Mimi mwanachuo

Mimi mwanachuo

Barua ya Wazi kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo,
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,

Kwa heshima na taadhima, napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya wanafunzi wa kitivo cha elimu kukupongeza kwa dhati kwa kuteuliwa kwako kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Uteuzi wako ni ishara ya imani kubwa waliyonayo viongozi na jamii ya kielimu juu ya uongozi wako thabiti, hekima na maono chanya kwa maendeleo ya elimu ya juu nchini. Tunakuombea mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yako.

Hata hivyo, sambamba na pongezi hizi, napenda kwa unyenyekevu mkubwa kuwasilisha malalamiko ya wanafunzi wa kitivo cha elimu tunaosoma shahada za uzamili na uzamivu kuhusu changamoto sugu ya ucheleweshaji wa kazi za utafiti unaofanywa na baadhi ya wasimamizi. Wasimamizi hawa wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kabisa kupitia kazi za wanafunzi, kuchelewa kutoa mrejesho au hata kutotoa majibu kwa mawasiliano ya mara kwa mara kutoka kwa wanafunzi.

Tabia hii isiyo ya kitaaluma imekuwa ikiwavunja moyo wanafunzi, kuwachelewesha kuhitimu kwa muda uliopangwa, na hata kuleta msongo wa mawazo miongoni mwao. Kwa mtazamo wetu, ucheleweshaji huu si wa bahati mbaya tena, bali ni wa makusudi, jambo linalodhoofisha lengo la chuo la kuwahudumia wanafunzi kwa njia ya haki na kwa wakati.
Mheshimiwa Mkuu wa Chuo, kwa kuzingatia dhamira yako ya kuboresha elimu, tunapendekeza hatua zifuatazo:
1. Kuweka miongozo yenye muda maalum wa kupokea, kupitia na kujibu kazi za wanafunzi.
2. Kuwabana wasimamizi kwa kuweka mfumo wa tathmini ya utendaji wao unaoshirikisha mrejesho wa wanafunzi.
3. Kuwepo kwa chombo maalum cha kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kwa haraka na kwa siri.
4. Kuchukua hatua za kinidhamu kwa msimamizi yeyote atakayekiuka kwa makusudi majukumu yake.

Tunaamini chini ya uongozi wako mpya, matatizo kama haya yatapatiwa suluhisho la kudumu kwa ajili ya maendeleo ya elimu na ustawi wa wanafunzi wote.
NI SISI WAHANGA WA KITIVO CHA ELIMU CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
 
Duh kiufupi education ni changamoto sana kwa miaka hii, ila inawezekana tu, kwan upo mwaka wa ngp saiv na unataka usome course gani?
Eee mkuu, hiyo ina kaaie kaka, mana sema ukweli education ni changamoto tukiachana na mambo mengne
 
Duh kiufupi education ni changamoto sana kwa miaka hii, ila inawezekana tu, kwan upo mwaka wa ngp saiv na unataka usome course gani?
Niko mwaka 1, nilitaka, nursing au Radiotherapy. Mkuu
Sema shida tena ipo kwenye admission competition daa
 
Aanha🙏🙏 sema insu ipo kwenye competition ya admission,
Mana hii Tanzania inafaidiwa na watu wenye connection zao, lakn kwetu kama ss ni kazi
Mkuu unaweza kutuambia uko chuo gani.
Labda tunaweza kukusaidia.
 
Back
Top Bottom