Mikopo elimu ya juu: Serikali yaweka vikwazo kupunguza waombaji ili kukidhi ahadi ya 100%

Na hao wa diploma ambazo hazikufika gpa ya 3.5 watarudia hiyo diploma? Maana yake si hawataweza milele kupata fursa ya kupata digrii?
Kwahiyo kama hawawezi kurudua mitihani tuwape tu fursa ya kuendelea kwa kuwa wana diploma hata kama hawajakidhi vigezo?
 
Aisee hili Taifa lina wajinga wengi ajabu! Kwani mwenye GPA ya 4.9 ndio anaweza kuandika application letter vizuri? Hata wale wenye masters za GPA 4.9 sio wote wanaoweza kuandika application letters kama hujui. Tuko wote maofisini tunaona hata wenye PhD wanavyoboronga. Application leteer ni technical sio shule kiraza wewe.
Ukiona hivyo mtu wa Masters au PhD hawezi kuandika CV rudi kwanza ufuatilie labda PhD ya magumashi, aaendike Thesis au dissertation hasindwe CV, ongea unachoelewa sometimes
 
Bora nilisoma enzi za mkwere boom alitupandishia, poleni sana madogo aisee so sad watoto wa wakulima mtaumia sana
 
Katika uchaguzi wa mwaka Rais aliahidi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote watakaofaulu kusoma vyuo vya Elimu ya juu. Baada ya Rais kuingia ikulu alijitahidi kutoa mikopo iliyokuwa imekwama kwa muda hivyo kuwapa wanafunzi matumaini.

Baada ya kukaa na kutengeneza budget ya mwaka wa fedha serikali imegundua kuwapa mikopo wanafunzi wote watakaofauru ni ngumu kwaani watakausha hazina yote hivyo serikali kushindwa kutekeleza ahadi nyingine hasa zile ambazo matokeo yake yanaonekana moja kwa moja kama ujenzi wa bara bara, huduma za maji na afya. Baada ya serikali kuliona hili imeamua kufanya yafuatayo:-

· Kuongeza madaraja kuingia vyuo vya elimu ya juu:- kwa sasa ili mwanafunzi aweze kwenda elimu ya juu lazima awe na alama D 2 katika mtihani wake wa kidato cha 6, ambayo ni sawa na daraja la pili. (Division two). Pia kwa wale waombaji wa Diploma lazima wawe na ufauru wa UPER SECOND 3.5 G.P.A

· Halafu ikaweka kipaumbele cha mwombaji kupata mkopo kwa wale waliosoma sayansi kidato cha 6.

Kwa vikwazo hivi serikali tayari itaweza kutoa mkopo kwa waombaji kwa asilimia 100 kwaani ni wachache sana wataoweza kupata mikopo. Nafikiri wengi waliosoma elimu ya juu wanatambua kuwa kupata alama A-D kwenye michepuo michepuo ya PCB, PCM, PGM, CBG siyo kazi nyepesi kwa shule zetu ambazo ambazo zina changamoto nyingi kama ukosefu wa maabala na upungufu wa walimu waliobobea katika masomo husika.

Pia ni ngumu kwa wanafunzi wa Diploma kufaulu kwa daraja la pili la juu yaani UPPER SECOND CLASS 3.5. mfano wanaosoma vyuo vya sayansi ya afya na sayansi nyingine km uhandisi na nk ni vigumu sana kupata alama tajwa.
Kweli kabisa...
 
Ukweli suala hili ni kukomoa wanafunzi na wazazi.
Kwanza kupandisha daraja la ufaulu na kutoa masharti kwamba mwanafunzi asipopata D mbili hatoruhusiwa kujiunga na chuo kikuu ilikuwa ni kuwaonea wanafunzi kwa vile matamko hayo yametolewa wanafunzi wakiwa katika vyumba vya mitihani.Serikali lazima wawe na huruma na wanchi wao.Wao wanaotoa matamko hayo wengi wamesoma vyuo vikuu kwa kupata E mbili.Bora wangesema serikali haina pesa wazazi wasomeshe watoto wao kwa pesa zao .Inabidi Rais aingilie kati zoezi hili lisitishwe kwa mwaka huu 2016.
Masharti yote haya lengo kuu ni kupata namba ndogo ya waombaji wa mikopo..ni bora serikali ingesema kuwa watu wenye ufaulu chin ya hyo gpa au hizo alama...ajisomeshe mwenyew wazaz wangeweza kuuza hata mapera kama walivozoea wangewasomesha watoto wao..
 
