Mikopo elimu ya juu: Serikali yaweka vikwazo kupunguza waombaji ili kukidhi ahadi ya 100%

Mtoa hoja usilete siasa kwenye elimu. Kuadmit watu wenye uwezo mdogo ni tatizo. Tuiamini mitihani yetu kwenye kutambua uwezo wa wanafunzi. Kama ni lazima kwenda chuo kikuu jitahidi upate alama stahili.
Kwa mwendo wa kuchukua alama E, hapo hapana. Rudia mtihani au tafuta kingine cha kufanya.
Yaani nilitaka kuandika hivi Mkuu siongezi neno kula LIKE KUBWA SANA
 
Ataingiliaje kati wakati yeye ndiye katoa maelekezo hayo? Natamani nifahamu Rais wetu ufaulu wake wa kidato cha 6 ulikuwaje. Pia me siamini GPA kubwa wana uwezo kichwani au uwezo wa kufanya kazi. unaweza kuwa na uwezo kichwani lkn ukasindwa kujiandaa vizuri au mtihani ukaji sehemu ambayo hukusoma. ndiyo maana nchi zilizoendelea course work ina marks nyingi zaidi ya 60% final exams ndiyo 20%-30%.
Kweli ndugu final exam sio kipimo toshaaa Bali hzo course work ndio kipimo kikubwa cha uwelewa kwa mwanafunzii
 
Jamani pia kusoma diploma sio kosa.watanzania wengi tunafikiria kupata mavyeti ya vyuo kuliko kujikita field.nlipokuwa diploma mwalimu mwenye asili ya urusi aliuliza darasa kuwa baada ya kuhitimu matarajio yenu ni nn? Asilimia 70 walikua wanataka waunge shahada si kufanya kazi.nlipokuwa advanced diploma tuliulizwa swali na vising prof toka ujeruman 60% tuliulizwa na wengi ilikua lengo kupata shahada ya uzamili kuunga moja kwa moja si kufanya kazi kwanza.hata nlipojiunga uzamili asilimia 80 ya darasa m
sababu ilikua sio kuongeza tija ila ilikua matumaini ya vitengo na maslahi kuzaraulika na vijana walotoka direct form six to chuo na ) na
si tija mahala pa kazi.kuna
 
Mkuu...
Lengo la kuweka masharti ni kubana matumiz kwa kupunguza namba ya wa nufaika wa bodi ya mikopo...hivi fikiria changamoto za shule za serikali hazina walim.vifaa na miundo mbinu..matokeo yake maskini watabaki nyuma kwa kuwa wao ndo wanaenda kusoma shule za gvt..
Hapana ndugu. This is too theoretical. Tupambane waboreshe elimu na si kupambana kupeleka mbele watu wasio na vigezo. Tujadili hata kwa kuanzisha asasi za kuwasaidia watoto wa masikini kupata elimu bora.
 
Acheni ushabiki usio na maana kwani inafahamika miaka yote kuwa chuo kikuu ni pass 2 kwa kiwango cha D sasa hii ya maneno yenu ya kuzusha inatoka wapi?

Tuwe tunaandika vitu vyenye maana sio mambo kama haya.
MIMI NIMEMALIZA UDSM MWAKA JUZI CIVIL ENGINEERING NIKIWA NA EED NA SIKUA PEKEYANGU VIP HAPO MKUU
NO RESEARCH NO SPEAKING
 
MZEE WAKAYA AMETOKEA DIPLOMA YA UALIMU VP KIWANGO CHAKE CHA UFAULU HADI KUDONDOKEA HUKU?
NA MWANAE JE-SC-A NADHAN MATOKEO YAKE MWAYAJUA DIPLOMA KASOMA MWAKA MMOJA LEO YUKO UDOM
ONGELA MZEE WAKAYA KWA KUSHIBA WEWE
 
Usitengeneze vigezo au sababu. Huyo mwenye A moja unataka akafanye nini chuo? Yaani asome nini. Bachelor in Mathematics??? Lets be serious.
WEWE KWEL UJITAMBUI
HIYO "A" YAKE YA PHYSICS INGEFAA KUTUMIKA KWA KUMWANDAA KUWA MWALIMU WA SOMO HILO
KWAN NI VIGUMU MWENYE WALAU DDD AENDE UWALIMU KWA RESEARCH YANYE SAMPLE TANO NILIYOFANYA KWAN HUFANYA UWALIMU KAMA ALTERNATIVE WAY MARANYING HUKIMBILIA ENGINEERING
 
WEWE KWEL UJITAMBUI
HIYO "A" YAKE YA PHYSICS INGEFAA KUTUMIKA KWA KUMWANDAA KUWA MWALIMU WA SOMO HILO
KWAN NI VIGUMU MWENYE WALAU DDD AENDE UWALIMU KWA RESEARCH YANYE SAMPLE TANO NILIYOFANYA KWAN HUFANYA UWALIMU KAMA ALTERNATIVE WAY MARANYING HUKIMBILIA ENGINEERING
Hatutaki bora liende. Tutengeneze heshima. Elimu yetu ni mbovu. Ingekuwa ruksa tungeweka script ya mwanachuo kisha tujiulize tunatengeneza nini. Kama suala ni A ya physics basi tuachane na combinations tufundishe somo moja A-level.
 
