Millard Ayo azuiwa kuweka nembo yake magazeti ya Mwananchi

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,241
4,466
Kwa kipindi kirefu Millard Ayo amekuwa akituhabarisha kwa kutupa vichwa vya magazeti ukurasa wa mbele na nyuma kila siku. Kwa bahati mbaya sana, amekuwa akiweka nembo yake ya MillardAyo.com kwa kazi za watu na pia alikuwa akikata matangazo ya biashara yaliyoko kwenye kurasa hizo, akiwa hataki kutangaza biashara za watu wakati yeye hizo kazi za watu anazifanya zake.

Wamiliki wa Magazeti ya Mwananchi yenye magazeti kama Mwananchi, The Citizen, na Mwanaspoti walimzuia kuweka nembo yake inayotangaza mtandao wake wa MillardAyo.com na pia kumzuia kufuta matangazo yao pale anapopiga picha.

Tuheshimu kazi za watu.

Magazeti anayoweka nembo
d6bae01daff7d30a6450896bec744c86.jpg

32398e3efc4fd2cf2fd7da1f0ada9985.jpg

5a35df4bd60d46316464589cf4f0c8b0.jpg

968b35b976baae53fe4fbce3e7ce7038.jpg


Magazeti ya Mwananchi aliyozuiwa kuweka nembo
e88f4bc42bec175da6bf6cd097253e7e.jpg

066149aecac4ea69cf6e9d4975561c49.jpg

fc8f2b445fadf0b2808ca4a2ee44f74d.jpg
 
Hakuna madhara yoyote kwake ili mradi tunaendelea kuhabarika huyu jamaa anajitahidi sana atafika mbali sana kimaisha sasa hivi Millardayo.com imekua chanzo kikubwa cha habari
 
Daah bora wamefanya hivyo huyu keshalewa sifa na pia yupo biased Sana kwenye kutangaza habari, kifupi tu huyu dogo hana jipya.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom