Mikopo Vs wanafunzi shule binafsi.

Mikopo Vs wanafunzi shule binafsi.

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
525
Reaction score
2,951
Mara ya kwanza kabisa, niliwahi sikia kauli ya namna hiyo kwa katibu wa wizara ya elimu mstaafu "Maimuna Tarishi " akisema kama umesoma private school hupati mkopo.

Kauli hii tuliipinga vikali, kipindi hiko . na tukasema sio fair sababu .

1.gharama za chuo ni kubwa (Ada, hela ya kula ,copy, usafiri,hela ya malazi, hela ya mafunzo kwa vitendo field). Ni tofauti kabisa na fedha ya ada shule ya private laki 8,au mil 1 ambayo pia watu husoma kwa ada hiyo private. Kuwanyima mkopo ni kuwakatishia Ndoto zao kabisa.

2.pia nakumbuka tulihoji kuwa uwezo wa mzazi haupo constant, mfano. Kipindi mtoto akiwa anasoma private mzazi alikuwa na uwezo wa kulipa ,kipindi mtoto anaingia chuo baba au mzazi amepata magonjwa, ameparalyze, amefirisika, kumnyima mkopo mtoto huyu ni kumkatishia malengo yake.

3.pia tulihoji juu ya kama mtoto amesoma kwa kudhaminiwa inakuwaje, kuna wanaodhaminiwa kusoma private schools na mashirika binafsi, watu binafsi, na husomeshwa shule tuu sio chuo, baadaye hutelekezwa chuo wajitegemee. Hii bodi ya mikopo walisema wataweka kipengele kuambatanisha vielelezo vya udhamini ,ila huwa ni geresha tuu huwa hawatoi hata uambatanishe .ndio maana sio sahihi kutoa mkopo kwa kigezo cha u private schools, au u government schools. Sio fair.

4.tulihoji pia wapo waliosoma kwa kuresit mitihani kutafuta credits Mara nyingi hawa huwekwa katika kundi la private schools,wapo QT (qualified Tests), wapo diploma wote hawa huwa termed as private schools. Kuwanyima mkopo kwa vigezo hivi ni kupoteza ndoto zao.

Kigezo cha kutoa au kutotoa mkopo kwa kuangalia ulisoma private au government sio kigezo sahihi. Kime katisha ndoto za wanafunzi wengi saana sababu hakitoi majibu halisi ya uwezo wa mwanafunzi kustahimili gharama.

Hakuna kipindi bodi ya mikopo wanakusanya makusanyo na marejesho
Kama kipindi hiki, tuwaasi bodi ya mikopo hiki kigezo hakifai.

Kama Bodi ya mikopo wataamua kukitumia kama kigezo cha kukosa mkopo, basi tunawaomba waandike katika muongozo wao wa 2018/2019 .wakiongeze kuwa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo"ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo. Itasaidia Sana hii kama ikiwa inaeleweka.

Abdul Nondo.
 
Hii kauli imenisikitisha sana. Ni ya kibaguzi na haikupaswa kutolewa na mtu ayeapa kuilinda na kuhifadhi Katiba ya nchi inayoeleza watu wote ni sawa.
Kwa nn tunaanza kuwabagua.!?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Waacheni watoto wa maskini wapate mikopo

Nimeshuhudia mtu asiye na shida yoyote aliyesoma private za mamilion maisha yake yote akipewa mkopo 100% na wazazi wake wakimpa pesa za kutosha miaka yote chuoni...mwisho akawa hana matumizi zaidi ya kulewa pombe kila siku

Huku classmet mwingine mtoto wa masikini akikosa mkopo, na kuishia kuwa na matumaini ya kuappeal kila siku huku darasa tukimchangia changia ili asifukuzwe shule
 
Hujamuelewa vizuri mleta mada
 
Kuna siku waliozaliwa private hospital hawatatibiwa government hospital.
Kwenye maisha kuna kupanda na kushuka sio kwamba kusoma private ndio ukwasi .
Mbona kuna watu walishakua hadi mawaziri halafu wanaomba msaada kusaidiwa matibabu hospitali.
Inabidi kufanya uchambuzi hili kuakiki wahitaji swala sio umesoma wapi?
 
Na ukizingatia kwa asilimia kubwa wanafunzi waliokuwa vyuoni wengi wao wametoka private, na hata shule za serikali za high school wanategemea idadi kubwa wanafunzi kutoka private. Ni ubaguzi usio na tija wala Afya kwa maendeleo ya taifa.
Hata ukijaribu kuangalia idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi wengi wao wana msingi wa kutoka private sasa sijui kwa idadi ya kiasi gani cha wainjinia, madaktari na kada zingine za kisayansi tunaweza kuwapata kutoka shule za umma hasa o'level. Kuna baadhi ya shule za serikali za o'level tangu zianzishwe hazijawahi kutoa mwanafunzi kwa mchepuo wa sayansi hadi sasa.
Kwa hili serikali itafakari upya huo mtazamo kwa kweli..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mimi naona mnaenda mbali sana, logic ni hivi:- Serikali ina uwezo wa kuwachukua wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba? Tuanzie hapo, ikishindikana ndio kuna ulazima wa wananchi kuingia mtaani sasa, ili kuiangusha hii serikali batili.
 
