Millard Ayo Unayumba

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,692
Reaction score
13,317
Kijana alianza vizuri lakini kwa sasa ameanza kuyumba, na endapo akitokea mtu mwingine au media nyingine nzuri anaweza akapotezwa

Millard kwa sasa ameanza mambo ya ubaguzi kwenye media yake, habalance tena habari zake, anapost mikutano ccm lakini habari za upinzani ameacha kupost, jana amepost mkutano wa ccm morogoro lakini kuhusu upinzani ameliruka

Kwa sasa hamna watu wanaofuatiliwa mitandaoni kama kundi la WCB lakini Millard haandiki kabisa habari zao kitu ambacho sio kizuri kwa mwandishi wa habari, ameshindwa kujifunza kwa wasafi media ambao wamekuwa hawana ubaguzi kwenye habari za wasanii na kucheza nyimbo zao

Kijana wetu anatakiwa abadilike la sivyo atajiharibia mwenyewe, sababu kazi ya uandishi haitaki ubaguzi kwenye swala la kureport habari, angalieni TBC baada ya kuacha kubalance habari na kugeuka kuwa tv ya kusifia sasa imepoteza watazamaji kabisa

Millard badilika
 
Usimsemee kijana kwa wakati kukiwa na sheria kandamizi kwa habari wakati huo huo ukitakiwa kutoa habari (ili ubebwe) za upande unaotawala.

Hizo za upande mmoja hata usipobalance hauwezi kuisoma hesabu.
 
Sema tu ulitaka kuwataja hao WCB..

Wanafwatiliwa sana kwa lipi la maana??

Millard anafanya kazi nzuri,jana nimecheki video ya mahojiano yake na yule jamaa aliyepata jiwe la billioni kadhaa shinyanga..was nice
 
SnS

Ndo wanaokuja kumpoteza vibaya

NA hakuna wa kuwazuia
 
Sema tu ulitaka kuwataja hao WCB..

Wanafwatiliwa sana kwa lipi la maana??

Millard anafanya kazi nzuri,jana nimecheki video ya mahojiano yake na yule jamaa aliyepata jiwe la billioni kadhaa shinyanga..was nice
haya dada mange
 
Umeongea ukweli mkubwa sana japo utapingwa.

Lkn kiukweli hata mimi nimeliona hili.
Usipokuwa huru kwa sababu ya kuogopa chama au serikali wakati hauvunji sheria huo ni utumwa tosha kabisa.

Mwisho wa siku wateja wake sio serikali wala chama fulani.

Sisi ndio wateja wake.

Atapotea soon
 
Na hizo habari zake za video zinaboa. Ni uvivu, kila habari fungua video. Muda na bando vinatoka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…