoji au kuongea lolote kwa kila anachokiona,hajikojolei wala hajisaidii choo kikubwa kwenye nguo yaani kiufupi ukikaa nae hautojisikia upweke,nyumba inachangamka sana kwa ajili yake yeye,kiufupi namtabiria mazuri na makubwa zaidi
 
Mm naamini tulizeni akili zenu vzr ,ondoweni stress ,mshauliane mtoto akulie katika mazingira gani, na pia itakuwa poua mkienda kwa daktar,vilevile muombe kwa mungu
 
Back
Top Bottom