Milioni 400 Kumng’oa Feisal Yanga

Smart codetz

Senior Member
Jan 25, 2023
180
703
C95DFBE1-51DC-480F-9D9B-1E68EB490BF7.jpeg
A
WAKATI vigogo waliowahi kuongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakifichua kwamba sakata la Feisal Salum ‘Fei Toto’ linacheleweshwa na mchezaji mwenyewe na TFF haiwezi kulimaliza bila kuwepo kwa mazungumzo ya mchezaji na klabu yake, wameeleza kama Yanga italazimika kumuuza, basi dau lake halitazidi Sh 400 Milioni. Hata hivyo, baadhi ya makatibu wakuu wa TFF kwa nyakati tofauti, Selestine Mwesigwa na Aden Rage (wakati ikiitwa FAT) kwa nyakati tofauti wamefichua kwamba, wanaomshauri Feisal ndiyo tatizo kwenye sakata hilo ambalo ni jepesi na mchezaji huyo hazuiwi kuondoka.

Rage alisema, Feisal kuingiza Milioni 100 kwenye akaunti ya Yanga halikuwa suluhisho la yeye kuondoka kwani hajui klabu inataka nini.

“Arudi Yanga akae nao mezani kwanza, inaweza ikamwambia hata Milioni 50, yeye kuomba TFF ili aondoke pia si suluhu japo ni kweli TFF ina mamlaka, lakini haiwezi bila kuwepo kwa mazungumzo ya Yanga na mchezaji,” alisema Rage.

Alisema Feisal anapaswa kuwa mkweli kwa Yanga, aeleze ni klabu ipi anahitaji kwenda na Yanga haiwezi kukataa kumuuza akifafanua kwamba dau lake halitakuwa zaidi ya Sh 400 milioni.

“Kama wakati anasainishwa ilikuwa ni milioni 100, sasa thamani imepanda haitokuwa chini ya milioni 350 hadi 400 kwa klabu inayomtaka kumnunua, Yanga wakiweka hesabu za ajabu, Fifa wanaweza kuingilia na utaratibu huko hivyo,” alisema Rage.
 
Fei & Co wanajua iwapo atauzwa kwa milioni 350+,hatoweza kupata zile stahiki alizoahidiwa itakuwa Ni kichekesho Bora angebaki Yanga na kujadiliana nao.na ameshanyea kambi Yanga wameshika mpini sasa.na umuhimu wake unapungua mechi baada ya mechi klabu inayomtaka inajaribu kupora stahiki za Yanga na kumpa Fei kumrubuni.kama Yanga wananunua wachezaji kwa kufuata taratibu naamini viongozi hawataruhusu kupoteza fedha kwa kuondoka chini ya thamani halisi.hakuna free agent waweke mzigo simple, au subiri may 30,2024.he will be available as free agent
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom