Mikopo elimu ya juu: Serikali yaweka vikwazo kupunguza waombaji ili kukidhi ahadi ya 100%

Shikulaushinye, Sasa unatetea ujinga kwanini?! Mwanao mwenyewe siyo mjinga alifaulu sana na nampongeza sana. Nilidhani ingekuwa bora ukatetea wanafunzi wenye ufaulu kama mwanao ndio wapewe kipaumbele. Kuna haja gani kujisumbua na wajinga wakati kuna wanafunzi wanaofaulu vizuri kama mwanao?! Wanafunzi wanatakiwa kupewa changamoto ili wasome.

Naona umenikosoa na kunipa sifa ambazo sikuwahi kuzipitia. Hayo maisha sikuwahi ishi. Mimi nilisoma Azania. Sikuwa nakaa hostel. Nilikuwa nakaa kijijini. Kwa wanaoijua Dar es Salaam watakubaliana nami kuwa miaka ya 80 mpaka 90, Kinyerezi hakukuwa na usafiri wowote zaidi ya kutembea kwa miguu mpaka majumba sita ama banana ambapo usafiri wa daladala ulipatikana mpaka kariakoo shule ya uhuru. Kutoka shule ya uhuru mwanafunzi alitembea kwa miguu mpaka Azania. Siku zote za wiki niliamka saa kumi na nusu kujiandaa, saa kumi na moja nipo njiani nakimbia kuelekea majumbasita kupanda daladala.

Miaka yote ya O level na A level nilisoma kwa mtindo huo. Na nilisaidiana na wazazi kutafuta karo. Na bado sikupata ufaulu wa ajabu kabisa huu mnaoutetea!!

Nakubaliana na wewe kitu kimoja kikubwa sana. Ni kweli wanafunzi waliosoma kwenye shule za serikali zamani ni wale waliofaulu tu. Yaani wenye akili. Zamani hizo ni kweli shule zilikuwa na walimu wazuri ambao nao walikuwa wamefaulu pia. Mwalimu mwenye akili alijisikia fedheha sana mwanafunzi kufeli somo lake. Siku hizi walimu ni wajinga pia na ndio hao mnaowatetea. Mwalimu anaona kufeli kwa mwanafunzi haimhusu maana Hata yeye mwenyewe ni mjinga. Hatutaki tuendelee kuzalisha ujinga.Wanafunzi wasome.

Enzi zetu ingawa alama ya mwisho kwenda chuo ilikuwa CD. Bado tulikuwa tunaonywa na walimu kukaza buti kwasababu ya ushindani. Kuna miaka wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi walipokuwa wengi, wenye CD waliachwa. Sasa vyuo vimekuwa vingi uzembe umeongezeka.

Wanafunzi wanakesha kwenye Twitter, YouTube, Facebook, whatsap nk kupigasoga tu, hawasomi. Unawatetea Nini lakini?! Hawa ni wajinga walazimishwe kusoma.

Jirani kuna shule ya kata, wanafunzi wanazagaa tu wanavuta bange kwenye majumba yaliyosimama ujenzi. Nililazimika kutumia nguvu ya ziada kuwasaidia walimu kwa kuleta kikosi cha polisi kuweka doria eneo jirani na shule. Sasa wajinga kama hawa nao mtu anawatetea. Wanafunzi wasome.
Kuna wanafunzi Kutoka shule za kata wanafanya vizuri. Tuliona mfano mwaka jana na mwaka huu. Hivyo mwanafunzi akiamua kuachana na anasa akaamua kusoma anafaulu na atasoma chuo kikuu kwa mkopo asilimia 100.
 
Soma ufaulu kijana... Hakuna Urahisi katika Fedha ya serikali ya JPM. Vigezo na masharti kuzingatiwa
 
Kuna mahali tulikosea sana katika mfumo wetu wa elimu. Inabidi tujifunze toka Ujerumani na hata Japan. Wanaweka mkazo sana kwenye Technical Colleges na sio Vyuo Vikuu. Watu wanajifunza taaluma fulani.

Tumekuwa na kasumba ya kila mtu kutaka kupata elimu ya Chuo Kikuu. Tulifika mahali tukashusha hata ufaulu ili watu wengi zaidi waende Chuo Kikuu. Tulipotoka sana, na tunahitaji kurekebisha hilo.

Mfano kwenye masomo ya uchumi na biashara, tunahitaji CBE nyingi zaidi kuliko wahatimu wa Chuo Kikuu kwenye fani hizo.
Tatzo mfumo tuliojengewa technical colleges hazina uzito compare to Uni, lakini ukiangalia ujuzi na maarifa wa mambo wanatofautiana Sana hasa wakikutana maeneo ya field
 
Hivi unajua kua mtihani unapima uwezo wa mwanafunzi kwa asilimia 20 tu? Kama haujui fuatilia

Pili kujua uwezo wa mtu ni sawa na kufanya research inabidi uwe na vyanzo vingi vya kukuletea data kwakua elimu yetu ni aina ya elimu inayotutengezea vyeti vya kuombea kazi basi sishangai kuona hili unalitetea

Mtu anasomea uhasibu anapelekwa field miezi mitatu kwa mwaka na kila anapoenda field anaanza kujifunza upya kama shule hakuwa akifanya kitu japo mitihani amepata A ama B+

Kwanini tusianze kubadili elimu yetu kuwa ya vitendo ili kutengeneza magwiji katika maeneo yao ya elimu?

Ndio maana leo unakuta mtu ana taaluma fulani lakini anakuja kupewa maelekezo yasio ya kitaalam na mtu mwingine anafuata hajiamini kwakua aliamini mitihani zaidi ya kujifunza
Hili Si tatizo la elimu ya hapa kwetu tu bali karibu sehem nyingi ulimwenguni. Mie mwenyewe ni muhanga wa siku ya mtihani maana niliumwa ghafla kwenye somo moja lakini hiyo haiondoi mtihani kuwa kipimo. Tatizo linaanzia kwenye mitihani kukosa ubunifu na hivyo kuwanyima wanafunzi ubunifu. Unakuta msahihishaji anang'ang'ana na marking scheme, na kutokuwa flexible. Tutengeneze elimu yenye kupima ambayo hata kama itapimwa kwa vitendo, huo pia ni mtihani. Mtihani utabaki kipimo.
 
Nakubaliana na wewe lkn siamini km mwanafunzi wa chuo kushindwa au kuonyesha umahili wake tatizo ni ufaulu wake wa kidato cha 6. kuna maprofesa wengi hawakufanya vizuri secondary lkn wakaamua kurudi kujipanga upya kwa kusoma checti, diploma na sasa ni walimu wa vyuo vikuu.

Tatizo la wanafunzi wa vyuo kuwa weupe ni njia ya ufundishaji wa vyuo vikuu, Tanzania tunaangalia sana kufaulu mitihani unavyotetea badala ya practical na continuous assessment; Mwanafunzi anasoma SUA kozi ya uvuvi na ufugaji samaki/aqual culture lkn mpaka anamaliza hajawahi kufanya practical ya kuangalia hata hilo bwaha linavyochibwa, hajawahi kufika hata ferry, hajawahi hata kwenda deep sea, hajawahi hata kuona vyavu, hakuna mabwawa ya kufundishia, hakuna maabara za samaki, unategemea nini? wenzetu course work pamoja na practical work, reserch na projec zinabeba mark 70% final exams ndiyo 30 sisi huku ni kinyume.

