Mikopo elimu ya juu-uchungu/machozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikopo elimu ya juu-uchungu/machozi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mkombozi, Jan 20, 2009.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana JF na watanzania wenzangu. Mimi jana nilitoa machozi ya uchungu. Mimi nimesoma pale UDSM miaka ya nyuma, nikafikiria sana kuendana na familia yetu kua ya hali ya chini sana, ingekua kipindi hicho ndio tunavyoshuhudia yanayofanyika pale Chuo Kikuu basi nisingesoma kabisa.

  Wanafunzi wanachukuliwa kama wahamiaji kwenye nchi yao. Licha ya ukweli kwamba kuchangia elimu ya juu linafanywa na mataifa mengi lakini inatupasa kuangalia mazingira ya kwetu. Mimi nadhani ni Muda muafaka wa kuwapa mikopo wanafunzi wote kwa 100% halafu serekali iweke mazingira mazuri ya kukusanya hiyo mikopo kwa watakaomaliza. Kufukuza wanafunzi zaidi ya 2,000 kwa sababu tu hawajaweza kuchangia garama za helium haiingi akilini..

  Kwa hali za wazazi wetu walioko huko vijijini kumsomesha mtoto wa UDSM hataweza kabisa, sasa uchukulie kwa mfano ana watoto wawili au watatu. Kijijini watu wanakula mlo mmoja tu, mwenye nacho mchana hushindia uji wa ndimu leo hii unamwambia achangie elimu ataweza?

  Wazazi wengi hutegemea kilimo lakini sehemu nyingi mvua zimekua haba na udongo umechoka hata wakipata mazao kidogo ni kwaajili ya kukidhi mahitaji ya nyumbani kwa miezi kadhaa tu. Mimi nadhani ifikie sehemu viongozi wetu wakumbuke mazingira walioyokulia, tena zamani kulikua na unafuu zaidi ya sasa.

  Maprofessor, Mawaziri, Madirector, watunga sheria, wabunge, wafanyakazi mbali mbali na wasomi wa inchi hii tusisahau tulikotoka. Elimu imekufanya umepata chochote cha kuweza kumsomesha mtoto na kutunga sera za kuchangia mikopo elimu ya juu na kusahau kwamba ulisoma bure na pia kunamkulima anashindia uji wa ndimu.

  Watanzania wengi hwana ajira kwa KULAZIMISHWA, yaani anaamka asubui na ana nia ya kufanya kazi lakini hakuna kazi za kuzalisha mali. Inanisikitisha sana.

  Wanafunzi wanateseka na watu tunakaa kimya bila kuwatetea, akiteswa mtoto wa jirani kesho keshokutwa atakua wako au mjukuu wako.

  Hija yangu ni kwamba wanafunzi wote wapewe mikopo kwa 100%, hela za EPA zipelekwe kutoa mikopo elimu ya Juu. Serikali iweke mezingira mazuri ya mtu akimaliza na pindi tu anapopata ajira aanze kulipa mara moja.

  NAOMBA KUWASILISHA HOJA
   
Loading...