mdaharunga
JF-Expert Member
- Sep 25, 2014
- 413
- 396
Shikulaushinye, Sasa unatetea ujinga kwanini?! Mwanao mwenyewe siyo mjinga alifaulu sana na nampongeza sana. Nilidhani ingekuwa bora ukatetea wanafunzi wenye ufaulu kama mwanao ndio wapewe kipaumbele. Kuna haja gani kujisumbua na wajinga wakati kuna wanafunzi wanaofaulu vizuri kama mwanao?! Wanafunzi wanatakiwa kupewa changamoto ili wasome.
Naona umenikosoa na kunipa sifa ambazo sikuwahi kuzipitia. Hayo maisha sikuwahi ishi. Mimi nilisoma Azania. Sikuwa nakaa hostel. Nilikuwa nakaa kijijini. Kwa wanaoijua Dar es Salaam watakubaliana nami kuwa miaka ya 80 mpaka 90, Kinyerezi hakukuwa na usafiri wowote zaidi ya kutembea kwa miguu mpaka majumba sita ama banana ambapo usafiri wa daladala ulipatikana mpaka kariakoo shule ya uhuru. Kutoka shule ya uhuru mwanafunzi alitembea kwa miguu mpaka Azania. Siku zote za wiki niliamka saa kumi na nusu kujiandaa, saa kumi na moja nipo njiani nakimbia kuelekea majumbasita kupanda daladala.
Miaka yote ya O level na A level nilisoma kwa mtindo huo. Na nilisaidiana na wazazi kutafuta karo. Na bado sikupata ufaulu wa ajabu kabisa huu mnaoutetea!!
Nakubaliana na wewe kitu kimoja kikubwa sana. Ni kweli wanafunzi waliosoma kwenye shule za serikali zamani ni wale waliofaulu tu. Yaani wenye akili. Zamani hizo ni kweli shule zilikuwa na walimu wazuri ambao nao walikuwa wamefaulu pia. Mwalimu mwenye akili alijisikia fedheha sana mwanafunzi kufeli somo lake. Siku hizi walimu ni wajinga pia na ndio hao mnaowatetea. Mwalimu anaona kufeli kwa mwanafunzi haimhusu maana Hata yeye mwenyewe ni mjinga. Hatutaki tuendelee kuzalisha ujinga.Wanafunzi wasome.
Enzi zetu ingawa alama ya mwisho kwenda chuo ilikuwa CD. Bado tulikuwa tunaonywa na walimu kukaza buti kwasababu ya ushindani. Kuna miaka wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi walipokuwa wengi, wenye CD waliachwa. Sasa vyuo vimekuwa vingi uzembe umeongezeka.
Wanafunzi wanakesha kwenye Twitter, YouTube, Facebook, whatsap nk kupigasoga tu, hawasomi. Unawatetea Nini lakini?! Hawa ni wajinga walazimishwe kusoma.
Jirani kuna shule ya kata, wanafunzi wanazagaa tu wanavuta bange kwenye majumba yaliyosimama ujenzi. Nililazimika kutumia nguvu ya ziada kuwasaidia walimu kwa kuleta kikosi cha polisi kuweka doria eneo jirani na shule. Sasa wajinga kama hawa nao mtu anawatetea. Wanafunzi wasome.
Kuna wanafunzi Kutoka shule za kata wanafanya vizuri. Tuliona mfano mwaka jana na mwaka huu. Hivyo mwanafunzi akiamua kuachana na anasa akaamua kusoma anafaulu na atasoma chuo kikuu kwa mkopo asilimia 100.