Mikopo elimu ya juu: Serikali yaweka vikwazo kupunguza waombaji ili kukidhi ahadi ya 100%

Hatuna pesa za kusomesha,pesa ni kwa ajili ya Uwanja wa ndege Chato.
Mm nafikiri lengo kubwa la hili ni kupata walimu wengi wa sayansi, kubana matumizi sbb watakao enda chuo watakuwa wachache na mikopo itajitosheleza.
Waliosoma diploma na wana GPA ya chini ya 3.5 ni kuwabana wasije wakajiendeleza, waendelee kufanya kazi sbb kuna wengine hasa wale upande wa elimu wanaenda kusomea faculty nyingine.
 
Wakati mmeletewa Division 5 mlilalamika kila mtu akasema maneno mengi...

haya viwango vya ufaulu vimeongezwa tena ufaulu wenyewe Mdogo eti D 2 ila mijitu bado inalalamika..

hao wa diploma ndo kabisa huwa hadi wanafanyiana mitihani halafu leo hii muone G.P.A ya 3 .5 kubwa
 
Katika uchaguzi wa mwaka Rais aliahidi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote watakaofaulu kusoma vyuo vya Elimu ya juu. Baada ya Rais kuingia ikulu alijitahidi kutoa mikopo iliyokuwa imekwama kwa muda hivyo kuwapa wanafunzi matumaini.

Baada ya kukaa na kutengeneza budget ya mwaka wa fedha serikali imegundua kuwapa mikopo wanafunzi wote watakaofauru ni ngumu kwaani watakausha hazina yote hivyo serikali kushindwa kutekeleza ahadi nyingine hasa zile ambazo matokeo yake yanaonekana moja kwa moja kama ujenzi wa bara bara, huduma za maji na afya. Baada ya serikali kuliona hili imeamua kufanya yafuatayo:-

· Kuongeza madaraja kuingia vyuo vya elimu ya juu:- kwa sasa ili mwanafunzi aweze kwenda elimu ya juu lazima awe na alama D 2 katika mtihani wake wa kidato cha 6, ambayo ni sawa na daraja la pili. (Division two). Pia kwa wale waombaji wa Diploma lazima wawe na ufauru wa UPER SECOND 3.5 G.P.A

· Halafu ikaweka kipaumbele cha mwombaji kupata mkopo kwa wale waliosoma sayansi kidato cha 6.

Kwa vikwazo hivi serikali tayari itaweza kutoa mkopo kwa waombaji kwa asilimia 100 kwaani ni wachache sana wataoweza kupata mikopo. Nafikiri wengi waliosoma elimu ya juu wanatambua kuwa kupata alama A-D kwenye michepuo michepuo ya PCB, PCM, PGM, CBG siyo kazi nyepesi kwa shule zetu ambazo ambazo zina changamoto nyingi kama ukosefu wa maabala na upungufu wa walimu waliobobea katika masomo husika.

Pia ni ngumu kwa wanafunzi wa Diploma kufaulu kwa daraja la pili la juu yaani UPPER SECOND CLASS 3.5. mfano wanaosoma vyuo vya sayansi ya afya na sayansi nyingine km uhandisi na nk ni vigumu sana kupata alama tajwa.
Looks you are talking sense-sensible!
 
Wakati mmeletewa Division 5 mlilalamika kila mtu akasema maneno mengi...

haya viwango vya ufaulu vimeongezwa tena ufaulu wenyewe Mdogo eti D 2 ila mijitu bado inalalamika..

hao wa diploma ndo kabisa huwa hadi wanafanyiana mitihani halafu leo hii muone G.P.A ya 3 .5 kubwa
Kuna watu sio mijitu! Rekebisha lugha!
 
Wakati mmeletewa Division 5 mlilalamika kila mtu akasema maneno mengi...

haya viwango vya ufaulu vimeongezwa tena ufaulu wenyewe Mdogo eti D 2 ila mijitu bado inalalamika..

hao wa diploma ndo kabisa huwa hadi wanafanyiana mitihani halafu leo hii muone G.P.A ya 3 .5 kubwa
Bawacha hawana jema walimtukana sana JK na waziri wa Elimu lakini leo hii tena wamegeuka..
Wasubiri lowasa akiingia waende hata kwa division four...
 
