Mikoa 7 kufunga Kampeni za CCM Tanzania

Mikoa 7 kufunga Kampeni za CCM Tanzania

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Wakuu,

Leo saa Saba mchana, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.

Nitawaletea moja kwa moja kile watakachokuwa wanakizungumza wa ajili ya Watanzania.

================
Hadi sasa wazungumzaji wa Chama hawajafika ukumbini, waliofika hadi muda huu ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Nimepata taarifa kuwa mkutano huu utarushwa moja kwa moja (live) Azam Two.

attachment.php


Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbvali vya habari wakiwa ukumbuni kusubiri kuanza kwa mkutano huo.

Pindi wahusika watakapofika nitakaanza kuwapa kile walichotuitia.

January Makamba ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni, ameingia ukumbini na sasa anazungumza na waandishi wa habari anasema jambo kubwa ni kuzungumzia jinsi CCM watakavyofunga kampeni zao.

-Amesema watafunga mikutano hiyo katika mikoa 7 nchini. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM kitaifa waliopo madarakani na wastaafu.

Anasema mikoa hiyo na viongozi wakaoongoza mikutano ni pamoja na mkoa wa Mwanza - ambao atakuwepo, Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais

-Mkoa wa Tanga – atakuwepo Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Mkoa wa Mbeya – Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na -Mtwara – atakuwepo Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu,

-Mkoa wa Kigoma –Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM,Kilimanjaro – Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Mara – Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu.

Amesema Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka.

-Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituoa vya redio 67.

-Katika mikutano hii watakaohudhuria wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanjani vyote hivi saba.

-Ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.

-Pia tutafanya historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.

-Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015.

-Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa.

-Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku.

-Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.

-Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.

-Anazungumzia suala la amani kuwa CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu.

-Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu.

-Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
-Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu.


-Makamba anasema kauli za mashabiki baada ya kupiga kura wabaki vituoni kulinda kura ni kauli za watu wasiotaka uchaguzi wa amani, amesema utaratibu hapa nchini, namna pekee ya kulinda kura ni kupitia wakala wako, wao wana nguvu na mamlaka ya kushuhudia zoezi zima la uchaguzi, kuanzia maboksi yanapofunguliwa, kuanzia karatasi zinapofunguliwa, kuanzi kura zinapopigwa, zinapohesabiwa na hadi kutangazwa kwa matokeo.

Kura zinapigwa vituoni, kukiwa na mawakala na wasimamizi na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na wa nje. Mawakala wa vyama wanaweka sahihi katika fomu za matokeo yaliyohesabiwa palepale kituoni na matokeo hayo yanabandikwa nje ya kituo cha kura kwa watu wote kuona lakini vilevile kuna kituo kikubwa cha kujumlisha matokeo hapa Dar es Salaam ambapo vyama vinaruhusiwa kupeleka mawakala wake ili matokeo yanayotoka nchi nzima waweze kuthibitisha kama yanafanana na yale ya mawakala wao waliopo vituoni

-Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha vujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura.

-Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwasababu halina nia njema.

-Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa.

-Tunaviomba vyombo ya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

-CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.

Amesema siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani.

-Kuhusu matokeo, CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama.

Sisi tunategemea kuwa na matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi.

-Amezungumzia pia ajali ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, anaendelea vizuri na pia anaendelea kufanya kampeni zake kaam kawaida.

Amemaliza kuzungumza.
 

Attachments

  • Waandishi wa habari.jpg
    Waandishi wa habari.jpg
    28.7 KB · Views: 16,803
Wakuu,

Leo saa Saba mchana, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.

Nitawaletea moja kwa moja kile watakachokuwa wanakizungumza wa ajili ya Watanzania.

Umesikika hata hivyo inaonekana hata Inzi wa UKAWA yuko maeneneo ya Lumumba kupata habari ya hapa na pale siunajua imebaki siku Mbili tu kuelekea mechi.

Ila ni vizuri Mwenyekiti akavunja Baraza la Mawaziri iliatue mzingo wa Mamluki ndani ya Chama.
 
watasema kuwa utafiti mpya unaonesha magufuli atachaguliwa kwa asilimia 80%

Watasema Lowasa amekimbia mdhalo

Watasema lowasa amikanyaga kwenye interview na BBC

Watasema CDM wamewalipa vijana wamzomee magufuli

Kwenye mdahalo Mbona hata Magufuli sikumwona japo Yeye alikuwa anajitapa kila siku kuwa anataka mdahalo!
 
Wakuu,

Leo saa Saba mchana, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.

Nitawaletea moja kwa moja kile watakachokuwa wanakizungumza wa ajili ya Watanzania.


Waeleze hawa vijana wanafikiri hii nchi imeota kama uyoga. Wataanza kulia nyau sasa hivi.

AAfENUG.img


Hako Ka-Jambazi Sugu kameshakubali
kwenda kuchunga ng'ombe Monduli
 
ngoja tuone mambo,keshokutwa na JK naye ataongea ila hizi sinema zinakaribia kuisha
 
Wakuu,

Leo saa Saba mchana, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.

Nitawaletea moja kwa moja kile watakachokuwa wanakizungumza wa ajili ya Watanzania.

Sawa tunasubiri kwa hamu hiyo saa 7
 
Kwenye mdahalo Mbona hata Magufuli sikumwona japo Yeye alikuwa anajitapa kila siku kuwa anataka mdahalo!
Miccm ilivyo ya ajabu watamsema sana Lowassa kutohudhuria mdahalo ilhali wanajua mgombea wao pia hakuhudhuria!
 
Back
Top Bottom