Cheers to everyone around here!!!
Naam tunamalizia mwaka, hopefully tutamaliza salama!
Back to the topic! Nini hasa kinasababisha mimba kuhama ikae nje ya mfuko ??
Nini madhara yake ? Kuna uwezekano wa kujifungua salama ??
Ps,,, kuna rafiki yangu amekutana na hii changamoto,,, ana mimba ya miez 7 , recently tumbo lilikuwa linamsumbua sana, akaenda hosp kupima ndio majibu yakatoka Kama hivo ,,, kwa hio amepewa bed rest mpaka ajifungue,,,Tena iwe ni hospital!
Naamini hapa wapo wataalam wa afya na madokta, watanisaidia kwenye Hili walau kujua abcd za hii changamoto,,,,!
Sky Eclat Carlos The Jackal ,
Mshana Jr ,
MziziMkavu , tafadhali mpite hapa walau, with due respect
Mimba Kutunga Nje ya Kizazi
Ectopic pregnancy/Mimba kutunga nje ya kizazi ni kitu gani?
Mimba ikishatungwa kwenye mirija ya uzazi inapitia hatua zingine nyingi mpaka kwenda kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi.
Endapo inatokea yai lililorutubishwa kukwama kwenye mirija ya uzazi na kushijikiza hapo au likajishikiza kwenye mlango wa kizazi ndipo tunaita ectopic pregnancy ama mimba nje ya kizazi.
Yai lililorutubishwa haliwezi kukua nje ya kizazi. Tafiti zinasema kwamba katika ya wanawake 50 wenye mimba mmoja kati yao anakuwa na ectopic. Kama tatizo halitatibiwa haraka linaweza kuleta madhara makubwa kwa mwanamke na kutishia hata uwezo wa kuzaa siku za mbele.
Nini Kinasababisha Mimba Kutunga Nje ya Kizazi?
Sababu hasa ya mimba kutunga nje ya kizazi bado haijafahamika. Wataalamu wanafikiri mambo haya yanaweza kuchangia mimba kutunga nje ya kizazi
kuvimba na kututumka kwa mirija ya uzazi kutokana na tatizo fulani la uzazi
changamoto za homoni
matatizo ya mabadiliko ya vinasaba
mwanamke kuzaliwa na mapungufu kwenye kizazi
changamoto za kiafya zinazoathri via vya uzazi kama vimbe na kuziba kwa mirija.
Daktari atakapokufanyia vipimo anaweza kukupa sababu hasa ya changamoto yako baada ya vipimo.
Wanawake Waliopo kwenye hatari zaidi ya mimba kutunga nje ya kizazi
Wanawake wote walio katika umri wa kuzaa wapo kwenye hatari ya kushika mimba nje ya kizazi. Hatari inaongezeka zaidi kwa makundi haya
kushika mimba katika umri zaidi ya miaka 35
historia ya kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi
wanawake wenye historia ya kuharibikiwa mimba nyingi hapo awali
kizazi kupanuka
Kushika mimba baada ya kufunga kizazi
Kushika mimba baada ya kutumia dawa nyingi za uzazi
kuvuta sigara
historia ya kuugua magonjwa ya zinaa kama kaswende na chlamydia
mirija kuwa miyembamba sana kiasi ya yai kushindwa kusafiri inavotakiwa.
Kama upo kwenye makundi ya wanawake hawa, zungumza na daktari atakupa mwongozo mzuri kulingana na afya yako ili upunguze hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi.
Dalili Za mimba Kutunga Nje ya Kizazi
Kupata kichefuchefu na matiti kuuuma ni dalili kuu za kwamba una mimba, aidha mimba ya kawaida ama mimba kutunga nje ya kizazi. Lakini dalili hapa chini zinajitokeza hasa ikiwa mimba yako iko nje ya kizazi na yahitaji kwenda hospitali haraka
maumivu makali yanayopita kama mshale tumboni, kwenye nyonga, mabega au shingoni
maumivu makali sana katika upande mmoja wa tumboni
kutokwa damu nzito ama nyepesi wakati una mimba
kukosa nguvu na kuanguka
kujisikia mgandamizo eneo la haja kubwa
Unahitajika kumwona daktari haraka endapo utapata dalili hizi kwani zaweza kukufanya ukapoteza maisha.
Matibabu kwa Mimba iliyotungwa Nje ya Kizazi
Mimba ya nje ya kizazi siyo salama kabisa kwa mama mjamzito. Hata hivo kiumbe hakitaweza kabisa kukua nje ya kizazi. Ni muhimu kwa kiumbe hicho kuondoloewa mapema iwezekanavyo ili kulinda afya ya mama. Tiba hutofautiana kwa kulingana na wapi mimba imetunga.
Daktari anaweza kuamua kukuanzishia dawa ili kuzuia kiumbe kutopasuka na kuleta madhara zaidi.
Daktari pia anaweza kupendekeza ufanyiwe upasuaji ili kutoa kiumbe na kutibu penye tatizo. Upasuaji huu huitwa laparatomy. Wakati wa upasuaji daktari anaweza kuamua kukata mrija endapo ikionekana umeathiriwa zaidi.
Huduma Baada ya Upasuaji. Daktari atakupa maelekezo sahihi ili ujiuguze na upone mapema ukiwa nyumbani kwako. Muhimu ni kuwa msafi na kidonda kiwe kikavu. Kila siku fatilia kidonda chako na kucheki dalili zisizo za kawaida kama
Bleed isiyokata kupata harufu kali kwenye kidonda kidonda kuwa chekundu na kuvimba kwa mshono
Ushauri huu hapa chini ni muhimu kuzingatia ili kupona mapema mshono wako.
Usinyanyue vitu vizito, kunywa maji ya kutosha ili kuzuia choo kigumu na kukosa choo, pata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo kuacha kufanya tendo la ndoa mapaka upone.
Siku zote ukiona kuna dalili isiyo ya kawaida mpigie simu daktari mweleze akupe uhakika kwamba ni kawaida au kuna shida. Madhara anayoweza kuyapata mama mjamzito baada ya mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi.
Mama mjamzito anaweza kukabiliana na athari kadhaa pale ambapo mimba itakuwa imetunga nje ya mfuko wa uzazi ambazo ni pamoja na mimba aliyobeba kuharibika, mirija ya uzazi kupasuka na kusababisha kuvuja kwa damu nyingi kunakoweza kukachangia kutokea kwa kifo!
Mama Mjamzito anapaswa kupatiwa huduma ya haraka punde tu akapobainika kuwa mimba yake imetunga nje ya mfuko wa uzazi ili kuepukana na madhara hayo!!
Tatizo la Mimba Kutunga Nje ya Mfuko wa Uzazi (Ectopic Pregnancy)