MIMI NIMEMALIZA UDSM MWAKA JUZI CIVIL ENGINEERING NIKIWA NA EED NA SIKUA PEKEYANGU VIP HAPO MKUU
NO RESEARCH NO SPEAKING
Kama nchi ilifikia hali hii, lazima turekebishe. Kama hilo ni jina lako ninakufaham na ninakushauri sifa za EED zifanye siri yako
 
Hapana ndugu. This is too theoretical. Tupambane waboreshe elimu na si kupambana kupeleka mbele watu wasio na vigezo. Tujadili hata kwa kuanzisha asasi za kuwasaidia watoto wa masikini kupata elimu bora.
Mkuu..
Unachosema ni kweli..lakini syo kwamba watu walikuwa wanaenda bila vigezo ..watu walikuwa wanaenda wakiwa na vigezo..kupandisha vigezo sasa hskumaniishi kuwa previous kulikuwa hakuna vigezo
 
Na wewe nae usitie kinyaa humu! Uandishi wa CV sio kipimo cha competency ya mtu wala intelligency ya mtu,elewa tu nacho kuzungumza hapa we ukoje? Uandishi wa CV nzuri ni ufundi tu na ndio maana hua zinatofautiana. Unaweza kwenda hata stationary na PhD yako ukamkuta form four failure akakuandalia CV nzuri kuliko unayoandaa wewe.
Hujitambui na uelewi unachoongea, endelea kufikiri EE ni qualifications za kuingia chuo, utasubiri sana
 
Kipindi CHA nyuma mpaka miaka ya 2000 mwanzoni tumeingia Chuo Kwa points Kama hizo cutoff points nakumbuka ilikuwa minimum D's Tena UD unapata nafasi Kwa mbinde
Hayo mambo yalikuja kubadilikA wakati wa JK na mambo yake ya VODAFASTA kilichofanyika ni kurudisha Ule utaratibu wa mwanzo uliokuwa umekiukwa

Vijana someni acheni kulalama.
 
Binafsi nililisema jambo hili mapema nikaonekana kama mnafki anayetetea ujinga, Nia ya serikali haikua kuboresha elimu kwa kupandisha madaraja ya ufaulu. Lengo lilikua kubana pesa na hiyo ndio sababu kuu ya kufanya hivyo,Wangekua na nia hiyo wangefanya maandalizi kwa angalau miaka 3 kuboresha miundombinu na kuwaanda vizuri wanafunzi.


Haiwezekani huyu mhitimu mwenye diploma ya Civil engineering mwenye GPA ya 3.0 amekaa barabarani miaka 7 na uzoefu wa kutosha, sasa anataka kusoma elimu ya juu wewe unamwambia hana vigezo! huo ni uonevu wa hali ya juu.
Kaka hapo umesema kweli, mimi nafundisha kwenye chuo cha habari, kuna wandishi wengi ambao wamefanya kazi za uandishi kwa miaka walibahatika kusoma short kozi ya miezi 3 wakaingia kazini, leo hii ndo wandishi mahili na maripota wa tv, kikwazo kinakuja pale wanapotaka kujiendeleza, tunaambiwa hatuwezi kuwafundisha hao kwa sababu hawana vigezo!

Najiuliza kusoma ni darasani tu? Na tena kigezo vha kuelimika ni masomo ua olevel tu? Mtu hawezi kujisomea kwa njia nyingine plus uzoegu akapata vigezo vya kujisongeza mbele? Huo ndo mfumo wa elimu yetu!
 
Kuna watu wajinga sana! Mnatetea ujinga? Naamini watu waende chuo kwa vigezo hafifu. Someni, acheni uzembe. Kwanza miaka niliyosoma mimi hatukutambua E kama kigezo cha kukupeleka chuo. Vilipoongezeka vyuo binafsi ndipo na hizi E zikawa ni qualification , lakini kwa udhamini binafsi. Kisha likaletwa pendekezo la kuundwa board ya mikopo. Sisi wanafunzi wa UDSM miaka hiyo tuliipinga kwa migomo na maandamano. Tulikuwa na sababu nyingi ikiwemo hii ya kuelekea kukumbatia ujinga. Enzi hizo ulikuwa ukishachaguliwa tu chuo kikuu taayari ushapata udhamini.Hivyo ushindani ulikuwa ni alama za ufaulu.

Wanafunzi tulisoma sana miaka ya nyuma. Leo wanafunzi wamekuwa wazembe wanataka kupunguziwa alama za ufaulu. Tupa kule vilaza. Tunataka msome
 
Hatutaki bora liende. Tutengeneze heshima. Elimu yetu ni mbovu. Ingekuwa ruksa tungeweka script ya mwanachuo kisha tujiulize tunatengeneza nini. Kama suala ni A ya physics basi tuachane na combinations tufundishe somo moja A-level.

Kama ni hivyo vyuo vikuu watasoma watoto waliosoma shule binafsi, kama FEZA, MARIAN, ST,ST kwani ndiyo hutoa wanafunzi kwa DIV 1-2 mara nyingi failure huwa ni div 3 tena wachache mmoja au wawili. kwa tuendelee kutengeneza matabaka, in ten years to come watoto wa maskini watakuwa hawana elimu, watoto wa wenye uwezo ndiyo watasoma university. tunajenga nchi ya namna gani? Shule Government za sasa siyo zile za miaka ile ya 90 kurudi nyuma.
 
Back
Top Bottom