Mwanafunzi wa degree anafanya mtihani wa multiple choice badala ya kujenga hoja kushawishi mwalimu, mwalimu kufundisha ni kama chui na simba, mwalimu analenga kukamata wanafunzi badala ya kuhakikisha wana uelewa. mwalimu anatoa quiz na test zisizo na miguu wala kichwa. wanafunzi wa vyuo vya kibango wanasomea mitihani tu. kwaani asipofanya hivyo atakosa chuo.
Kusema mgawanyo wa assignments na finals unaweza kusaidia, nina mashaka kiasi. Huko kwenye dunia ya kwanza, huwa ni discretion ya mwalimu husika. Pia si kwamba walimu wanawaza kukamata mwanafunzi.
Kumkamata mwanafunzi ni kutunga mtihani Mara mbili na kusahihisha mara mbili. Hakuna mtu anayependa ujinga huo. Lakini multiple choice kwenye final, hilo ni tatizo. Mitihani haikidhi viwango.
Huyo mwanafunzi unayeona ni kawaida kutoweza kuandika atafanyaje kazi zake? Au ndio kibongobongo? Mfumo umeoza huu, hasa baada ya kuanzishwa private universities na loan board bila usimamizi wa kutosha na siasa kuingia.
 
Hili Si tatizo la elimu ya hapa kwetu tu bali karibu sehem nyingi ulimwenguni. Mie mwenyewe ni muhanga wa siku ya mtihani maana niliumwa ghafla kwenye somo moja lakini hiyo haiondoi mtihani kuwa kipimo. Tatizo linaanzia kwenye mitihani kukosa ubunifu na hivyo kuwanyima wanafunzi ubunifu. Unakuta msahihishaji anang'ang'ana na marking scheme, na kutokuwa flexible. Tutengeneze elimu yenye kupima ambayo hata kama itapimwa kwa vitendo, huo pia ni mtihani. Mtihani utabaki kipimo.
Nlispecialize kwenye written exam japo kuna baadhi ya vyuo vina oral exams mfano bugando hii ni nzuri pia ndio maana nikasema tusiwe na conclusion kwenye written exams tu hasa level za chini kama tunataka kuboresha elimu

'many sources of data conclude better outcome'

kupandisha grade haifanyi elimu kua bora kwakua kuna njia nyingi pia za kufanikisha hizo grade zaidi ya kupata kwa kusoma

All in all system nzima ni mbovu ila kama wenye dhamana ya kusimamia elimu wanamalengo ya dhati wanatakiwa kuboresha kuanzia chini kwanza
 
Ndugu yangu pole sana, siku hizi mwalimu kukamata wanafunzi wengi inalipa, sup kila mwanafunzi lazima akate si chini ya 50,000/= mpaka 100,000/= mwalimu ndiyo atafundisha na kuwalengesha mitihani. fikiria mwalimu aliyekamata wanafunzi 100 ana kiasi gani: 100x50,000/= siyo milioni 5? mchezo huu upo Taasisi za elimu ya juu nyingi. sitaki kuzitaja hapa. lakini tukiamua tunaweza kutaja majina mpaka ya walimu wanofanya hivyo.

Walimu ni wavivu, hawataki kusumbua vichwa. Mulptiple choice kwenye Universities examinations zipo amini usiamini. haijarishi ni Test au final exam kwaani hata test baadae ndiyo hutengeneza GPA ya mwanafunzi.
 
Shikulaushinye, Sasa unatetea ujinga kwanini?! Mwanao mwenyewe siyo mjinga alifaulu sana na nampongeza sana. Nilidhani ingekuwa bora ukatetea wanafunzi wenye ufaulu kama mwanao ndio wapewe kipaumbele. Kuna haja gani kujisumbua na wajinga wakati kuna wanafunzi wanaofaulu vizuri kama mwanao?! Wanafunzi wanatakiwa kupewa changamoto ili wasome.