Ukiona hivyo mtu wa Masters au PhD hawezi kuandika CV rudi kwanza ufuatilie labda PhD ya magumashi, aaendike Thesis au dissertation hasindwe CV, ongea unachoelewa sometimes
Na wewe nae usitie kinyaa humu! Uandishi wa CV sio kipimo cha competency ya mtu wala intelligency ya mtu,elewa tu nacho kuzungumza hapa we ukoje? Uandishi wa CV nzuri ni ufundi tu na ndio maana hua zinatofautiana. Unaweza kwenda hata stationary na PhD yako ukamkuta form four failure akakuandalia CV nzuri kuliko unayoandaa wewe.
 
Masharti yote haya lengo kuu ni kupata namba ndogo ya waombaji wa mikopo..ni bora serikali ingesema kuwa watu wenye ufaulu chin ya hyo gpa au hizo alama...ajisomeshe mwenyew wazaz wangeweza kuuza hata mapera kama walivozoea wangewasomesha watoto wao..
Umeongea ukweli mtu! Hongera sana.
 
Mtoa hoja usilete siasa kwenye elimu. Kuadmit watu wenye uwezo mdogo ni tatizo. Tuiamini mitihani yetu kwenye kutambua uwezo wa wanafunzi. Kama ni lazima kwenda chuo kikuu jitahidi upate alama stahili.
Kwa mwendo wa kuchukua alama E, hapo hapana. Rudia mtihani au tafuta kingine cha kufanya.
Mkuu...
Lengo la kuweka masharti ni kubana matumiz kwa kupunguza namba ya wa nufaika wa bodi ya mikopo...hivi fikiria changamoto za shule za serikali hazina walim.vifaa na miundo mbinu..matokeo yake maskini watabaki nyuma kwa kuwa wao ndo wanaenda kusoma shule za gvt..
 
Nimekuelewa vizuri kabisa vijana tunataka tuwe na elimu kubwa wakati hata zile skills za kuendesha maisha yetu ya kawaida hatuna..
Mfano juzi kati hapa Kuna kijana anahangaika kusoma masters wakati hata nauli ya kufanyia application hana, kiatu kimechanika, sharti limepauka, jasho linatiririka, anahangaika kujaza fomu za mkopo sijui wamehaidiwa kupewa ambao hawakupata enzi wanasoma bachelor....!!
No longer at ease!!!!!!!!!
 
Binafsi nililisema jambo hili mapema nikaonekana kama mnafki anayetetea ujinga, Nia ya serikali haikua kuboresha elimu kwa kupandisha madaraja ya ufaulu. Lengo lilikua kubana pesa na hiyo ndio sababu kuu ya kufanya hivyo,Wangekua na nia hiyo wangefanya maandalizi kwa angalau miaka 3 kuboresha miundombinu na kuwaanda vizuri wanafunzi.


Haiwezekani huyu mhitimu mwenye diploma ya Civil engineering mwenye GPA ya 3.0 amekaa barabarani miaka 7 na uzoefu wa kutosha, sasa anataka kusoma elimu ya juu wewe unamwambia hana vigezo! huo ni uonevu wa hali ya juu.
Mahanju..
Mi nimesoma diploma huwez amini wanafunzi walopata above 3.5..ni only 20%....this is unfair at all
 
Mahanju..
Mi nimesoma diploma huwez amini wanafunzi walopata above 3.5..ni only 20%....this is unfair at all
Na wao wanalijua hilo kwamba ni 20% ndo maana kwenywe kozi utakuta admission capacity ni 5 kwa kozi yenye mkopo. endelea kuisoma namba
 
Binafsi nililisema jambo hili mapema nikaonekana kama mnafki anayetetea ujinga, Nia ya serikali haikua kuboresha elimu kwa kupandisha madaraja ya ufaulu. Lengo lilikua kubana pesa na hiyo ndio sababu kuu ya kufanya hivyo,Wangekua na nia hiyo wangefanya maandalizi kwa angalau miaka 3 kuboresha miundombinu na kuwaanda vizuri wanafunzi.


