Mikopo ya Benki na Matumizi Sahihi kwa Watumishi

Mtoa mada hongera kwa kutoa ushauri mzuri. Hofu yangu ni hii tu; inawezekana kwa upande wako unatokea familia yenye unafuu wa kipato! Nikimaanisha huna wategemezi! Hivyo kwa sababu hiyo, unaweza ukafanya hiyo saving!

Ila kwa wale wenzangu na mimi wanaotokea familia maskini; unaanza tu kazi, unakabidhiwa mdogo wako kuanza kumsomesha; Bado utume hela ya matumizi kwa wazazi; Kwa hali hii useme eti utaweka hela akiba itakua ni kujidanganya!

Ishu nyingine ni hii ya kuoa/kuolewa! Mkishaingia kwenye maisha haya ya kuanzisha familia, hakuna namna lazima utajenga tu maana ni wanawake wachache sana wanaoridhika kuishi nyumba za kupanga! Wengi wanataka kuishi kwenye nyumba zao.

Hivyo wacha tukope ili tujenge kwanza. Baada ya hapo, tukija kukopa tena basi tutafanya biashara kwa ajili ya kujiingizia kipato cha ziada nje ya mshahara. Binafsi sioni kama ni tatizo kubwa kuitwa baba mwenye nyumba badala ya kuitwa baba mwenye gari.
Huyo kaongea tu kujifurahisha unafikiri ni rahisi kuweka saving kwa mishahara hii yetu mtu una mke watoto waende shule hujalipa kodi ya nyumba hamjala wote nyie kila siku ndo maana watumishi wana madeni hayaishi ni ngumu sana kuweka savings labda kama ni bachelor au umetokea familia ya kitajiri sana
 
Ni wachache sana wanaoweza kuwa na mawazo ya hivi na wakayatekeleza.

Wakati naanza kazi yeyote ambaye angeniambia nisinunue gari ningemwona kichaa, leo hii natamani ningepata mentor mapema wa kunipa ushauri wa kipi kianze kipi niache.

Kuna watu kibao wanaingia sana kwenye mitego ya mikopo, na mwisho wa siku hata kazi zinakuja kuwa mbaya.

Tukope kwa matumizi sahihi.
mwanzo tunakuwa na kaulimbukeni. ukishalizoea gari + gharama zake na kudaiwa juu. unaanza kujuta bora mkopo wako ungefanyia jambo lingine la kukuongezea kipato.
 
Mkuu mimi ninaamini kwenye try and error. Aliyekopa na kuharibu atakuwa amejifunza kuliko ambaye hajawahi kukopa kabisa.

Watu tunaaminishana kwenye savings ni nani akiyewahi kusave pesa kwa miaka 10 mfululizo bila kuvunja kibubu chake!

Mkuu mambo ni marahisi ukikaa nyuma kibodi na kucharaza maandishi ila maandishi hayohayo ukiyapeleka filidi yanakusaliti.

I think you are not getting my point, au una escape plan mambo yanapokuwa mabaya.

Chukulia mfano wa mtu aliyesomeshwa na mzazi ambaye ni mkulima, first born anapewa majukumu ya kuangalia wadogo zake, kuwaangalia wazazi na baadhi ya ndugu.

Hapo ukiharibu umeharibu pakubwa, recovery inabaki kutegemea Neema za Mungu.
 
Pia Naomba kama kuna mtu anaweza nisaidia namna ya kuacha kazi Serikalini ila nina mkopo Bank sijui inakuwaje. Natanguliza shukrani
 
Umezungumza kitu nilichotaka kukiandika kwenye comments, jinsi dependent families zinavyoathiri mfumo.

Kukopa ili ujenge, I support you 100%. Tahadhari nayokupa ni moja, hakikisha hela unayokopa inatosha kumaliza zoezi.

Ili, ukishamaliza unahamia moja kwa mmoja, kukwepa gharama za kupanga.

Otherwise ukikopa hela ambayo hutamaliza ujenzi, utajikuta unalipa interest benki, unalipa rent mahali ulipopanga na nyumba kule inakupa pressure maana unaweza kujikuta huiendelezi hata ndani ya miaka 3 na inaanza kuharibika.

Kopa mkopo unaotosha kumaliza ujenzi.

Mkuu mimi nina zaidi ya miaka 10 kwenye ajira ya serikali hivyo nilishajenga kitambo tu kupitia mkopo wangu wa pili wa benki! Ule wa kwanza kama ilivyo kwa vijana wengi, nilinunulia gari (corolla kwa enzi zile, nilitisha sana).

