Milele

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
Ni miaka mingi, mingi sana iliyopita katika ufalme wa bahari Kule kilipoishi kitu pekee nilichokipenda sana. Kwa jina Malaika. Naye aliishi bila wazo lolote zaidi ya kupenda na kunipenda mimi.
Nilikuwa mtoto nae alikuwa Mtoto
Kule katika ufalme wa bahari
Lakini tulipendana Kwa upendo uliozaidi upendo, mimi na Malaika wangu.
Kwa upendo ambao malaika wa mbinguni waliufunika na mabawa yao.
Na hii ndio iliokuwa sababu hapo zamani sana
Katika ufalme wa bahari,
Upepo ulikuwa mkuu na kutisha usiku wa mwisho wa malaika wangu. Radi na ngurumo za ajabu, watu wakubwa waliotuzidi walimchukua malaika wangu na kumtupa baharini
Katika ufalme wa bahari.
Malaika wa mbinguni hawakuwa na furaha tena, wao walikuwa wakitembea nasi mahali pote katika ufalme wa bahali.
Ndio, hii ndio sababu ambayo watu wote waliijua katika ufalme wa bahari, kwamba upepo tu ulikuja usiku na kumchukua Malaika wangu, kumuua na kumpoteza mbali katika ufalme wa bahari. Lakini penzi letu lingali hai na imara kushinda upendo wa wote walio wakubwa kutuzidi,
Labda Kwa malaika wa mbinguni, sio Kwa mashetani wa chini ya bahari ya ufalme wa bahari ambao kamwe hawatoweza kuitenganisha roho yangu kutoka katika roho ya Mrembo malaika wangu.
Mwezi hauwezi kuandama bila kumbukumbu na njozi ya Mrembo malaika wangu na yote kila usiku nakaa, natizama chini moyoni mwangu, kwa mpendwa wangu, mpendwa Mrembo malaika wangu,
Kutoka katika ufalme wa bahari, maisha yangu yamekuwa na ningali Mkubwa na mrefu sasa, hapa katika ufalme wa bahari. Nikisimama na kutizama na kukumbuka kilicho tokea miaka mingi iliopita katika ufalme wa bahari. Tukitenganishwa na mamilioni ya maili ndani ya ufalme wa Bahari.
 
Mhh bado sijang'amua kitu hapa.
Ila nahisi hizi mvua zinazoendelea kunyesha Zinaweza kuwa chanzo!!?

Oky ngoja nitafute maana kwanza nitarudi.
 
nimeanza kusoma commet za wadau kabla ya kusoma uzi wenyewe... nimegundua kumbe hata mimi sitaelewa.. acha nisepe zangu!!!!
 
Back
Top Bottom