Katika suala la mikopo kuna upotoshaji kidogo
Serikali kupitia Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu imeweka vigezo lakini ukiangalia kiundani wahitaji wote wa mikopo wana sifa na watapata bila kuangalia courses/programs(sciences or arts).
Hoja ya msingi hapa ni kuwa watanzania wengi ni masikini na hiki ni kigezo cha kupata mkopo, orphanage (yatima), disabled zote hizi ni sifa za kupata mkopo
Swali kuna Mtu hana kigezo mojawapo na hivyo?
Nafikili wahitaji ni kuwa watulivu time will tell.
Na hili la ufaulu nalo kuna siasa na utoto unaingia hapa kwa vile tu serikali inataka uwe DD unaweza ukawa na DDE=13,DDS=14 Bado una sifa ya kwenda chuo hapa ni accumulation of 4.0 from the two subjects and this is not the case.
Nafikili watu tutafute alternatives on how to copy with the system rather than condemning the system miaka 10 ni mingi sana so try to adjust.
 
Yaani wewe elimu yako unaona mwenye uwezo wa kuandika barua ya kizungu ndiyo kuelimika, mbona wale watoto waliosoma st. ukimchukua wa STD 7 AU FOMRM ONE ATAKUANDIKIA HIYO BARUA.

Nimekwambia application letter sijasema barua ya kizungu. Ndo matokeo ya division 4 hayo kwenda chuo kikuu. Jitahidi uwe unasoma na kuelewa kabla ya kukurupuka kuandika
 
Katika suala la mikopo kuna upotoshaji kidogo
Serikali kupitia Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu imeweka vigezo lakini ukiangalia kiundani wahitaji wote wa mikopo wana sifa na watapata bila kuangalia courses/programs(sciences or arts).
Hoja ya msingi hapa ni kuwa watanzania wengi ni masikini na hiki ni kigezo cha kupata mkopo, orphanage (yatima), disabled zote hizi ni sifa za kupata mkopo
Swali kuna Mtu hana kigezo mojawapo na hivyo?
Nafikili wahitaji ni kuwa watulivu time will tell.
Na hili la ufaulu nalo kuna siasa na utoto unaingia hapa kwa vile tu serikali inataka uwe DD unaweza ukawa na DDE=13,DDS=14 Bado una sifa ya kwenda chuo hapa ni accumulation of 4.0 from the two subjects and this is not the case.
Nafikili watu tutafute alternatives on how to copy with the system rather than condemning the system miaka 10 ni mingi sana so try to adjust.

Soma vigezo kutoka TCU CAS. angalia coz zenye vipaumbele ndiyo useme. Ukienda kwa ndani ya system ya TCU ukichagua course kuna sehemu unaonyeshwa kiwango kilichotengwa kwa ajili ya coz husika, coz zote zilizoandikwa not priority hazina mkopo. somo undergraduate admission guideline
 
Sidhani kama kuna wahitimu wanaonewa. Qualifications ya vyuoni haiwezi kuwa holela tu bila videzo.Kama ww hukupata D2 , basi una nafaai ya ku resit. Unaweza pia kwenda college na baadae university na siyo kupiga kelele unaonewa. Tena naombea vigezo vya ufaulu iongezwe uwe juu zaidi
 
Mimi ni mwanachama hai wa Chadema. Lakini napenda kuipongeza Serikali kwa kukaza uzi kwenye elimu na kurudisha kama zamani.

Ni sahihi kabisa kuwa aliepata Division 1 na 2 ndio wapate mkopo wa chuo kikuu, hii itarudisha heshima ya nchi katika elimu na uwezo wa wahitim.

Tukumbuke ilifika mahali ambapo kwenda chuo kikuu na kupata mkopo utadhani ni kujiunga na darasa la kwanza maana hapakuwa na vigezo. Hii ilisababisha ubora wa wahitimu kushuka kwa kiwango cha juu kwa sababu hawakuwa na haja ya kusoma kwa bidii, yaani mwenye Division 1 na 3 wana uhakika wa kukutana lecture room moja huko chuo kikuu.

Jambo lingine, wahitimu wa vyuo vikuu hawana tija sana katika nchi yoyote ile, wengi ni watu wa taaluma, managers, tunawahitaji lakini kwa kiasi cha kati. Nchi hii inahitaji watu wengi wenye technical skills, yaani wenye ujuzi wa kiufundi. Leo China inapaa kiuchumi kwa sababu wana vijana wengi wa technical. Sasa kama serikali imehamua kubana namna hiyo, wahakikishe tunawekeza kwenye vyuo vya ufundi, kuanzia kushona nguo, kutengeneza viatu, kutengeneza vinu vya aina mbalimbali ambavyo tunaagiza china kwa sasa, nk.