Naona umenikosoa na kunipa sifa ambazo sikuwahi kuzipitia. Hayo maisha sikuwahi ishi. Mimi nilisoma Azania. Sikuwa nakaa hostel. Nilikuwa nakaa kijijini. Kwa wanaoijua Dar es Salaam watakubaliana nami kuwa miaka ya 80 mpaka 90, Kinyerezi hakukuwa na usafiri wowote zaidi ya kutembea kwa miguu mpaka majumba sita ama banana ambapo usafiri wa daladala ulipatikana mpaka kariakoo shule ya uhuru. Kutoka shule ya uhuru mwanafunzi alitembea kwa miguu mpaka Azania. Siku zote za wiki niliamka saa kumi na nusu kujiandaa, saa kumi na moja nipo njiani nakimbia kuelekea majumbasita kupanda daladala.

Miaka yote ya O level na A level nilisoma kwa mtindo huo. Na nilisaidiana na wazazi kutafuta karo. Na bado sikupata ufaulu wa ajabu kabisa huu mnaoutetea!!

Nakubaliana na wewe kitu kimoja kikubwa sana. Ni kweli wanafunzi waliosoma kwenye shule za serikali zamani ni wale waliofaulu tu. Yaani wenye akili. Zamani hizo ni kweli shule zilikuwa na walimu wazuri ambao nao walikuwa wamefaulu pia. Mwalimu mwenye akili alijisikia fedheha sana mwanafunzi kufeli somo lake. Siku hizi walimu ni wajinga pia na ndio hao mnaowatetea. Mwalimu anaona kufeli kwa mwanafunzi haimhusu maana Hata yeye mwenyewe ni mjinga. Hatutaki tuendelee kuzalisha ujinga.Wanafunzi wasome.

Enzi zetu ingawa alama ya mwisho kwenda chuo ilikuwa CD. Bado tulikuwa tunaonywa na walimu kukaza buti kwasababu ya ushindani. Kuna miaka wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi walipokuwa wengi, wenye CD waliachwa. Sasa vyuo vimekuwa vingi uzembe umeongezeka.

Wanafunzi wanakesha kwenye Twitter, YouTube, Facebook, whatsap nk kupigasoga tu, hawasomi. Unawatetea Nini lakini?! Hawa ni wajinga walazimishwe kusoma.

Jirani kuna shule ya kata, wanafunzi wanazagaa tu wanavuta bange kwenye majumba yaliyosimama ujenzi. Nililazimika kutumia nguvu ya ziada kuwasaidia walimu kwa kuleta kikosi cha polisi kuweka doria eneo jirani na shule. Sasa wajinga kama hawa nao mtu anawatetea. Wanafunzi wasome.
Kuna wanafunzi Kutoka shule za kata wanafanya vizuri. Tuliona mfano mwaka jana na mwaka huu. Hivyo mwanafunzi akiamua kuachana na anasa akaamua kusoma anafaulu na atasoma chuo kikuu kwa mkopo asilimia 100.

Aksante kwa hoja kwani hoja hujibiwa kwa hoja, nimecheka kidogo. sitetei viraza lkn chuo Div 1 na 2 haitoshi. nitabaki kutetea watoto wa wanyonge. kwa kifupi alifanya vizuri ni mtoto wa ndg yangu, lkn chini ya usimamizi wangu, wanangu wanasoma huko ST. SECONDARY SCHOOL sina tatizo na nimejipanga kugharimia mpaka chuo hata wasipopata mkopo, lkn naumia kuna watoto wa walala hoi huko kijijini, wengine ni watoto wa ndg zetu, hata hiyo ada ya 40,000/= kwa mwaka wazazi walikuwa wameshindwa mpka baada ya msamaha wa JPM. mazingira ni magumu sana kupata daraja lwa kwanza.
 