Sema tu kuna jamaa hapo juu (bossless) ameelezea point yenye tija pia. Kuna baadhi ya watumishi wanaumia kwa sasa baada ya kukopa ili wajenge halafu kwa kutokujua, wakajenga majumba makubwa aidha kwa kuiga au kushindwa kuitafsiri ramani!

Mwisho wa siku nyumba imeshindwa kukamilika, halafu wanalipishwa deni na riba juu! Hapa lazima uuchukie ujenzi. Jambo la msingi ni kuanza na nyumba ndogo ya kawaida (ikibidi mabanda ya uwani) itakayotosheleza mahitaji ya pesa uliyokopa then unahamia kwako! Baadae ikishatulia, ndipo ujenge nyumba ya kustaafia. Mimi nilifanya hivyo na sijutii kwa hayo maamuzi yangu.
 
Sure mkuu kujenga kunamaliza hela halafu nikitathimini faida yake sioni kama ipo kwa wastani wa miaka 5 au 6 ya kwanza.
Ukiiwekeza mahali ni vyema coz itazaa. Iliyozalishwa ndio unajengea.
Sawia kabisa, jijengee kwanza msingi wa kiuchumi ndio ukajenge. Ama ninaweza kununua gari likawa ndio la kazi na hilo hilo likawa la kulia bata.
 
Nilikuja kupiga hesabu nikagundua kukimbilia kujenga nyumba ni hasara sana. Kama ilivyo kununua gari.
Cha kufanya jibane nunua kiwanja then kiache maana ardhi inapanda thamani.
Sasa basi ni heri uanzishe biashara au mradi wowote ambao ukitoa gharama za uendeshaji wastani itakuingizia 20 kwa siku Hata ikiwa 15 si mbaya. Kwa mwezi unaweza kupata 400 - 500 ( nb: hata hii pesa kuitengeneza kwa mwezi si rahisi inahitaji bidii sana)
Hii pesa sasa + na uliyosave kwenye mshahara ndio unaweza kuchagua kama unaanza kujengea au kugharamia usafiri. Ila itakuchukua wastani miaka miwili hadi mitatu ya kuhustle
Nilipoanza kazi kwasababu ya maisha niliyotoka nilijibana na kuanza ujasiriamali wa kilimo cha mbogamboga, nashukuru baada ya mwaka nikasave na kufanikiwa kupata kiwanja, nikakomaa mwaka unaofata nilihakikisha napata matofali nakweli nashukuru nilipata.
Mwaka uliofata mambo yakawa magumu magonjwa na baadhi ya mambo yalinitinga. Nikaendelea tu na harakati zangu, mwaka jana nilipata hela nikaanza ujenzi rasmi now nipo kwenye lenta, nataka nimaliza kupaua then ndio niingie bank nikachukue mkopo nimalize kibanda changu.
Nashukuru mambo yangu yanaenda bila kukwama wala familia haimenyeki sana na ukali wa maisha kwa kuwa vitu kama mchele, maharage, viazi mviringo natoa shamban kwangu.

N.b; Kujenga kwa hela ya mkopo peke yake utapata tabu sana kuna mfanyakazi mwenzetu hata vitafunwa huwa vinampiga chenga alikopa jengo halikuisha pesa imeisha na maisha magumu anasubiri mkopo uishe arudi tena bank, nilipata somo.
 
My first job ilikuwa ni benki, I was very fortunate kuwa kwenye department ambayo at least it was giving some bonuses, kwa hiyo hata ukikopa, ndani ya mwezi kuna add-ons ambazo zinafidia.

Lakini jamaa zangu wengi sana walijikuta wako very fixed, hapo ni kuanza kutafuta kazi nje, mawazo kila siku, ugomvi na mabosi kuomba nyongeza za mishahara nk nk.

And then nikaja nikahamia kampuni ambayo ni Consulting, most of the companies na individuals tuna tatizo la kuitumia mikopo kwa malengo tofauti na ya awali au yale tuliyopanga, ukishabadili matumizi ya mkopo, hata marejesho yatakusumbua.

Nikajikuta kazi zangu nyingi zikawa ni kutoa ushauri juu ya matumizi ya mikopo, ila kazi ilikuwa ngumu sana, maana unakuwa rated kulingana na response za clients.
 
Mkuu mimi nina zaidi ya miaka 10 kwenye ajira ya serikali hivyo nilishajenga kitambo tu kupitia mkopo wangu wa pili wa benki! Ule wa kwanza kama ilivyo kwa vijana wengi, nilinunulia gari (corolla kwa enzi zile, nilitisha sana).

