Mikataba yote ya madini ipitiwe upya tuache kukurupuka

Ray waniache

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
737
507
Ni mara ya kwanza kupost jukwaa hili. Mara nyingi nakua kwenye issue ambazo sio za kisiasa
USHAURI KWA SERIKALI YETU.

Mikataba yote ipitiwe upya ambayo haina faida kwa taifa tuachane nayo itatucost.Nchi hii kuna mikataba mibovu kupindukia hususan ya madini na gas ipo siku nchi itabaki mashimo na tutakua tumekumbuka shuka asubuhi

Kuna mikataba sijui niseme maagano tulosaini kule IMF na world Bank kuhusu wawekezaji sijui kuwalinda na kutoshika mali zao au kusitisha mikataba yao Tujitoe kwenye huu ujinga utatunyonga sisi wenyewe.

Lazima tuondoke kwenye mitego yote ambayo baadae inageuka kuwa mwiba mfano kukopa kwa ajili ya kutafiti ambayo sometimes wale watafiti au hayo makampuni yanayotafuta kuwalipa.mikopo inatubidi tuingie makubaliano ya wao kupewa tenda kwenye madini au gas ili wafidie mkopo wao.

Mikataba mingine yote ijyao tusikurupuke kusaini km tulivyokurupuka gas, tukae chini km taifa watafutwe wataalam waweke planning nzuri ili tukishatangaza kuhitaji wawekezaji tuwe tayar tumejipanga ili wakileta ujinga tuwabane vilivyo.

Lazima ifike mahali serikali iachane na huu ubepari wa kuwaachia wawekezaji tu wafaidi au kuwekeza kwenye rasilimali zetu badala yao na serikali nayo imiliki baadhi ya migodi ama vitalu vya gas iajiri watanzania wapate ajira, serikali ipate income,Kwasababu tunachokipata kwa wawekezaji ni kodi tu.

Tuingie ubia na wawekezaji kwamba mfumo utumike wa kugawana mapato kwamba serikali na mwekezaji wachimbe pamoja kama ni madini au gas faida ikija wagawane kwa namna walivyokubaliana.

[HASHTAG]#Tanzanianiyetusote[/HASHTAG]
 
Ikipitiwa upya watapigaje???Hawatakubali wataendelea kusaini mikataba vyumbani mwao ili waendelee kupiga
 
Sio ya madini tu, bali ya mambo yote yenye mchango mkubwa na maana pana kwa Taifa.
 
Sio ya madini tu, bali ya mambo yote yenye mchango mkubwa na maana pana kwa Taifa.
Ikibidi hata mkataba wa sisi kupewa madawa ya kupunguza makali ya ukimwi Arv's upitiwe upya maana unawafanya watu wabweteke na ngono zembe,watuuzie tununue ili hii bure bure iishe.
 
lazima watanzania tukubali kwamba ccm ndio iliyotufikisha hapa,ili nchi hii ifaidike na mali asili zake lazima tuitoe kwanza ccm madarakani, maana ukiwa kiongozi kupitia ccm inakubidi uwe mtu wa ndio kwa kila kinachosemwa na serikali au mkubwa vinginevyo unanyofolewa
 
Wewe pia ukipewa fursa utakula ndio hulka ya mwanadamu chadema wakipewa watakula,cuf wakipewa watakula,hashim rungwe na saccos yake pia watakula hata bakwata na baraza la maaskofu wakipewa watakula tu.
 
Ikibidi hata mkataba wa sisi kupewa madawa ya kupunguza makali ya ukimwi Arv's upitiwe upya maana unawafanya watu wabweteke na ngono zembe,watuuzie tununue ili hii bure bure iishe.
haki vile hii ndo inatucost
 
hilo ni wazo zuri sana. lakini vijana wa lumumba wamekazana kusema mkuu ni mzalendo na anuchungu na mali asili zetu lakini hawataki kuongelea kabisa suala la mikataba iliyosainiwa na wenyeviti wa ccm waliomaliza muda wao. huu ni unafiki mkubwa sana kwa taifa letu na utazidi kutuumiza. analolifafanya mkuu wa nchi ni zuri sana na muunga mkono lkin kama hataweka mikata iwe ya uwazi na ipitiwe upya basi huu ni usanii tupu
 
well said
 
Back
Top Bottom