kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,289
- 12,582
Wazazi kulala chumba kimoja na watoto, watoto kulala kwa jirani, watoto kukosa mahitaji muhimu kama chakula, mavazi, nauli ya shule, chakula shuleni, mila zinazofundisha watoto mapenzi, wazazi kusafiri kwa muda mrefu. Serikali kushindwa kutoa usafiri, mabweni, chakula shuleni, kujenga uzio mashuleni. Mchanganyiko huu wa mapungufu ya wazazi na serikali unatumiwa na wanaume kupata nafasi ya kuwadanganya watoto kimapenzi kwa kigezo cha kutaka kuwatatulia watoto matatizo yao yanayowakabili kama vile ukosefu wa pahala pa kulala, mavazi, chakula, nauli, usafiri wa kwenda na kurudi shuleni, na ada. Wazazi wakali sana kwa mtoto wao anapopata alama za chini darasani, hivyo kusababisha mtoto atafute alama za juu darasani kutoka kwa wanafunzi wenzake darasani na walimu kwa gharama na mashariti yoyote. Utafiti unaonyesha kuwa ni watoto wachache saana ambao wanajiingiza kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza kwasababu ya kutaka kujirusha/starehe tu.