Mimba ilikuwa furaha zamani, nini kinafanya sasa isiwe furaha?

jumajs

Senior Member
Oct 20, 2015
134
23
Hapo zamani mwanamke alikuwa akipata ujauzito kila mtu alifurahi na kupongezwa na kila mtu isipokuwa wale waliokuwa na roho za korosho.

Miaka ya sasa imekuwa tofauti mwanamke akipata mimba huenda hata aliyempa akakimbia, ikatolewa au akazaliwa na kutupwa.

Je, wazamani walikuwa washamba?
 
Zamani maisha yalikuwa cheep ndio maana watu walikuwa na furaha mwanamke apatapo mimba lkn maisha ya sasa ni balaa maana kulea hiyo mimba ni mtihani kutokana na gharama zake maana mpaka ajifungue wewe ushatoboka balaa kazi inakuja kwenye malezi hapo ndio utajua kama huyo mtoto mpaka akue mtakuwa mshaparurani na mwenza wako kwa kiasi gani
 
Mimba ni haki ya kila mwanamke na mtoto ni zawadi kwa wazazi kutoka kwa mungu.
 
Majukumu,pesa,umaskini.

Ila asilimia kubwa ni mimba zisizotarajiwa wengi wana kwichi kwich sababu ya tamaa ya mwili,pesa,kuonekana mjanja(yap wapo wanawake kwa wanaume wana date ili tu aonekane nae yumo) matokeo yake mimba.

Wanawake wengine wanajibebesha mimba makusudi kumnasa mwanaume(ndoa) na ukute mwanaume hampendi mwanamke husika inaongeza mateso.hali inayopoteza furaha ya mimba.
 
Kwa sababu Wanaume wamebaki wachache wengi ni wavulana
 
Ni kweli kipindi cha nyuma mtoto alikuwa nuru na nadra kukuta abortion na haya mambo ya kukuta watoto jalalani

√√ siku hizi hali iko tofauti utaona single parent ni mingi kwa town hasaa wadada ,na hukuti mkaka yuko hivyoo kubaki na mtoto au hupeleka kwa bibi akaishi, si unajua wanawake wako na roho ya huruma ya kupenda sana hujikuta kapewa mimba Accidentally na hufanya abortio

√√ now days watoto wanaozaliwa ni kama show off flani kwa watu kuiga wathunngu,yani hana ile deep love kwa mtoto yani yeye ni kujionyesha kuwa she is someone in front of womens, ukija katika matunzoo yanaenda decelerate hamna kipya

* to stop single parent inakera
 
Back
Top Bottom