Mikopo ya Biashara: Jinsi ya kuipata na usimamizi wake

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,504
5,539
Habari za wakati huu ndugu,

Wengi tunafahamu kuhusu Mikopo, kuna wanaokopa vyakula dukani kwa mangi, kuna wanaokopa mikopo ya mishahara, magari, nyumba au hata biashara katika benki na taasisi nyingine. Kuna pia wanaokopa mali kwa ajili ya biashara au uzalishaji.

Katika biashara yoyote ile njia rahisi na haraka ya kukua ni kwa kupitia mikopo.

Mikopo ipo ya muda mfupi au mrefu ipo ya masharti nafuu na masharti magumi. Ipo mikopo inayojidhamini na pia ipo mikopo inayodhaminiwa kwa rasilimali nyinigine. Kwa kawaida watu wengi wanaokopa huwa wanasahau mambo mawili yamsingi sana kuhusu madeni ambyo ni kama ifuatavyo:

Jambo la kwanza ni kwamba KUKOPA ni HARUSI na kulipa ni MATANGA. Jambo la Pili dawa ya DENI ni kulipa

Kwa kawaida ukishatambua haya mawili na kuyaishi mikopo haitakusumbua lakini leo nataka nizungumze katika mtazamo wa kifedha(Financial Management aspect juu ya Madeni na mikopo)

Katika biashara na makampuni huwa kuna kitu kinaitwa DEBT VS EQUITY MIX ASSET VS DEBT etc ambavyo vinalenga aidi katika kumsaidia mjasiriamali kuamua achukue mkopo kiasi gani na kwa masharti gani. Mara nyingine wajasiriamali hushawishika kudanganya katika taarifa zao za fedha ili tu waweze kupata mkopo mkupwa zaidi ila wanachosahau ni kujiambia na ukweli halisi na kujiandaa namna ya kuhakikisha kwamba ukweli wao utaweza kuhimili deni husika.

Bahati mbaya kabisa ni kwamba katika kudanganya huku wengi hujikuta wakiingia katika madeni ya gharama kubwa.Gharama kubw aya madeni iko katika RIBA na jinsi inavokokotolewa.Kwa mfano RIBA ambayo iko fixed ni hatari sana kwa biashara kuliko riba ambayo inakuwa inapungua kulingana na salio la PRINCIPAL. Kwa wale ambao wanataka kuelewa zaidi PRINCIPAL ni kle kiasi cha PESA ulichopewa na RIBA ni kile kiwango cha ziada unacholipa.Sasa mara zote tafuta mkopo unaokokotolewa kwa njia ya reducing balance na uulize na uone na uelewe hio reducing inakokotolewaje.

Vile vile wengine hupotea katika eneo muda wa mkopo,mfano mkopo wa zaidi ya Mwaka mmoja huwa na expensive zaidi katika biashara hasa kama hautakuwa mjanja katika kunegotiate RIBA kuliko mkopo wa mwaka mmoja.

Vile kiwango kinachotumika kukotoa RIBA ya mkopo hasa pale unapoambiwa 3% per month inabidia uulize iwapo ni reducing na inakokotolewa kila mwezi ili uone kwa mwaka ni kiasi gani kwani unaweza ambiwa unapewa RIBA 3% kwa mkopo wa milioni 10 kwa mwezi ulipe kwa miezi 6 ambyo ni kama laki 3 kwa mwezi ili kama sio reducing utalipa riba ya milion 1.8 kwa miezi 6 ambayo ni sawa na 18% Deni likifika mwaka inakuwa 36% ambayo ni sawa na milioni 3.6.

Ukiwambi rejesho lako kwa mwezi ni milioni 1130000 unaona ni ndogo ila kiuhalisia unapigwa sanakwa sababu kwa kila milioni unatakiwa uingize faida isiyopungua laki 2 kila mwezi.Kutengeza hii faida ni rahisi sana kusema wakati unaomba mkopo ila kama wewe ni mfanya biashara unaelewa ugumu wake hasa ukitoa na matumizi mengine ya kibiashara na gharama za uendesha na kodi.

Jambo lingine linasumbua katika mikopo ni kubadilisha matumizi ya mkopo mara baada ya kuupata.Kubadilisha matumizi ya mkopo hasa ambayo ni ya mhemuko hupelekea kufanya maamuzi ambayo hayana faida kibaishara ana ambayo huna taarifa sahihi

Mjadala huu ni endelevu nitaendelee kuongezea nyama lakini pia nakaribisha michango na wadau wengine
 
Mkopo (Leverage)

(1). Ratio ya assets vs liability inatakiwa iwe minimum 2:1 meaning, lazima uwe na sources mbili au zaidi za pesa ndio uchukue mkopo mmoja au hela ukopayo iwe nusu ya asset (2).Mkopo mzuri ni ule ambao unawekwa kwenye biashara zinazoweza ku service huo mkopo na sio kulipa kwa jasho na damu eg from salaries.

(3). Invest mkopo according to PLANS not product or procedure. Plans ndio speed governor ya financial instruments yoyote. Usikope kama huna plans.
 
Back
Top Bottom