Mike Tyson Ampasua Uso Mpiga Picha, Atiwa Mbaroni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mike Tyson Ampasua Uso Mpiga Picha, Atiwa Mbaroni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Mike Tyson Ampasua Uso Mpiga Picha, Atiwa Mbaroni
  [​IMG]
  Mike TysonFriday, November 13, 2009 7:52 AM
  Bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu duniani Mike Tyson ameingia matatani kwa mara nyingine tena baada ya kumtandika ngumi na kumpasua usoni mpiga picha aliyekuwa akimletea kero kwenye uwanja wa ndege.Polisi nchini Marekani wamesema kuwa bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu, Mike Tyson na mpiga picha mmoja wamefunguliana mashtaka kila mmoja baada ya ugomvi uliozuka kwenye uwanja wa ndege wa Los Angeles International Airport.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Mike Tyson alikuwa safarini kuelekea Las Vegas kwa kupitia uwanja wa ndege huo akiwa pamoja na binti yake mwenye umri wa miezi 10 na mkewe wakati tukio hilo lilipotokea.

  Taarifa zinasema kuwa Tyson na paparazzi huyo walirushiana ngumi lakini alikuwa ni Mike Tyson aliyempachika ngumi moja mpiga picha huyo iliyompeleka moja kwa moja chini na kumpasua sehemu ya juu ya uso wake.

  Mpiga picha huyo alipelekwa hospitali kupatiwa matibabu kwa majeraha aliyopata kufuatia kipigo alichokitafuta mwenyewe kwa kumghasi mbabe huyo wa zamani wa uzito wa juu.

  Alishonwa nyuzi tano katika sehemu yake ya juu ya uso wake iliyopasuliwa kwa ngumi nzito ya Tyson.

  Mike Tyson alikamatwa baada ya tukio hilo na kutupwa selo kwa muda kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000.

  Akiongea baada ya tukio hilo, mwanasheria wa Tyson, Richard Schonfeld, alisema kuwa Tyson hajafanya kosa lolote na alirusha ngumi katika harakati za kujilinda.

  Tyson katika utetezi wake alisema kuwa akiwa kama baba alikuwa na haki ya kumlinda mtoto wake mchanga baada ya kushambuliwa na paparazzi huyo.

  Mwanasheria huyo alisema kuwa watahakikisha Tyson anatendewa haki katika suala hilo.

  Ni kawaida kwa wapiga picha wa Marekani kuingia kwenye migogoro na mastaa kutokana na kero wanazowasababishia wanapotaka kuwapiga picha nzuri kwaajili ya magazeti na majarida yao.

  Huwafuatilia kila kona wanayoenda na wakati mwingine huwazuia hata kupita ili mradi wapate nafasi ya kupiga picha nzuri.

  Tyson sio staa wa kwanza wa Marekani kupigana na paparazzi wanaoranda randa wakati wote kwenye uwanja huo wa ndege lakini amekuwa bondia wa kwanza kumpeleka sakafuni kwa ngumi paparazzi.
   
Loading...