Nlispecialize kwenye written exam japo kuna baadhi ya vyuo vina oral exams mfano bugando hii ni nzuri pia ndio maana nikasema tusiwe na conclusion kwenye written exams tu hasa level za chini kama tunataka kuboresha elimu

'many sources of data conclude better outcome'

kupandisha grade haifanyi elimu kua bora kwakua kuna njia nyingi pia za kufanikisha hizo grade zaidi ya kupata kwa kusoma

All in all system nzima ni mbovu ila kama wenye dhamana ya kusimamia elimu wanamalengo ya dhati wanatakiwa kuboresha kuanzia chini kwanza

Kasome vitabu vya primary utachoka, mwandishi ni mjasiliamali aliyeshindwa akamua kujifunza kuandika vitabu, kuna kitabu cha sayansi kinatumiwa na shule nyingi za English media, kwa darasa la kwanza na chekechekea ya pili yaani UKG. kitabu hicho kinasema LIZARD NA FROG ni aina ya insects. Ukienda secondary kila shule ina vitabu vyake. wazazi tunapa shida kweli, unaambiwa nunua vitabu vya OXFORD, mara cha ZANZIBAR, mara VIKAS mara mtunzi fulani yaani ni shida kweli kweli. chuo sasa ndiyo mambo yapo shaghala bagala kabisa, mwalimu anaingia na project kufundisha statistics analysis, Quantitative techniques na nk, vitabu hakuna, walimu na wanafunzi wana GOOGLE maswali ya assignment, wanacopy na paste, hakuna kusumbua kichwa.
 
Hili Si tatizo la elimu ya hapa kwetu tu bali karibu sehem nyingi ulimwenguni. Mie mwenyewe ni muhanga wa siku ya mtihani maana niliumwa ghafla kwenye somo moja lakini hiyo haiondoi mtihani kuwa kipimo. Tatizo linaanzia kwenye mitihani kukosa ubunifu na hivyo kuwanyima wanafunzi ubunifu. Unakuta msahihishaji anang'ang'ana na marking scheme, na kutokuwa flexible. Tutengeneze elimu yenye kupima ambayo hata kama itapimwa kwa vitendo, huo pia ni mtihani. Mtihani utabaki kipimo.

Labda kije kizazi cha walimu wengine.
 
Kasome vitabu vya primary utachoka, mwandishi ni mjasiliamali aliyeshindwa akamua kujifunza kuandika vitabu, kuna kitabu cha sayansi kinatumiwa na shule nyingi za English media, kwa darasa la kwanza na chekechekea ya pili yaani UKG. kitabu hicho kinasema LIZARD NA FROG ni aina ya insects. Ukienda secondary kila shule ina vitabu vyake. wazazi tunapa shida kweli, unaambiwa nunua vitabu vya OXFORD, mara cha ZANZIBAR, mara VIKAS mara mtunzi fulani yaani ni shida kweli kweli. chuo sasa ndiyo mambo yapo shaghala bagala kabisa, mwalimu anaingia na project kufundisha statistics analysis, Quantitative techniques na nk, vitabu hakuna, walimu na wanafunzi wana GOOGLE maswali ya assignment, wanacopy na paste, hakuna kusumbua kichwa.
Ni kweli mkuu lakini swala ni kubadili mambo haya yanayoendelea tunatakiwa kuset curriculum na jinsi ya kumeet that curriculum sio siasa kama ilivyo sasa
 
Labda kije kizazi cha walimu wengine.
Sio ivyo mkuu tunaweza kulaumu walimu lakini sio wao ndio sababu kila mtu anatetea kiti chake

Kuna movie moja nliangalia kuna quote moja nliipenda jamaa alisema "don't ever tell a soldier he did not know the cost of war."
 
Wewe ni kiraza wa kutupa! Mbona viongozi wako wengi wa nchi wamesomeshwa kwa ufaulu huo? Siasa gani kwenye mambo ya msingi? Mbona Kenya,Zambia na Uganda ambao wametuacha mbali kielimu bona wanampokea huyo mwanafunzi mwenye EE au GPA ya 2.7? Mbona china ambao ameanza kuisumbua dunia kiuchumi sasa mbona mwanafunzi akitoka Tz na GPA ya 2.5 wanampokea? Usiwe kiraza au punguani, unakokotwa tu hata huelewi.