Sema tu kuna jamaa hapo juu (bossless) ameelezea point yenye tija pia. Kuna baadhi ya watumishi wanaumia kwa sasa baada ya kukopa ili wajenge halafu kwa kutokujua, wakajenga majumba makubwa aidha kwa kuiga au kushindwa kuitafsiri ramani!

Mwisho wa siku nyumba imeshindwa kukamilika, halafu wanalipishwa deni na riba juu! Hapa lazima uuchukie ujenzi. Jambo la msingi ni kuanza na nyumba ndogo ya kawaida (ikibidi mabanda ya uwani) itakayotosheleza mahitaji ya pesa uliyokopa then unahamia kwako! Baadae ikishatulia, ndipo ujenge nyumba ya kustaafia. Mimi nilifanya hivyo na sijutii kwa hayo maamuzi yangu.
yaah hii nayo point, una kiwanja unaanza hata na servant kota kwanza.
 
Ni wangapi wa aina yako wenye akili hiyo?

Matumizi sahihi ya mkopo, hicho ndicho kikubwa.

Wanasema kopa kwa sababu maalumu.
 
Pia Naomba kama kuna mtu anaweza nisaidia namna ya kuacha kazi Serikalini ila nina mkopo Bank sijui inakuwaje. Natanguliza shukrani

Vumilia tu yataisha. Usikimbie tatizo. Unless otherwise uwe tayari umeshapata mahali pengine ambapo ni bora zaidi ya hapo ulipo. Ila usije ukasema lengo nikalime! Unaweza ukalima ukiwa bado unafanya hiyo kazi yako.

Nb: Najua tu salary slip itakua ina mkeka mrefu wa makato na hivyo yamekukatisha tamaa! Vumilia tu aisee! Au nenda kwa waajiri wako ukawaambie lengo lako, watakupa utaratibu mzuri wa kuacha. Huna sababu ya kutoroka.
 
Wahindi hawajengi nyumba sijui Chanika, Mapinga na huko Goba kwenu ila wao ndo mabilionea wa Wazalendo Star kutwa kukopa kopa.
#tusipangiane#
 
Sure mkuu kujenga kunamaliza hela halafu nikitathimini faida yake sioni kama ipo kwa wastani wa miaka 5 au 6 ya kwanza.
Ukiiwekeza mahali ni vyema coz itazaa. Iliyozalishwa ndio unajengea.
Inategemeana mkuu, ni namna mtu alivyojipanga na mikakati yake.
 
Mkuu mimi ninaamini kwenye try and error. Aliyekopa na kuharibu atakuwa amejifunza kuliko ambaye hajawahi kukopa kabisa.

Watu tunaaminishana kwenye savings ni nani akiyewahi kusave pesa kwa miaka 10 mfululizo bila kuvunja kibubu chake!

Mkuu mambo ni marahisi ukikaa nyuma kibodi na kucharaza maandishi ila maandishi hayohayo ukiyapeleka filidi yanakusaliti.
Hii ya saving ni uzushi mkuu ķwenye mtu ordinary,mfn unasav lak kila mwez itakuchukua miaka mingi kufanya mln 5 na muda plus thamañ ya vitu itakua imepanda.Mim nilvyoanza kaz nılîkopà nikanunua plot thaman iliyopo kwa ss nisingeweza kununua.
So far ushaur ni mzur but sio kuchukua km ulivyo koz hatuna formula moja ya maisha.
 
Last week kuna mdau alizungumzia kuhusu kufanya maamuzi ya kuacha kazi ili akapige mishe zingine mtaani, kwenye mjadala ikaibuka point ya makato ya mikopo kuwa mikubwa kiasi cha kusababisha net kuwa ndogo kiasi cha kutokidhi mahitaji.

Nikawaza kwamba hili tunaweza kulijadili kama topic inayojitegemea.

Hii itawahusu zaidi wale wanaoanza kazi kwa mara ya kwanza, baada ya kutokea vyuoni. Ingawa pia hata wale ambao tuko makazini tayari na tumeshauingia huu mtego tunalo la kujifunza na kuangalia namna sahihi ya kudili nalo.

Unapoanza kazi kunakuwa na changamoto kuu mbili, makazi na usafiri; hizi ndizo kwangu nimeona kama ndizo hasa zinaongoza kwenye mlolongo wa mahitaji.

Nitaiandika kwa kutumia mfano wa kijana wa kiume ambaye ameanza kazi na Gross Salary ya Tshs 1,000,000/- kila mmoja ataiweka kulingana na mazingira yanayomhusu.

Gross ya 1m makato ya NSSF ni 100,000, kodi ni 150,000/- kwa hiyo jumla ya makato ni shilingi 250,000/- bila kuweka Loan Board. So, take home ni 750,000/-.

