Mikopo Elimu ya Juu sasa kutolewa vyuoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikopo Elimu ya Juu sasa kutolewa vyuoni

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BabuK, Aug 21, 2011.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]SERIKALI imetangaza kwamba wanafunzi wa sayansi za tiba waliopata udahili kwa ufaulu wa daraja la kwanza na la pili watasomeshwa bure.Mbali ya wanafunzi wa madaraja hayo, hata wale wa wenye ufaulu wa daraja la tatu kutokana na kushindwa kwa somo la stadi za maendeleo, watasomeshwa bure kwa kupewa ruzuku badala ya mikopo.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema jana mjini hapan kuwa: “Ruzuku zitatolewa kwa wanafunzi wa sayansi za tiba waliopata udahili kwa ufaulu wa daraja la kwanza na la pili kulingana na ukomo wa bajeti,” alisema Dk Kawambwa huku akifafanua kuwa wanafunzi hao hawatawajibika kuzirejesha kwa kuwa siyo mkopo.

  Waziri Kawambwa alisema utaratibu huo wa utoaji ruzuku kwa wanafunzi wa sayansi za tiba utaanza katika mwaka wa masomo wa 2011/2012.

  Mbali na hatua hiyo, Waziri Kawambwa alisema: “Kuanzia mwaka wa masomo 2011/12, fedha zote za mikopo zitapelekwa vyuoni ili viwalipe wanafunzi baada ya kuwahakiki. Maelekezo na utaratibu utakaotumika utaandaliwa na Bodi ya Mikopo kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu na wadau wengine.”

  Ili kuboresha ufanisi wa utoaji wa mikopo hiyo alisema kila chuo kitatakiwa kuwa na dawati litakaloshughulikia masuala ya mikopo litakaloendeshwa na watumishi wenye sifa stahiki na kwamba litakuwa chini ya makamu mkuu wa chuo anayeshughulikia taaluma.
  Alisema chini ya utaratibu mpya, waombaji wa mikopo wanaosoma ualimu wa sayansi, hisabati na sayansi za tiba watapatiwa mikopo kwa asilimia 100 na kwamba wale ambao si wa taaluma hiyo watapewa asilimia 50 ya mkopo.

  Alisema mfumo wa utoaji mikopo utazingatia vigezo mbalimbali ambavyo ni pamoja na kuwapa kipaumbele wanafunzi wanaosoma ualimu, sayansi ya tiba, uhandisi pamoja na sayansi za kilimo na mifugo.

  Dk Kawambwa alisema mikopo itatolewa kwa wanafunzi waliodahiliwa katika vyuo vya elimu ya juu vyenye usajili kamili na kwamba utaratibu huo unaanza katika mwaka wa masomo kwa wanafunzi wapya 2011/12.

  Alisema wanafunzi waliopo vyuoni hawatahusika na utaratibu mpya.Dk Kawambwa alisema kuwa kwa upande wa vyuo binafsi, mkopo utatolewa kulingana na ada zinazotozwa na vyuo vya umma kwa fani husika na kwa fani ya udaktari ukomo wa mikopo utaendelea kupangwa na Bodi ya Mikopo.

  “Kiwango cha mkopo wa wale wanaostahili kukopeshwa kitategemea matokeo ya tathmini ya uwezo wa kiuchumi wa mwombaji na mzazi au mlezi kwenye vipengele vya ada na mahitaji maalumu ya vitivo,” alisema na kuongeza:

  “Aidha, mikopo itatolewa kwa asilimia 100 katika chakula na malazi, mafunzo kwa vitendo kwa fani ambazo zitabainishwa na tume ya vyuo vikuu pamoja na vitabu na utafiti.”

  Alisema uratibu wa kuwabaini wahitaji wa mikopo utazingatia vigezo vinavyopimika kwa urahisi kama vile shule aliyosoma, yatima, ulemavu na uwezo wa kiuchumi wa mzazi au mlezi.Alisema kwa upande wa ugharamiaji wa elimu ya juu, Serikali itaendelea kugharamia akiwataka wanafunzi wanaoomba mikopo wakatathmini uwezo wao wa kuirejesha ili wasielemewe na madeni wakati wa urejeshaji.

  Alisema katika kuhakikisha ufanisi wa urejeshaji wa mikopo, jitihada zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kurekebisha baadhi ya sheria za taasisi mbalimbali ili kuhakikisha wakopaji wanarudisha mikopo yao.“Kuanzia sasa kiwango cha chini cha marejesho ya mkopo kitakuwa asilimia nane ya mshahara halisi kwa mwezi wa mnufaika wa mkopo,” alisema.

  Tamko hilo la Serikali ni matokeo ya tume iliyoundwa kuchunguza na kutoa mapendekezo ya kuboresha utoaji wa mikopo ya elimu ya juu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, Februari 14, mwaka huu.“Kutokana na kazi ya Tume ya Rais, Serikali imefanya uamuzi mahsusi kuhusu utaratibu wa ugharamiaji, utoaji na urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kuanzia mwaka wa masomo 2011/12,” alisema

  Source: Mwananci


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...