Simba mnyama
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 348
- 129
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikijiuliza mikataba mingi ambayo Serikali hii ya Awamu ya Nne kupitia chama cha mapinduzi na Rais Kikwete imeingia na inaendelea kuingia na mataifa mbalimbali ya nje inavyomnufaisha mtanzania wa kawaida lakini sipati jibu. Naweza kusema Serikali hii imevunja rekodi ya kuingia mikataba mingi sana kuliko awamu nyingine yoyote tangu taifa hili lijipatie uhuru wake. Kila kiongozi mkubwa kutoka nje anapozuru hapa tumekuwa tukipewa taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa mojawapo ya shughuli kubwa itakayofanyika wakati wa ziara hiyo ni kusaini mikataba mbalimbali, lakini aina ya mikataba na kilichomo katika mikataba hiyo imekuwa ni SIRI kubwa. Sehemu mojawapo ya taarifa iliyotolewa majuzi na mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhusiana na shughuli itakayofanywa na Waziri Mkuu wa Thailand aliyopo hivi sasa hapa nchini ilisema,
"Akiwa Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand."
Ndani ya kipindi cha miezi minne tu tumeshuhudia viongozi wakubwa kutoka mataifa mbalimbali ya nje wakipishana hapa nchini. Viongozi hao ni kama vile:
1. Bi. Helle Thorning-Schmidt, Waziri Mkuu wa Denmark aliyekuja Tanzania Mwezi Machi, mwaka huu
2. Xi Jinping, Rais wa China aliyekuja Tanzania pia mwezi Machi mwaka huu.
3. Barack Obama, Rais wa Marekani aliyekuja mwanzoni mwa mwezi huu wa Julai
4. Bi. Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa Thailand aliyopo nchini hadi muda huu.
Na wengine kibao bado watakuja muda si mrefu.
Siamini kabisa kuwa viongozi hawa wanakuja tu nchini kuuza sura, makumbusho ya taifa na mbuga ya Serengeti, ninachoamini ni kwamba kuna kitu wanachokitafuta. Tusipokuwa makini katika mikataba mingiii tunayoingia, tutakuja kulia siku moja, na watakaolia zaidi ni wananchi wa kawaida.