Urasa upo aise?
 
Nlispecialize kwenye written exam japo kuna baadhi ya vyuo vina oral exams mfano bugando hii ni nzuri pia ndio maana nikasema tusiwe na conclusion kwenye written exams tu hasa level za chini kama tunataka kuboresha elimu

'many sources of data conclude better outcome'

kupandisha grade haifanyi elimu kua bora kwakua kuna njia nyingi pia za kufanikisha hizo grade zaidi ya kupata kwa kusoma

All in all system nzima ni mbovu ila kama wenye dhamana ya kusimamia elimu wanamalengo ya dhati wanatakiwa kuboresha kuanzia chini kwanza
Tatizo kwa nchi yetu hasa kwenye elimu ya chini ukiingiza tu teachers' assessment km part ya final Basi umekaribisha rushwa.
 
Binafsi nililisema jambo hili mapema nikaonekana kama mnafki anayetetea ujinga, Nia ya serikali haikua kuboresha elimu kwa kupandisha madaraja ya ufaulu. Lengo lilikua kubana pesa na hiyo ndio sababu kuu ya kufanya hivyo,Wangekua na nia hiyo wangefanya maandalizi kwa angalau miaka 3 kuboresha miundombinu na kuwaanda vizuri wanafunzi.

Haiwezekani huyu mhitimu mwenye diploma ya Civil engineering mwenye GPA ya 3.0 amekaa barabarani miaka 7 na uzoefu wa kutosha, sasa anataka kusoma elimu ya juu wewe unamwambia hana vigezo! huo ni uonevu wa hali ya juu.
Kwani ni lazima kila mtu awe shahada?
 
Katika uchaguzi wa mwaka Rais aliahidi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote watakaofaulu kusoma vyuo vya Elimu ya juu. Baada ya Rais kuingia ikulu alijitahidi kutoa mikopo iliyokuwa imekwama kwa muda hivyo kuwapa wanafunzi matumaini.

Baada ya kukaa na kutengeneza budget ya mwaka wa fedha serikali imegundua kuwapa mikopo wanafunzi wote watakaofauru ni ngumu kwaani watakausha hazina yote hivyo serikali kushindwa kutekeleza ahadi nyingine hasa zile ambazo matokeo yake yanaonekana moja kwa moja kama ujenzi wa bara bara, huduma za maji na afya. Baada ya serikali kuliona hili imeamua kufanya yafuatayo:-

· Kuongeza madaraja kuingia vyuo vya elimu ya juu:- kwa sasa ili mwanafunzi aweze kwenda elimu ya juu lazima awe na alama D 2 katika mtihani wake wa kidato cha 6, ambayo ni sawa na daraja la pili. (Division two). Pia kwa wale waombaji wa Diploma lazima wawe na ufauru wa UPER SECOND 3.5 G.P.A

· Halafu ikaweka kipaumbele cha mwombaji kupata mkopo kwa wale waliosoma sayansi kidato cha 6.

Kwa vikwazo hivi serikali tayari itaweza kutoa mkopo kwa waombaji kwa asilimia 100 kwaani ni wachache sana wataoweza kupata mikopo. Nafikiri wengi waliosoma elimu ya juu wanatambua kuwa kupata alama A-D kwenye michepuo michepuo ya PCB, PCM, PGM, CBG siyo kazi nyepesi kwa shule zetu ambazo ambazo zina changamoto nyingi kama ukosefu wa maabala na upungufu wa walimu waliobobea katika masomo husika.

