Mikoa kumi kuwekewa mfumo mawasiliano ya inteneti

sayicom

Member
Jul 2, 2011
66
1
Umeisikia Hii Mikoa kumi kuwekewa mfumo mawasiliano ya inteneti pengine itakuwa mkombozi
KAMPUNI ya Six Telecoms Data, imezindua mpango wa kusambaza mfumo mpya wa mawasialino ya inteneti katika mikoa kumi nchini, ili kupunguza adha ya mawasiliano kwa wakazi wa maeneo ya vijijini.

Ofisa Mtendaji Mkuu, Nick Odero, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, mfumo huo wa mawasiliano unaolikana kama Metro Network, utasambazwa katika mikoa ya Tanzania bara ili kupunguza tatizo la mawasiliano.

"Mfumo huo ni wa kisasa na umekuwa ukitumika katika nchi za bara la Asia na Ulaya, utaunganishwa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya na Mtwara," alisema.

Aliongeza,"Metro Network itaondoa tatizo la kukosekana kwa huduma hiyo kwa watumiaji wa mtandao wa mawasiliano ya Inteneti kutokana na kutengenezwa kwa ubora wa hali ya juu."

Alisema kwa watumiaji wa kawaida, huduma hiyo imekuwa ikiwakwaza kutokana na kupata huduma isiyo bora huku wengine wakiingia gharama kubwa ya kuunganishiwa ili kuweza kutoa huduma bora kwa wateja wao.

"Wateja wamekuwa wakipata usumbufu wa hapa na pale na wengine wakishindwa kufanya mawasiliano ya kibiashara na washirika wao. Baada ya kuona usugu wa tatizo hilo, tukaamua kuanzisha huduma hii kwa lengo la kuondoa matatizo hayo,” alisema Odero,"alisema.

Alisema kwa kampuni zilizoko katika majengo marefu ya mikoa kwenye mikoa iliyoingizwa katika huduma hiyo, hawatakuwa na tatizo hilo tena.

Alifafamua kuwa huduma hiyo imetengenzwa kisasa zaidi kupitia utaalamu wa digitali wa ambao tayari kampuni mbalimbai zimeanza kupata huduma hiyo na kuondokana na usumbufu.
 
Nimefurahi kusikia hivyo.lakin kwa nilivyoelewa it means hii inalenga kuwanufaisha wafanyabiashara wanaotoa huduma ya intaneti,makampuni na maofisi.vipi kwa mtanzania wa hali ya chini hususan mteja,ambae hutumia huduma hii katika vituo vya intanet.je,hudama itarahisishwa kiasi cha kupunguza bei na kuongeza kasi ya mtandao?
 
wameniudhi sana yaani yule jmakamba ndio naibu waziri wa wizara science & ICT, mtu hana background yoyote ya technical issues unaenda kumpa wizara kama ile 2012
 
Back
Top Bottom