Waacheni watoto wa maskini wapate mikopo

Nimeshuhudia mtu asiye na shida yoyote aliyesoma private za mamilion maisha yake yote akipewa mkopo 100% na wazazi wake wakimpa pesa za kutosha miaka yote chuoni...mwisho akawa hana matumizi zaidi ya kulewa pombe kila siku

Huku classmet mwingine mtoto wa masikini akikosa mkopo, na kuishia kuwa na matumaini ya kuappeal kila siku huku darasa tukimchangia changia ili asifukuzwe shule
Unaleta Liwaya kwenye mambo ya muhimu kuliko yote duniani.
 
Ukitaka hasara na umaskini maishani mwako basi itegemee serikali
 
Mara ya kwanza kabisa, niliwahi sikia kauli ya namna hiyo kwa katibu wa wizara ya elimu mstaafu "Maimuna Tarishi " akisema kama umesoma private school hupati mkopo.

Kauli hii tuliipinga vikali, kipindi hiko . na tukasema sio fair sababu .

1.gharama za chuo ni kubwa (Ada, hela ya kula ,copy, usafiri,hela ya malazi, hela ya mafunzo kwa vitendo field). Ni tofauti kabisa na fedha ya ada shule ya private laki 8,au mil 1 ambayo pia watu husoma kwa ada hiyo private. Kuwanyima mkopo ni kuwakatishia Ndoto zao kabisa.

2.pia nakumbuka tulihoji kuwa uwezo wa mzazi haupo constant, mfano. Kipindi mtoto akiwa anasoma private mzazi alikuwa na uwezo wa kulipa ,kipindi mtoto anaingia chuo baba au mzazi amepata magonjwa, ameparalyze, amefirisika, kumnyima mkopo mtoto huyu ni kumkatishia malengo yake.

3.pia tulihoji juu ya kama mtoto amesoma kwa kudhaminiwa inakuwaje, kuna wanaodhaminiwa kusoma private schools na mashirika binafsi, watu binafsi, na husomeshwa shule tuu sio chuo, baadaye hutelekezwa chuo wajitegemee. Hii bodi ya mikopo walisema wataweka kipengele kuambatanisha vielelezo vya udhamini ,ila huwa ni geresha tuu huwa hawatoi hata uambatanishe .ndio maana sio sahihi kutoa mkopo kwa kigezo cha u private schools, au u government schools. Sio fair.

4.tulihoji pia wapo waliosoma kwa kuresit mitihani kutafuta credits Mara nyingi hawa huwekwa katika kundi la private schools,wapo QT (qualified Tests), wapo diploma wote hawa huwa termed as private schools. Kuwanyima mkopo kwa vigezo hivi ni kupoteza ndoto zao.

Kigezo cha kutoa au kutotoa mkopo kwa kuangalia ulisoma private au government sio kigezo sahihi. Kime katisha ndoto za wanafunzi wengi saana sababu hakitoi majibu halisi ya uwezo wa mwanafunzi kustahimili gharama.

Hakuna kipindi bodi ya mikopo wanakusanya makusanyo na marejesho
Kama kipindi hiki, tuwaasi bodi ya mikopo hiki kigezo hakifai.

Kama Bodi ya mikopo wataamua kukitumia kama kigezo cha kukosa mkopo, basi tunawaomba waandike katika muongozo wao wa 2018/2019 .wakiongeze kuwa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo"ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo. Itasaidia Sana hii kama ikiwa inaeleweka.

Abdul Nondo.
Kiongozi upo?
Pole Na maswahiba
 
Yuko mwingine amekwenda mbali zaidi anashauri wanaodahiliwa vyuo visivyo vya serikali (yaani private) wasipewe mikopo.
 
Hatari sana, tunakokwenda Mungu peke yake ndio anajua.
 
Mambo mengine yanasikitisha sana...

Kuna mambo ya kutetea, ila kuna mengine ni too much...

Kama serikali haina pesa, ni vizuri kuweka bayana, ila siyo kubagua...

Cc: mahondaw
 
Ukipitia vifungu vya utoaji wa mikopo kutoka bodi umefafanua kwamba kama ulisoma kupitia udhamini au mzazi amepata ulemavu njia ya kufuata kuambatanisha fomu zinazothibitisha hilo ili huweze kuwa na vigezo vinavyohitajika.
 
Back
Top Bottom