Pia ni ngumu kwa wanafunzi wa Diploma kufaulu kwa daraja la pili la juu yaani UPPER SECOND CLASS 3.5. mfano wanaosoma vyuo vya sayansi ya afya na sayansi nyingine km uhandisi na nk ni vigumu sana kupata alama tajwa.
Wanafunzi someni acheni siasa kwenye elimu siyo kila mtu lazima awe na shahada
 
Nilimaliza siku nyingi labda kama wewe: miaka ya nyuma kulikuwa na kuchaguliwa siyo kufaulu; kuanzia secondary kutoka primary. shule za secondary na vyuo vilikuwa vichache. wengi walikuwa wanafikia vigezo lkn nafasi zilikuwa chache. mfano hata sasa course ya Medical doctror pale MUHAS kama hujafaulu kwa A,A ,A au ,B,B A au BBB huwezi kwenda, unataka kunambia ufaulu wa BCC siyo ufaulu mzuri? sababu ni kwamba nafassi ni chache japo vijana wengi wanafaulu. Mwaka jana kuna kijana wangu alimaliza KIBITI SECONDARY alifaulu kwa Div 2 comb ya PCB. Physics alipata D, Chemistry alipata B, Biology alipata B. alipenda kuwa Doctor, lkn ndoto zake zilizimwa kwani walioomba MUHAS walikuwa zaidi ya 5000 huku nafasi zikiwa 80 tu. waliofanikiwa kupata nafasi ni wale waliofaulu zaidi kwa alama AAA, ABB, BBB lakini pia waliowahi kuomba sasa kijana anasomea kufuga samaki huko SUA tena chagua la pili. Hivyo kipindi unasoma wewe wengi walikuwa wanakidhi vigezo lkn nafasi zilikuwa chache.

Chuo kikuu kilikuwa kimoja tu; UDSM, SUA ilikuwa na shule ya UDSM Huku MZUMBE ikiwa na chuo cha kuandaa wataalamu ktk fani ya uongozi-IDM Mzumbe. Institute of Developement Managment maalumu kwa kutua TECHNICIANS Educations. baada ya hapo Mzumbe ilikuwa kuwa chuo kikuu; nakumbuka mwaka 2002 kipindi hicho vijana wanaomba moja kwa moja chuo, chuo kilikuwa kina uwezo wa kudahiri wanafunzi 1200 tu lakini walioomba walikuwa zaidi ya 20,000 chuo ilibidi kiweke vigezo kuwa ili upate udahili lazima uwe una Div one. je hao wengine hawakuwa na vigezo?

Ilikuwa mwanafunzi akienda kusoma UDSM km vile amepata nafasi ya kwenda mbinguni, kwa sasa kuna vyuo vingi vinavyotoa elimu bora km ya UDSM kama siyo zaidi ya UDSM. UDSM imezidiwa na wanafunzi nasikia wengine sasa wanasimama nje wkt walimu wanafundisha, zamani ukisoma wote mlikuwa mnakaa mpaka viti vinabaki.

Nitarudi ukijibu. ....
Umeongea vizuri, tatizo la sasa hivi hatufuati kitu kinaitwa pyramid structure katika elimu na ni muhim sana katika uchumi na maendeleo ya nchi yeyote ile, miaka tunaingia chuo kikuu (1983) COET , Tanzania nzima tulichaguliwa wanafunzi 74 tu, wenye Ufaulu wa juu kabisa , na wale wa daraja la pili walipelekwa kusoma vyuo vya diploma, kama IFM, IDM ambavyo vilikuwa vinaandaa watu kulingana na matakwa ya wakati huo, UDSM Ilibidi uwe umefaulu kwa ufaulu wa alama za juu sana, siku hizi hata wenye E zote wanasombwa tu , nashauri wangeendelea na utaratibu wa zaman ila sasa wangechaguliwa wa daraja la kwanza na la pili tu, na vyuo view makin katika udahili
 
Kama kuna vyuo vya nje vinavyowapokea kusoma kwao wanafunzi wenye ufaulu wa GPA 2.7 sisi tunawazuiaje? Inawexekana kweli hii inabanwa ili kukifhi matakwa ya mkopo.
 
Back
Top Bottom