Mikutano ya kampeni ya CCM ina mantiki yoyote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikutano ya kampeni ya CCM ina mantiki yoyote

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TIMING, Oct 3, 2010.

 1. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu mie ni mdau wa nchi yangu na ni mpenzi sana wa bongo

  For the last 4 weeks nimekua naangalia sana habari za mikutano ya kampeni na nimepata wazo mbadala kidogo kuhusu impact ya mikutano ya CCM, nijuavyo mimi kampeni ni kuvutia watu wakuchague

  sasa napata shida kuona kwamba katika mikutano ya CCM, zaidi ya asilimia 90 ya wanaohudhuria, tayari wanakua na nguo za CCM, sasa je kuna haja tena ya kumkampenia mtu aliyekwisha kupa kura yake????? kuna mantiki ipi kwenda kutoa ahadi kwa aliyekwisha kupa moyo wake?

  isnt it a waste of time and resources??
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Acid,
  Mimi nadhani CCM inataka kuonyesha kwamba bado ni maarufu nchini na kuwashawishi wapiga kura wanaosita kuipigia tena kura. Kwa sababu ukiangalia kulikuwa na sababu gani za kuchapisha na kusambaza mapicha ya Jakaya Kikwete, mabango, na ma-t shirt ili hali huyu jamaa anafahamika Tanzania nzima? Ingetosha tu kuweka mabango ya kuwakumbusha wapiga kura waichague CCM lakini si kutumia dola millioni 2 kuchapisha mabango Canada kumtangaza mtu ambaye tayari anafahamika. Kikwete angekuwa na utendaji mzuri Ikulu, hivi sasa all he had to say ni kwamba nipe muhula mwingine ili tuendeleze yale mazuri tuliyoyaanzisha. Lakini hamna, kwa hiyo lazima wasambaze t-shirts, kanga na kugawa shilingi elfu moja elfu mbili na malori ya kusomba watu.
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hojayako ina mantiki
  yaani hakuna mantiki kwa CCM wanavyoenenda
   
 4. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  Ni mapenzi ya wananchi wenyewe kwenda kwenye mikutano wamevaa kijani.. sawasawa na kwenda kwenye kampeni ukiwa tayari ushafanya maamuzi na umebeba bango "hatudangayiki"..
   
 5. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Ujanja wa CCM wagundulika


  na Mwandishi wetu, Dodoma


  [​IMG] MBINU chafu za Chama cha Mapinduzi (CCM), zinazotumika katika kukusanya na kujaza watu kwenye mikutano ya mgombea urais wa chama hicho, zimegundulika baada ya baadhi ya walimu wa shule za msingi mjini Dodoma kutoboa siri.
  Ilibainishwa jana mjini Dodoma, kuwa agizo limetolewa kwa walimu wote walioko kwenye shule zilizoko kwenye mji huo, kuhudhuria kampeni za mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kesho; huku onyo likitolewa kwa watakaoshindwa kuhudhuria kuwa watawajibishwa.
  Kwa mujibu wa baadhi ya walimu waliozungumza na Tanzania Daima, walimu wakuu wa shule walipokea ujumbe kutoka kwa waratibu wa elimu wa kuwataka watoe matangazo kwa walimu wao kuhudhuria mkutano huo bila kukosa.
  Walimu hao, walisema baada ya kupewa tangazo na walimu wao wakuu walihoji na kuambiwa kuwa ni agizo kutoka kwa waratibu wa elimu.
  Mbali ya walimu, agizo hilo limewalenga wanafunzi wa darasa la tano na la sita kwa baadhi ya shule kutokana na wanafunzi wa darasa la saba kuhitimu shule wiki chache zilizopita.
  Baada ya kupata habari hizo, Tanzania Daima ilitembelea baadhi ya shule na kuzungumza na walimu na baadhi ya wanafunzi ambao walikiri kuwepo kwa hali hiyo, huku wengine wakidai hawajaelewa wanakwenda kufanya nini kwenye kampeni hizo. Kwa upande wa wanafunzi waliozungumza na Tanzania Daima katika shule za Makole, Medeli na Nkuhungu, walisema wametangaziwa na walimu kuwa wafike nje ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma majira ya saa 8 siku ya Jumapili bila kukosa.
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  saa nane usiku iweje? ili wapewe chai? au mnaji awafanyia dawa za kufikia vizuri siku ya kupiga kura?
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  WASTED :llama:
  ccm hawawezi ikajaza watu amabo hawajajiandikisha au hawana haki ya kupiga kura katika malori! sasa si itakuwa wanajinganya wenyewe.. kama ikiwakusanya watu na malori toka sehemu za mbali! TATIZO NINI?!! inabeba waje wasikilize sera then inarudisha au wewe ulitaka watembee kwa miguu

  ALAFU HIYO ADD. YA Gazeti la Sayari unalipia!
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Of course it is
   
Loading...