milangomitatu
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 1,469
- 1,166
Huyo kaongea tu kujifurahisha unafikiri ni rahisi kuweka saving kwa mishahara hii yetu mtu una mke watoto waende shule hujalipa kodi ya nyumba hamjala wote nyie kila siku ndo maana watumishi wana madeni hayaishi ni ngumu sana kuweka savings labda kama ni bachelor au umetokea familia ya kitajiri sanaMtoa mada hongera kwa kutoa ushauri mzuri. Hofu yangu ni hii tu; inawezekana kwa upande wako unatokea familia yenye unafuu wa kipato! Nikimaanisha huna wategemezi! Hivyo kwa sababu hiyo, unaweza ukafanya hiyo saving!
Ila kwa wale wenzangu na mimi wanaotokea familia maskini; unaanza tu kazi, unakabidhiwa mdogo wako kuanza kumsomesha; Bado utume hela ya matumizi kwa wazazi; Kwa hali hii useme eti utaweka hela akiba itakua ni kujidanganya!
Ishu nyingine ni hii ya kuoa/kuolewa! Mkishaingia kwenye maisha haya ya kuanzisha familia, hakuna namna lazima utajenga tu maana ni wanawake wachache sana wanaoridhika kuishi nyumba za kupanga! Wengi wanataka kuishi kwenye nyumba zao.
Hivyo wacha tukope ili tujenge kwanza. Baada ya hapo, tukija kukopa tena basi tutafanya biashara kwa ajili ya kujiingizia kipato cha ziada nje ya mshahara. Binafsi sioni kama ni tatizo kubwa kuitwa baba mwenye nyumba badala ya kuitwa baba mwenye gari.