Kwanza mkuu huwezi kujifunza kupitia nchi hizo ulizotaja kwa kua tunatofautiana changamoto na mazingiraKuna mahali tulikosea sana katika mfumo wetu wa elimu. Inabidi tujifunze toka Ujerumani na hata Japan. Wanaweka mkazo sana kwenye Technical Colleges na sio Vyuo Vikuu. Watu wanajifunza taaluma fulani.
Tumekuwa na kasumba ya kila mtu kutaka kupata elimu ya Chuo Kikuu. Tulifika mahali tukashusha hata ufaulu ili watu wengi zaidi waende Chuo Kikuu. Tulipotoka sana, na tunahitaji kurekebisha hilo.
Mfano kwenye masomo ya uchumi na biashara, tunahitaji CBE nyingi zaidi kuliko wahatimu wa Chuo Kikuu kwenye fani hizo.
Kwani mtihani ndio kipimo cha uwezo? Hata wewe unaamini hivyo?Mtoa hoja usilete siasa kwenye elimu. Kuadmit watu wenye uwezo mdogo ni tatizo. Tuiamini mitihani yetu kwenye kutambua uwezo wa wanafunzi. Kama ni lazima kwenda chuo kikuu jitahidi upate alama stahili.
Kwa mwendo wa kuchukua alama E, hapo hapana. Rudia mtihani au tafuta kingine cha kufanya.
kaka umemaliza chuo mwaka gani Miaka ya nyuma kujiunga UDSM LAZIMA UWE NA C,D Kwenda juu DD HULIKUWA HUCHAGULIWI;Katika uchaguzi wa mwaka Rais aliahidi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote watakaofaulu kusoma vyuo vya Elimu ya juu. Baada ya Rais kuingia ikulu alijitahidi kutoa mikopo iliyokuwa imekwama kwa muda hivyo kuwapa wanafunzi matumaini.
Baada ya kukaa na kutengeneza budget ya mwaka wa fedha serikali imegundua kuwapa mikopo wanafunzi wote watakaofauru ni ngumu kwaani watakausha hazina yote hivyo serikali kushindwa kutekeleza ahadi nyingine hasa zile ambazo matokeo yake yanaonekana moja kwa moja kama ujenzi wa bara bara, huduma za maji na afya. Baada ya serikali kuliona hili imeamua kufanya yafuatayo:-
· Kuongeza madaraja kuingia vyuo vya elimu ya juu:- kwa sasa ili mwanafunzi aweze kwenda elimu ya juu lazima awe na alama D 2 katika mtihani wake wa kidato cha 6, ambayo ni sawa na daraja la pili. (Division two). Pia kwa wale waombaji wa Diploma lazima wawe na ufauru wa UPER SECOND 3.5 G.P.A
· Halafu ikaweka kipaumbele cha mwombaji kupata mkopo kwa wale waliosoma sayansi kidato cha 6.
Kwa vikwazo hivi serikali tayari itaweza kutoa mkopo kwa waombaji kwa asilimia 100 kwaani ni wachache sana wataoweza kupata mikopo. Nafikiri wengi waliosoma elimu ya juu wanatambua kuwa kupata alama A-D kwenye michepuo michepuo ya PCB, PCM, PGM, CBG siyo kazi nyepesi kwa shule zetu ambazo ambazo zina changamoto nyingi kama ukosefu wa maabala na upungufu wa walimu waliobobea katika masomo husika.
Pia ni ngumu kwa wanafunzi wa Diploma kufaulu kwa daraja la pili la juu yaani UPPER SECOND CLASS 3.5. mfano wanaosoma vyuo vya sayansi ya afya na sayansi nyingine km uhandisi na nk ni vigumu sana kupata alama tajwa.
Kuna watu wajinga sana! Mnatetea ujinga? Naamini watu waende chuo kwa vigezo hafifu. Someni, acheni uzembe. Kwanza miaka niliyosoma mimi hatukutambua E kama kigezo cha kukupeleka chuo. Vilipoongezeka vyuo binafsi ndipo na hizi E zikawa ni qualification , lakini kwa udhamini binafsi. Kisha likaletwa pendekezo la kuundwa board ya mikopo. Sisi wanafunzi wa UDSM miaka hiyo tuliipinga kwa migomo na maandamano. Tulikuwa na sababu nyingi ikiwemo hii ya kuelekea kukumbatia ujinga. Enzi hizo ulikuwa ukishachaguliwa tu chuo kikuu taayari ushapata udhamini.Hivyo ushindani ulikuwa ni alama za ufaulu.
