Millya Amedisturb Political Equillibrium Tanzania

In Politics:

No permanent friends and enemies but permanent interests

Very true mkuu, but nashauri, hata kama Lowasa akiachia madaraka na kujiondoa ccm, but ni mapema sana kuhamia chadema naamini hata mwenyewe hawezi kufanya hivyo. Lakini na yeye ataaamua kumaliza zama za ccm katika siasa za Tz, anaweza kuweka kila kitu kilichotokea hadharani, kuhusu Richmond na kuhusu mengine yote ambayo yanamuhusu mkuu wa kaya...kwa kufanya hivyo tu, CDM wataonekana wapo right kwa kila ambacho kiliongelewa kuhusu ufisadi na yeye atakuwa safe side kwa kumuachia mwenyekiti tuhuma nzito...hilo tu linatupa ushindi asilimia zingine zaidi ya sabani....akibaki bila chama ataaminika zaidi kuliko kuhamia CHADEMA kwani ataonekana ni mroho wa madaraka....kitu ambacho kinaweza kuwa kweli kama atahama chama....akiacha siasa ataonekana wa maana zaidi....

TOGHETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED....YES WE CAN.....GOD BLESS CDM
 
Kauna kauli watu huitumia sana.... ''We have entrusted you to lead us'' kama wanaCDM mmewaamini viongozi wenu basi fahamuni kama watampokea Lowasa watakuwa wamepima na kuwazua na itakuwa ni kwa faida ya chama zaidi.
 
Litakuwa kosa kubwa strategically kwa CDM kumchukua Lowassa. It will be the beginning of the end of the opposition in Tanzania kwa sababu itapelekea picha kwamba tunaongozwa zaidi na personal interests badala ya ideology na vision ya Tanzania tunayoitaka, na hatuna tofauti na CCM. Kwangu binafsi nitaacha kuiunga mkono Chadema.

Hata mimi nitaacha kuiunga mkono kabisa
 
Lowassa siyo mzalendo wa kweli wa Tanzania, atabaki CCM, kwani ukitoa yote analinda alichochuma na CDM haina funguo za ikulu kwa sasa na akithubutu kuhama tu unakumbuka Prof Kighoma Malima? nafikiri atabaki CCM ila huku akipenetrate CDM in case wakiula alindwe kote kote
 
Kama Lowasa ameshindwa kuibomoa CCM from within ataweza akiwa CDM? Afanye hivyo akiwa huko then ukweli ukiwa wazi na watanzania wakaelewa aende CDM

Anaweza mkuu,
Chukulia kwa mfano akitoa ukweli wake kuhusu Rchmond,akahamisha mzigo wote kwa wahusika alafu akahama.Atakua ameivunja CCM trust me.Hayo ndo yatakuwa maamuzi magumu.Mpaka sasa hajafanya maamuzi magumu
 
Kambi ya JK inanguvu sana, siyo tu kwa vile inamwenyekiti pia kwa kuwa yeye JK ambaye anaonekana dhaifu aliweza kuupata huu uraisi akipigiwa debe na wote. On that particular matter he is very strategic.

Pili Jk siyo mpole kama watu wanavyodhani na tabia yake kamili marafiki zake walii under estimate. Sasa inakula kwao, kwani ana upper hand kwenye kila uamuzi ndani ya chama.

Labda ni maizie kwa kusema kuwa huyu jamaa naona kama ni selfish kidogo, au kikubwa muda utaonyesha kwani hataki sisiemu ieishi au iendelee kuwa madarakani ili kama yeye ni wa mwisho angalau atakumbukwa na vizazi kwa muda mrfu.

Lowasa sasa amekwisha sasa na hataweza kujikwamua tena. Six mnamkumbuka wakati fulani CD4 ya kisiasa ilishuka lakini anaendelea kurefusha maisha ndani ya sisiemu,

Viva mwnyekiti wangu
 
unajua wakati wa vita yetu na uganda, kuna kamanda alitoa ushauri kuwa mgambo, jkt na servicemen wapelekwe front line, makamanda wengine walipinga sana kuwa tutakuwa tunatafuta matatizo na kushindwa vita. Jamaa alijenga hoja kuwa wakati fulani ni vizuri kuwatanguliza mbele ili wawe chambo. Cdm wanaweza kumtumia kama chambo, though nakubaliana pia na mtazamo wako.

