Mikoa yote Tanzania yaagizwa kupima wananchi virusi vya UKIMWI (HIV)


LENGISHO

LENGISHO

Member
Joined
Sep 15, 2017
Messages
79
Likes
63
Points
25
LENGISHO

LENGISHO

Member
Joined Sep 15, 2017
79 63 25
MIKOA yote nchini imeagizwa kuwapima wananchi wake, virusi vya ukimwi (HIV) bure kwenye wiki ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi.

Wiki hiyo inaanza Novemba 24 na kuisha siku ya kilele cha Siku ya Ukimwi duniani Desemba Mosi. Kaulimbiu ni “Changia mfuko, okoa maisha, Tanzania bila Ukimwi inawezekana”. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema hayo jana.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa Dar es Salaam. Aliagiza kupatikana wataalamu wa kutosha kwa kila mkoa kwa upimaji huo na ushauri nasaha.

Alisema katika wiki hiyo, kutazinduliwa Ripoti ya utafiti wa kitaifa wa virusi vya Ukimwi, utafiti ambao hufanyika kila miaka minne. Alitaja shughuli nyingine ni uzinduzi wa mkakati wa kondom wa kitaifa, kongamano la kitaifa la wataalamu watakaojadiliana kukabili Ukimwi na huduma ya kupima kwa hiari.

Chanzo-Habarileo VIA Ukomboz blog
 

Attachments:

Jagarld

Jagarld

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2011
Messages
1,763
Likes
531
Points
280
Jagarld

Jagarld

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2011
1,763 531 280
Awaambie na wananchi nao wachukue majibu yao sio waendelee kuyakimbia.... !
 
mlogolaje

mlogolaje

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Messages
1,478
Likes
742
Points
280
Age
41
mlogolaje

mlogolaje

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2016
1,478 742 280
Awe wa kwanza
 
Moisemusajiografii

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2013
Messages
9,892
Likes
8,396
Points
280
Moisemusajiografii

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2013
9,892 8,396 280
Naamini wote tukipimwa itapunguza umasikini wa nchi. Tupige makofi kwa kujipongeza.
 
U

unruly gang

Member
Joined
Nov 17, 2017
Messages
46
Likes
32
Points
25
U

unruly gang

Member
Joined Nov 17, 2017
46 32 25
Kupima ukimwi ni bure watu wajitokeze kupima tu...
 
N

nzoka boy

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2017
Messages
586
Likes
447
Points
80
N

nzoka boy

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2017
586 447 80
hata nkiambiwa nkipima ntapata uwazir mkuu, sitaaaaakiii
 

Forum statistics

Threads 1,236,622
Members 475,218
Posts 29,264,575