Mimi naunga mkono hoja, wacha enzi za msuli wa kuweka miguu kwenye beseni zirudi
 
Tunahitaji kuiridisha ile hadhi ya degree sio kama ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma...degree nilikuwa za bure MTU ana max za ajabu unashangaa kumkuta yupo chuo kikuu....tena anasomea ualimu ili aende kutufundishia watoto wetu UJINGA...

We kama umefail tafuta chuo cha hadhi yako.....nenda hata ukajifunze cherehani.
 
Ataingiliaje kati wakati yeye ndiye katoa maelekezo hayo? Natamani nifahamu Rais wetu ufaulu wake wa kidato cha 6 ulikuwaje. Pia me siamini GPA kubwa wana uwezo kichwani au uwezo wa kufanya kazi. unaweza kuwa na uwezo kichwani lkn ukasindwa kujiandaa vizuri au mtihani ukaji sehemu ambayo hukusoma. ndiyo maana nchi zilizoendelea course work ina marks nyingi zaidi ya 60% final exams ndiyo 20%-30%.
Hivi ni nani alianzisha utaratibu wa mtu asome miaka miwili darasani topic zaidi ya 200 alafu mwisho apewe masuali toka topic 18 tu ndizo ziamue uelewa wake,ifike wakati mtu asome topic 200 kwa miaka 2 na wakati wa kutahiniwa apewe wiki moja kujibu maswali 6 toka kila somo alilosoma kwenye combination yake toka topic zote zilizoko kwenye sylabus.mfano aliyesoma PCM na kama somo la Hesabu ametakiwa kusoma topic 48 kwa miaka 2 basi mtihani wa mwisho apewe maswali 48 toka kila topic na atakiwe kujibu masuali 6 kwa muda wa masaa 5,nadhani uwanja utakuwa level na ufaulu utakuwa wa haki.
 
Elewa vigezo alivyotumia yeye si lazima na wewe utumie hivyo. Policy na sera zina change. Lazima tuheshum vigezo vilivyotolewa. Muda wa short cuts ulisha isha. Hata kama GPA zao zilikuwa chini si kigezo cha wewe kwa sasa kuhalalisha failure wa sasa afike chuo kikuu wkt vigezo vimebalidilika. Waongoze watoto wako wasome vyema na na kupass na flying colors na siyo kulalamika hapa. Chuo gani duniani chenye heshima kichukue mtu hata D hana? Tena hata hizo D2 shukuru mungu... Inatakiwa angalau iwe juu zaidi
 
Inabidi wanafunzi waendane na kasi ya serikali, wakati wa Kikwete waliendana na kasi yake ya kupata Div 3 na 4, sasa waendane na kasi ya Div 1 na 2
 
Hii nchi inahitaji watu wengi wenye elimu ya kati na wachache wenye elimu za juu ambao watatumika kama wataalamu. Haiwezekani kila mtu akasome chuo kikuu bwana, kusoma ni kazi na si lelemama. Unapotaka kila mmoja afike chuo kikuu
1. Wafanyakazi utawatoa wapi
2. Hao wataalamu kutoka vyuo vikuu utawalipa nini, nyumba za kuwahifadhi za hadhi yao utazipata wapi
3. Hao watu ukiwapeleka kazini wakafanya chini ya kiwango kwasababu hujawalipa kwa malipo stahiki hiyo hasara utaifidiaje?
 
Elewa vigezo alivyotumia yeye si lazima na wewe utumie hivyo. Policy na sera zina change. Lazima tuheshum vigezo vilivyotolewa. Muda wa short cuts ulisha isha. Hata kama GPA zao zilikuwa chini si kigezo cha wewe kwa sasa kuhalalisha failure wa sasa afike chuo kikuu wkt vigezo vimebalidilika. Waongoze watoto wako wasome vyema na na kupass na flying colors na siyo kulalamika hapa. Chuo gani duniani chenye heshima kichukue mtu hata D hana? Tena hata hizo D2 shukuru mungu... Inatakiwa angalau iwe juu zaidi
Excellent brother, mbona hata JK aliweka masharti hayo hayo 2006 kwa div 1&2 ili upate mkopo na watu wakasoma? Tatizo hawa vijana wengi wa leo ni wavivu mno, walalamishi na wapenda starehe sana. Kama ningelikuwa waziri mie ningeweka C&D iqw sifa ya kukanyaga chuo. Chuo kikuu siyo mahala pa kila mtu kwenda, na hapawezi kufanywa ionekane ni sehemu ya watu kwenda kuuza sura
 
Back
Top Bottom