Milipuko gongo la mboto - wana intelijensia hawakuwa na taarifa?

fredmlay

JF-Expert Member
Apr 30, 2008
1,849
388
Ni hivi majuzi tumeshuhudia jeshi la polisi kupitia IGP likieleza kwamba limepokea taarifa za ki-intelijensia zinazo hadharisha kuwepo kwa machafuko katika maandamano ya amani mjini Arusha yaliyoandaliwa na chama cha CHADEMA.

Kimsingi nilishangaa kuwepo kwa taarifa hizo saa chache kabla ya siku ya maandamano yenyewe kufika, kama ilivyo kwa wananchi wengi tulio shuhudia jinsi amani ikivurugwa katika maandamano hayo ya amani na jeshi hilo la polisi, tulishangaa na kujiuliza taarifa za ki-intelijensia zilizotolewa na jeshi hilo la polisi zilitoka wapi na ninani huyo mwana-intelijensia wa Taifa hili.

Nipende kuchukua fursa hii kuwauliza wale wenye dhamana ya kulinda amani katika nchi hii, je hakukuwepo na taarifa za ki-intelijensia kwamba mabomu ya Gongo la Mboto yanaweza kulipuka wakati wowote na kusababisha maafa makubwa kwa jamii ya wa-Tanzania? Kama taarifa hizi zilikuwepo (kwa hakika hazikuwepo) walichukua hatua gani? Hivi hawa wana-intelijensia kazi yao ni usalama wa nchi na watu wake au usalama wa CCM na Mafisadi???

Nchi za wenzetu kitengo cha intelijensi kinafanya kazi kubwa hata kuielekeza nchi ki-mwelekeo wa uchumi, kwa mfano nchi kama Marekani inaingia vitani wakati mwingine kwa manufaa ya kiuchumi, lakini kwa bahati mbaya sana hapa kwetu kitengo hicho kimejisahau kiasi kwamba majukumu yake sasa ni kukilinda chama tawala (CCM) na mafisadi wake huku wanachi wakiangamia kwa mabomu (Mbagala & Gongo la Mboto), njaa, ufisadi, ukosefu wa elimu bora, umeme, nk.

Kwa elimu ya kawaida, bila kuhitaji kuwa na ujuzi wa ki-intelijensia, ghala za mabomu karibu na makazi ya watu ni hatari kubwa, na kwa nchi makini yenye viongozi makini tahadhari kubwa ingekuwa imeshachukuliwa mapema, lakini kwakuwa viongozi wetu si makini tuendelee kusubiri matukio ya namna hiyo kutokea tena na tena, kwani bila kuwa na utashi wa kiutawala hakuna mabadiliko katika hili. Pangekuwepo na utashi wa kiutawala leo tungesikia angalau kiongozi mmoja akijiuzulu kwa tukio hili ila cha ajabu wanaomba ushirikiano kwa wananchi.. ushirikiano upi jamani toka kwetu??

Wa Tanzania tufungue macho, utawala wetu umejisahau hasa kushughulikia masuala ya wananchi na kujikita kuulinda utawala ili utawale milele... Mbagala ingekuwa mwisho lakini mambo yanajirudia.
 
Sasa bado maghala ya silaha POLISI na FFU.
Bado kuambiwa kuna upotevu mkubwa wa AK47 na Makasha elfu kadhaaa ya Risasi.
Tutapata haberi za kuyeyuka kwa mabomu ya kurushwa kwa mono na Rocket Launcher.

Hata magari makubwa ya jeshi nadhani mengi yameshwa uzwa kwa waasi na maghaidi wa Congo na Sudan.

Hivi karibuni Tutegemee kulipuka kwa kiwanda cha Risasi kule Ngerengere.

SIASA potofu huzaa Serikali haramu na watendaji wa ovyo.
Sitegemei chochote cha maana kutoka katika idara yeyote ya serikali ya CCM kwa sababu CCM chama kilichounda serikali hiyo ni Dhaifu mno.

Mwenzetu Dr Slaa alisha yaona haya na mengine mengi mabaya yajayo kutoka mikononi mwa serikali ya CCM,akatugawia maono yake.

"Kuchagua CCM ni kuchagua Maafa"
 
Back
Top Bottom