Hata wewe umeeleza point mkuu
Mkuu mimi nina zaidi ya miaka 10 kwenye ajira ya serikali hivyo nilishajenga kitambo tu kupitia mkopo wangu wa pili wa benki! Ule wa kwanza kama ilivyo kwa vijana wengi, nilinunulia gari (corolla kwa enzi zile, nilitisha sana).
Sema tu kuna jamaa hapo juu (bossless) ameelezea point yenye tija pia. Kuna baadhi ya watumishi wanaumia kwa sasa baada ya kukopa ili wajenge halafu kwa kutokujua, wakajenga majumba makubwa aidha kwa kuiga au kushindwa kuitafsiri ramani!
Mwisho wa siku nyumba imeshindwa kukamilika, halafu wanalipishwa deni na riba juu! Hapa lazima uuchukie ujenzi. Jambo la msingi ni kuanza na nyumba ndogo ya kawaida (ikibidi mabanda ya uwani) itakayotosheleza mahitaji ya pesa uliyokopa then unahamia kwako! Baadae ikishatulia, ndipo ujenge nyumba ya kustaafia. Mimi nilifanya hivyo na sijutii kwa hayo maamuzi yangu.