Mikopo elimu ya juu haitoshi

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Ndungu zangu. Naileta hili swala mbele yenu ili angalau tujadiliane jinsi gani ya kuishauri serekali. Hili swala la mikopo linakera sana. Bodi ya mikopo haina vigezo maalumu vya kuzingatia kwaajili ya kutoa mikopo. Mwaka huu kwa anayeenda kusoma Science amepewa mko kwa 100% hata kama ana uwezo. Lakini wapo wengi sana ambao hawana uwezo hata wa kula milo miwili kwa siku lakini hajapata mkopo au amwpata 10%. Mimi inanisikitisha sana.

Ukija kwa waalimu wetu waliotufundisha, wanaofundisha watoto wetu, wajukuu na vitukuu, hawajapewa mkopo kwa 100%, wapo waliopata 0%, 10%, 30%, 40% n.k. Mwalimu huyu huyu akiajiriwa analipwa TShs 188,000. Huu ni mfano halisi natoa. Nina rafiki yangu mwalimu ameajiriwa Arusha Sec School analipwa TShs 188,000. Pale ni mjini sasa sijui ataishije ili alipe kodi ya nyumba, chakula, usafiri, nguo, matibabu, umeme, maji, pia akatwe mkopo n.k. Mwalimu huyu huyu, anapata mkopo 40% au asipate kabisa. Tena tunamtaka afundishe watu wapate division one. Mimi sijui kwa nini walimu wasisomeshwe bure? Au wapewe mkopo 100% kama madaktari?

Naomba tuchangie hoja kwa kuishauri serekali
 
Back
Top Bottom