Mila gandamizi dhidi ya wanawake wa Kichagga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mila gandamizi dhidi ya wanawake wa Kichagga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shelute Mamu, Apr 6, 2011.

 1. S

  Shelute Mamu Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kuona kuwa mpaka leo hii kabila la Kichagga linawakandamiza wanawake katika familia zao. Wiki iliyopita nilishuhudia familia moja ikimfukuza dada yao ambaye hakubahatika kuolewa na kulazimika kuendelea kukaa kwenye mji wa wazazi wake. Lakini kaka zake kwa kushirikiana pamoja walimlazimisha kuondoka pale nyumbani pasipo kujali atakwenda kuishi wapi? na kwa nani! Si huyu tu bali wako wengine ambao wamefukuzwa nyumbani kwa kisingizio kwamba hawajaolewa na pale siyo kwao. Wanawake wasioolewa wanaitwa (WALIFU) kwa kichagga cha SIHA.

  Lakini kinachosikitisha zaidi Wazee na Jamii ya SIHA inakubaliana na jambo hili. Nafikiri sasa umefika wakati kwa jamii kuondoa hii mila potofu ya unyanyasaji wa jinsi hii. Naamini ndani ya Jamii Forum kuna Waandishi, Wanasheria naomba wasaidie suala hili.
   
 2. A

  Anold JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Hizo ni baadhi ya mila potofu zinazopigwa vita. Hao waliomfukuza ni wahalifu kama wahalifu wengine, na tabia hii imekuwa sugu kwa badhi ya maeneo ya mkoa wa kilimanjaro, cha msingi huyo dada ni kupeleka suala hili kwenye serikali ya kijiji kwa kuanzia na kama ataona hana msaada wowote, kabla ya kukimbilia mahakamani kudai haki yake, amuone mkuu wa wilaya na kumweleza hayo yaliyomkuta, maagizo ya mkuu wa wilaya kwa watendaji wa kata yanaweza kumsaidia kuokoa muda. aidha ajaribu kuwasiliana na taasisi kama TAWLA au WILAC naamini atapata msaada wa kisheria ili safari yake ya kwenda mahakamani iwe ya kishindo.
   
 3. S

  Shelute Mamu Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru sana kwa ushauri wako, isipokuwa hao Serikali ya kijiji eneo hilo ni hao hao wanaounga mkono ukandamizaji huo.
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  shule bado hazijatuoa kwenye utumwa wa fikra
   
Loading...