Wanafunzi tulisoma sana miaka ya nyuma. Leo wanafunzi wamekuwa wazembe wanataka kupunguziwa alama za ufaulu. Tupa kule ******. Tunataka msome
Ulivoandika tu hapa nimepata tathmini kama ungesoma ungepata daraja gani lakini sijashangaaMlibebwa sana watu na E zao walikua vifua mbele chuo kikuu. Huku mtaani graduate wanashindwa hata kauandika application letter. Kuandika CV mpaka wa google
Mkuu hivi lowasa alikufanya nini?Msubirini Lowasa akiingia mtasoma hata kwa division four na mtapewa mkopo asilimia mia..
kaka umemaliza chuo mwaka gani Miaka ya nyuma kujiunga UDSM LAZIMA UWE NA C,D Kwenda juu DD HULIKUWA HUCHAGULIWI;
Kama wewe ni kizazi cha walimu wa voda faster hatutakushangaa
tena tunaomba ufaulu wa C,D URUDISHWE SIO WA D,D;
Magap waliyokuwa wanaangaika kuziba kutokana na kukosa watu wenye sifa ya shazibika ; warudishe ufaulu wa C,D
Kwahiyo tuachane na mitihani na tuwapime kwa vigezo gani?Kwani mtihani ndio kipimo cha uwezo? Hata wewe unaamini hivyo?
Tutengeneze mazingira na kuboresha elimu katika shule za sekondari na Si kushusha viwango vya ufaulu.Kama ni hivyo vyuo vikuu watasoma watoto waliosoma shule binafsi, kama FEZA, MARIAN, ST,ST kwani ndiyo hutoa wanafunzi kwa DIV 1-2 mara nyingi failure huwa ni div 3 tena wachache mmoja au wawili. kwa tuendelee kutengeneza matabaka, in ten years to come watoto wa maskini watakuwa hawana elimu, watoto wa wenye uwezo ndiyo watasoma university. tunajenga nchi ya namna gani? Shule Government za sasa siyo zile za miaka ile ya 90 kurudi nyuma.
Kuna njia nyingi za kupima uwezo wa mwanafunzi nikiwa vizuri ntakuja na majibu kwa upanaKwahiyo tuachane na mitihani na tuwapime kwa vigezo gani?
Tutengeneze mazingira na kuboresha elimu katika shule za sekondari na Si kushusha viwango vya ufaulu.
Ndugu hakuna majibu. Usije na dhana za assignments wala field placements.Kuna njia nyingi za kupima uwezo wa mwanafunzi nikiwa vizuri ntakuja na majibu kwa upana
Kwa bahati mbaya hawana vigezo. Hakuna namna. Hatuwezi kwenda tu kwa kuhofia matabaka. Tutaharibu zaidi. Haya mapambano yangeenda kwenye elimu bora shule za sekondari tungeweza kuona matunda yako. Ungepata fursa ya kuona elimu ilivyovurugwa, ungeshangaa. Mwanafunzi wa chuo kikuu akikuandikia paragraph unafikiria kweli ili uweze kutambua alitaka kusema nini. Tujipange.Tuanze lini? watoto wa wakulima wataenda kuunguna na kazi ya wazazi wao st.secondary schools ndiyo watafikia vigezo vya kwenda vyuo na kupata mikopo.
Kwa bahati mbaya hawana vigezo. Hakuna namna. Hatuwezi kwenda tu kwa kuhofia matabaka. Tutaharibu zaidi. Haya mapambano yangeenda kwenye elimu bora shule za sekondari tungeweza kuona matunda yako. Ungepata fursa ya kuona elimu ilivyovurugwa, ungeshangaa. Mwanafunzi wa chuo kikuu akikuandikia paragraph unafikiria kweli ili uweze kutambua alitaka kusema nini. Tujipange.
Tungejua sababu za kuanzishwa kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
Aiingii akilini mwanafunzi kulipiwa 5M O and A level na mzazi wake akaweza, eti Leo hii amefaulu vizuri then alipiwe 3M na serikali wakati mzazi anaweza kumlipia!
Mna utani nyie na watoto Wa maskini, endeleeni na upuuzi Wa ubafuzi na matumizi mabaya ya madaraka
Hivi unajua kua mtihani unapima uwezo wa mwanafunzi kwa asilimia 20 tu? Kama haujui fuatiliaNdugu hakuna majibu. Usije na dhana za assignments wala field placements.
Lakini sasa ni Dr au siyo? kama jibu ni ndiyo why wanaweka vikwazo kwa watoto wetu huku mazingira ya shule ni mabovu, shule hazina maabala, walimu na nk.