Mikopo ya masomo kwa wanafunzi wa PhD iko wapi mkurugenzi?

mwamola

Senior Member
May 28, 2012
109
15
Habari ya mapumziko ya sikukuu ya kuzaliwa Yesu kristo na kuelekea mwaka mpya wa 2013.

Nakuandikia habari hii kutokana na hali iliyopo katika utoaji wa fedha za wanaosoma shahada za Uzamili na Uzamivu kuwa mbaya, usioeleweka, wenye ucheleweshaji mkubwa, na wenye kuambatana na majibu mabaya toka kwa maafsa wanaohudumia idara hizo.

Ni wiki moja tu imepita tangu majina machache wanafunzi hao hasa wanaondelea (continuing students) yalitolewa katika moja ya chuo wakasaini. Inadaiwa waliodahiliwa kwa mwaka 2012/2013 bado mnaprocess maombi yao tena maafsa wako wanadai maombi hayo hata mezani kwao hayajafika isipokuwa kwa wale walioamua kwenda BODI makao makuu kufuatilia walau wameambiwa maombi yataanza kushughulikiwa mwisho wa mwezi February, 2013. ilipoulizwa ni kwa nini, maafsa wanajibu kuwa KWA NINI NYIE WANAFUNZI WA UZAMILI NA UZAMIVU msitumie mishahara yenu kujisomesha?

Maafsa wanaenda mbali zaidi kudai kuwa licha yakutaka wanafunzi hao watumie mishahara yao, wanashangaa kuona tunafuatilia pesa hiyo wakati wanafunzi hao wana mishahara, kwani UNDERGRADUATES wote wanaokopeshwa hawana mishahara kwa maana kuwa hawajajiriwa? Ama kile vyuo vikuu kilipofanaya mazungumzo nanyi na kukubaliana wanafunzi hawa wasomeshwe na BODI mlilenga kuwapa wanaosoma shahada hizo huduma ama majibu yakashfa kama yanavyotolewa na maafsa wako?
Maafsa wako wanalipwa mshahara na posho mbalimbali kwa kejeli hizo ama kwa Utumishi bora? Maafsa wako wanadai kuwa wanafunzi hao form zao zinakasoro, mmoja wa alieelezwa kuwa hajapata mkopo huo kwakuwa form yake inautambulisho wa Afsa asie Deputy Vice Chancellor (Planning, Finance and Administration). Najiuliza, Barua ya utambulisho hutolewa na DVC-PFA ama na Afsa aliepewa jukumu hilo. Kibaya zaidi mwanafunzi huyo alipouliza mbona BODI haijawahi kumtaja katika majina yaliyotolewa na BODI kuwa form za wanafunzi fulani zina kasoro, Afsa huyo alijibu kuwa hiyo ilikuwa SAMPLE tu. Mkurugenzi, kwa wale amabo hawajeenda huko na majina yao haya kuwekwa kwenye mtandao, tunaomba OFISI yako iyatoe yote wenye kasoro warekebishe.

Mwisho, OFISI yako ilipokubali kutoa mkopo kwa wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu naamini haikulazimishwa kiasi kwamba inahamishia hasira hizo kwa wanafunzi hawa nakuanza kuwasanifu kuwa wanamishahara wajisomeshe.
TUNAOMBA MKOPO HUO MAANA KAMA OFISI YAKO HAIKUTAKA KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI HAWA MNGETOA TAARIFA NA SERIKALI ISAIDIE KUTOA MIKOPO HIYO MAANA WANAFUNZI HAWA HAWATAWEZA KUWEKA KAMBI BODI KUDAI PESA HIYO NA KIBAYA ZAIDI ELIMU YAO MNATAKA IWEJE?
 
mkuu inawezekana una point ila hujui kujielezea hebu fuguka vzr ni mkurugenzi gani?? na litaka mkopo wa nn na ni muda gani umepita hamjapata.
 
Hayo majibu siyo ya ofisi ni ya mtu binafsi ambaye anaflustration zake tena nayeye anatamani kwenda kusoma lakini nafasi hiyo haapewa.
 
Khaaaaaaaa,achane zenu nyie yani hata nyie wa PhD mnalilia mikopo toka HESLB,Mi nawashangaa sana waachieni madogo mikopo nyie mjisomeshe wenyewe na kama huna ela waache wenye ela wajisomesha,UNDERGRADUATE kibao hawajapata hiyo mikopo afu nyie PhD mnalia kabisa.....!Nyie si mna ajira au,sasa mikopo ya nini au mnafikiri mnapewa bure,kama huwezi kujisomesha kausha tu kwani kila mmoja anakula kulingana na urefu wa kamba yake,HUSITAMANI VITU VIKUBWA WAKATI HUNA UWEZO,........HUYO AFISA ANAEKUJIBUNI HIVYO NAMPA BIGUP,MNATAKA NINYI TU NDO MFAIDI INCHI HII,ACHENI UNDERGARDUATE WAPATE MIKOPO KWANZA THEN NDO NINYI PhD...........
 
Back
Top Bottom