Mimba ya jirani yangu inatishia maisha yangu

Mimba ya jirani yangu inatishia maisha yangu

Omuzirambogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2018
Posts
685
Reaction score
753
Kuna mke wa jirani yangu amepata mimba nasikia kuwa anatamani kuvaa shati langu alimueleza mume wake hapo ndipo sakata lilipoanzia juzi jumamosi mume wake alinifuata na kunitaka nitoe maelezo ya kina kwanini mke wake atamani kuvaa nguo yangu.

Hali hii ilipelekea mke wangu naye kuuwasha moto akitaka maelezo kama hayo kusema kweli sijawahi kumtamkia neno lolote mwanamke huyo natamani hata leo ajifungue tuone mtoto atafanana na nani! Naomba ushauri hali hii inatokeaje; mimba ya mwingine mke anatamani nguo ya mwingine?
 
Angekuwa mke wangu angechezea kofi hilo nahisi kudeka kungeishia siku hiyohiyo.Msiniambie mimba inamtoa mtu ufahamu eti hajui anasema nini na anachosema kina madhara gani
Je, mkeo alishatamani nguo yako? Mimi kuna mimba alikuwa anashinda amevaa nguo zangu~
 
Hii ni hatari!!
Ningekuwa mimi nisingewachekea wote hata kidogo yaani ningeanza na mme wa huyo mwanamke mwenye mimba nikaanza kummmind kwa kuja nyumbani kwangu kuniambia mambo ya ajabu kuhusu nguo zangu..

Yàani tifu lake angekuja kuamua polisi
 
Kuna mke wa jirani yangu amepata mimba. Nasikia kuwa anatamani kuvaa shati langu. Alimueleza mme wake hapo ndipo sakata lilipoanzia. Juzi jumamosi mme wake alinifuata na kunitaka nitoe maelezo ya kina kwanini mke wake atamani kuvaa nguo yangu. Hali hii ilipelekea mke wangu naye kuuwasha moto akitaka maelezo kama hayo. kusema kweli sijawahi kumtamkia neno lolote mwanamke huyo. Natamani hata leo ajifungue tuone mtoto atafanana na nani! Naomba ushauri hali hii inatokeaje; mimba ya mwingine mke anatamani nguo ya mwingine?
Na mara nyingi mtoto akizaliwa huwa anafanana na yule mtu aliyempenda so usishangae akafanana na wewe huu ni ukweli ninaokwambia wala sikutanii
 
Hii ni hatari!!
Ningekuwa mimi nisingewachekea wote hata kidogo yaani ningeanza na mme wa huyo mwanamke mwenye mimba nikaanza kummmind kwa kuja nyumbani kwangu kuniambia mambo ya ajabu kuhusu nguo zangu..

Yàani tifu lake angekuja kuamua polisi
Nilimzingua kweli nikamuita mwanga kwasababu hainiingiii akilini mimba yake itake nguo zangu!
 
kutokana na biolojia niliyosoma ufanano utokana na vinasaba katika mbegu za uzazi sasa atafananaje na mimi wakati sikutunga mimba?

Usikatae ndo ukweli
Kuna DNA shapping

Ni kama unavyopata dalili za ukimwi ukidanganywa unao
 
Muwasamehe bure tu. Hili kasheshe lilishawahi kunikuta. Yupo jirani yangu nae anaurafiki na mke wangu. Yeye ni mjamzito na wala sijawahi mtongoza. Nikiwa home anapenda kuja kushinda home kwangu na hata nikiwa kazini anamuomba mumewake eti amlete kazini kwangu walau anione tu. Nimejaribu kumdadisi ananiambia eti anapenda ucheshi na story zangu tu.
 
Kweli mimba zinamambo! Je, kama mna uhasama atakuja kweli?
 
Back
Top Bottom