Familia zetu nyingi, kijana anapoanza kazi anatakiwa kuondoka nyumbani kwenda kukaa kivyake, pia kuna wale tunaotokea mikoa tofauti na tulipopata kazi hivyo zoezi la kupanga linahusika.
Kwa net ya 750,000/- unaweza kupanga chumba kimoja chenye self-contained kwa 100,000-150,000 kwa mwezi maisha yakaenda. Hapo ndani ya mwaka mzima utajikuta una zoezi la fridge, makochi, redio, TV, nk. Matumizi ya kila siku ni yaleyale, msosi, nauli, mavazi, kwa wale wa moja moto moja baridi pia.

Soon mawazo ya gari ama kiwanja yanakuja kichwani, maana unajikuta washkaji wana magari wewe unazunguka on foot, au washkaji wanakwambia issue za kununua kiwanja ili ujenzi uanze. Hizi pia zinakuwa influenced na wapenzi (partners), unapoanza kazi na ukawa na mshahara mzuri, ndicho kipindi cha kutafuta mtu au cha kuwa na mtu ambapo mnaweza hata kutoka mkaenda sehemu za starehe, za kupunga upepo au ukamnunulia baadhi ya vitu, swala la usafiri linakuja pale ambapo mnalazimika kupanda daladala wakati mmependeza, hapo utaanza kuona umuhimu wa kutafuta gari.

Mawazo ya kununua gari au kiwanja yakishakuja, kwa mshahara huo na matumizi niliyoyataja, uwezekano wa kwamba umesevu 5m za ndani ya miaka hata 3 ni ngumu, hivyo, unaamua kwenda benki kukopa.

Kwa net ya 750,000/- bank unaweza kupata mkopo wa shilingi 14,500,000/ na makato ya mwezi yatakuwa ni around 370,000/- kwa rate ya 18%. Maana yake hapo utabaki na net isiyozidi 400,000/-.

Kazi ni kwako, ununue gari 10,000,000/- au ununue kiwanja. Kwa options zote mbili hakuna lenye faida;-
  • Ukinunua gari, tayari una makato ya 350,000/-, gari kwa mwezi linakula zaidi ya 150,000/- na siyo gari la biashara, hapo tayari umeshajipa kifungo cha miaka 5 cha kuhangaika na gari na mkopo, unaanza kuwaza nyongeza za mishahara, ulipo huongezewi unaanza kutafuta kuhama kazi, unajikuta ndani ya miaka 5 huna kazi uliyoweza kui-master kwa sababu hutulii sehemu moja ukajifunza.
  • Ukinunua kiwanja ukaanza kujenga, hiyo hela haitoshi kumaliza nyumba, hivyo utakuwa unakaa kusubiri top up ili uendeleze, kumbuka pango linakudai, makato ya benki yapo yanakudai pia. Frustrations za nyongeza za mishahara zinaanza, unajikuta matumizi pia yanazidi. Pressure zinakupeleka kule kule kuanza kutafuta kazi.
Kuna exceptions, kuna wale ambao kazi zao zinawapa nafasi ya kupata allowances katikati ya mwezi na hivyo maisha kusonga.

Nini cha kufanya:
Saving, hii ni kitu muhimu sana, mfano ukijiwekea malengo ya kusema nitanunua gari/kiwanja bila mkopo, unafanya saving mdogo mdogo bila pressure, hata kazi unakuwa unaipenda na uko likely ku-grow kwa sababu akili yako umeiweka hapo.

Kuna wale wenye minds za entrepreneurship, kopa fanya biashara ambayo unajua itakuwa inarudisha makato ya benki na unabaki na faida kiasi, baada ya muda unaweza kufanya vitu vikubwa. One thing to note, business is not everyones’ cup of tea.

Kuna umuhimu wa kupata ushauri kwa watu mbalimbali na kuufanyia upembuzi ili ikitokea ukaamua kuchukua mkopo iwe ni kwa matumizi sahihi ambayo hayakuingizi kwenye kukufix.
Nafungua mjadala wa nini kinaweza kufanyika ili kuepukana na hili janga la kujifix kwenye mikopo ya benki na kuishia kuiona kazi ni chungu, maana mwezi mzima unafanyia makato tu.
Umeongea ukweli mtupu
Nna ndugu zangu wanakumbana na hili tatizo..mmoja kamaliza juzi mkopo bank, ilikuwa wa miaka mitano..take home aliyokuwa anapata inasikitisha

Huu ujumbe utamfaa sana
 
I couldnt agree more...
 
Back
Top Bottom