Ila je kama lowasa akiaamua kufunguka na kusema version yake kuhusu richmond, na yale mwakyembe aliyoyaficha naamini watu wengi watampa the benefit of the doubt lowasa. Nakwambia cdm itakuwa imelamba dume...............mwanahalisi wanajua hii siri majina ya awali yaliyosajiliwa brela kampuni ya richmond, mbona walishawahi kuandika siku za nyuma ......anyway tusirudi nyuma.

Lengo la cdm ni kuibomoa ccm kama lowasa anaweza kuiboa ccm kwa 70% halafu cdm ikaathirika kwa 30% sisi wajasiliamali tunasema hiyo inalipa

positive trend
 
Vile Tanzania is in stable,unstable or neutral equilibrium. If in unstable equilibrium Mungu mrehemu marehemu.
 
Sidhani km kila mwana CCM anaweza pata no CDM.CDM walisema Nape haku qualify.wewe ukimwangalia Zitto, Lisu, au Mnyika ...nani ktk ccm awe kijana au mzee anweza pima? makamba, Nape, kingunge, Chaguo la mungu..?Nadhani km Millya kakubaliwa basi atakuwa smat zaidi ya Nape..
 
Kambi ya JK inanguvu sana, siyo tu kwa vile inamwenyekiti pia kwa kuwa yeye JK ambaye anaonekana dhaifu aliweza kuupata huu uraisi akipigiwa debe na wote. On that particular matter he is very strategic.

Pili Jk siyo mpole kama watu wanavyodhani na tabia yake kamili marafiki zake walii under estimate. Sasa inakula kwao, kwani ana upper hand kwenye kila uamuzi ndani ya chama.

Labda ni maizie kwa kusema kuwa huyu jamaa naona kama ni selfish kidogo, au kikubwa muda utaonyesha kwani hataki sisiemu ieishi au iendelee kuwa madarakani ili kama yeye ni wa mwisho angalau atakumbukwa na vizazi kwa muda mrfu.

Lowasa sasa amekwisha sasa na hataweza kujikwamua tena. Six mnamkumbuka wakati fulani CD4 ya kisiasa ilishuka lakini anaendelea kurefusha maisha ndani ya sisiemu,

Viva mwnyekiti wangu

Kikwete ni mdhaifu sana lakini waliomzunguka wanajua hilo na elewa wanafanya kazi kubwa kuficha upuuzi wa huyo mzee'
 
Muelewe kuwa huyu jamaa bado hajautoa ukweli wake hadharani. Vile vile muelewe kwamba huyu jamaa bado analaumiwa kutoka upande mmoja tu. Ni yale tu tuliyoyasikia juu yake kutoka kwa hao wanaomtuhumu. Hivi kujiuzulu kwake kwa kashfa ya Richmond kwa ajili ya kuwajibika, nani hasa anaweza kusimama na kumshutuma kuwa alihusika barabara. Mimi naamini EL si mjinga na ndiyo maana kila anapoulizwa kuhusu Richmond anajibu kuwa atalizungumzia hilo wakati muafaka. Nilizungumza na kiongozi mmoja wa nafasi ya juu sana CCM, nae akanifahamisha kuwa iwapo EL ataamua kuihama CCM nakujiunga na chama kingine cha siasa hususan CDM, na akaamua kusema ukweli wote jukwaani kuhusu Richmond na madudu mengine, basi atakuwa amepigilia msumari wa mwisho ktk jeneza la CCM. Pia atakuwa amejisafisha mbele ya wa Tanzania wote, maana kwa kiasi kikubwa ametumika kama mbuzi wa kafara. Huenda likitokea hilo na iwapo atakuwa amejiunga na CDM, hiyo itakuwa ni njia rahisi na ya mkato kabisa kwa CDM kuingia Magogoni.
 
Siku Lowasa akija kufunguka kuhusu Richmond, JF itasimama kwa muda.....nakwambia itakuwa siku ya ufufuo maana kufumba na kufumbua Lowassa atakuwa shujaa
 
Back
Top Bottom