Haiwezekani huyu mhitimu mwenye diploma ya Civil engineering mwenye GPA ya 3.0 amekaa barabarani miaka 7 na uzoefu wa kutosha, sasa anataka kusoma elimu ya juu wewe unamwambia hana vigezo! huo ni uonevu wa hali ya juu.



Tatizo letu ni kuwa na mtazamo wa kiujamaa mno. Sasa kama serikali haina fedha ya kutosha ifanyeje ili wewe uende chuo kikuu. Tukizingatia haki, basi hapa sehemu kubwa ya lawama lazima irudi kwa wazazi pia. Mzazi kukosa fedha ya kulipia elimu bora ya mwanao siyo tatizo la serikali per se.

Pia, kuongeza kiwango cha ufaulu kwa waombaji wa nafasi za kuingia vyuo vikuu ni vizuri, kuhakikisha wanaoenda vyuo vikuu wamejiandaa vizuri kuingia chuo kikuu. Hakuna alama ya juu ya ufaulu inayowekwa ambayo binadamu hawezi kuifikia. Tatizo langu kwa serikali ni kwamba kuna matatizo mengine mengi pia vyuo vikuu na mashuleni lakini hayatatuliwi ipasavyo, ukiwemo uhaba wa walimu/wahadhiri etc wenye sifa za kufundisha hata hao wanafunzi wachache watakaodahiliwa, na ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunza. Asilimia kubwa ya shule na vyuo vikuu nchini bado havina capacity ya kutoa quality graduates, ukiondoa tatizo la viwango duni vya udahili.
 
Kuna mambo matatu ambayo ya kuzingatia:-
Mahitaji ya nchi (nguvu kazi) hapa bila kupoteza muda ukweli tumeweka nguvu kwa ma graduate kuliko technician.huku mfumo wetu ukitambua technician ndio yuko field na ndo mzalishaji mkubwa ktk kila fani.matokeo yake tumekuwa tukisema vijana hawajui ka I japo wana vyeti bila kujua mitasla iliandaliwa kwa kutegemeana

Uwezo w serikali kugharamia elimu: kutokana na hali halisi yaani pato letu la ndani pamoja na misaada(wote mnajua madeni,ufisadi,vipAumbele na gha
Lama za kuendesha serikali nk) serikali haiwezi kulipia wanafunzi wote wenye vigezo vya kimataifa kuingia chuo kikuu yaani mwenye E mbili hata km tunaongeza mapato inahitaji kujipanga mwishowe unaweza kuchukua wanafunzi wengi mwaka ujao wa fedha pato
likashuka ukai ua maandamano na karaha kwa jamii.

Changamoto za vyuo; vyuo vingi vinaweka

wanafunzi wengi kuliko uwezo wao hivyo hii imekuwa ni kero hata kwa wanafunzi wenyewe.mabweni,kumbi za
mihadhara,maktaba,maabara zimekuwa zikibeba karibia mara mbili ya uwezo wake.wahadhiri hawatoshi vifaa havitoshi mwisho wa siku tunapata mtaalamu wa fani kilaza.hii imesababisha wanafunzi wengi kukomaa na kozi weki ili gpa iwe nzuri ukimleta field shida inaanzia hapo.
Pia hii imesababisha vyuo vya kati kukosa wanafunzi hivyo kila chuo cha kati kufikilia kuanzisha shahada na kupunguza astashahada na stashahada.ambapo baadhi ya wamiliki wa kampuni wameanza kuajiri technician kutoka nje ya nchi kwa kua kwa mfumo tulio kuwa nao shahada sio mzalishaji ni msimamizi,pia tatizo la kuwa na wahitimu wengi wa shshada wakati waajiri hawahitaji shahada nyingi linaleta shida ya ukosefu wa ajira
 
Back
Top Bottom