KERO Kilio cha watumishi wa mikataba (Project staffs) - NIMR

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ni miongoni mwa taasisi muhimu za utafiti nchini, ikiwa na vituo kadhaa vilivyoanzishwa kwa nyakati tofauti.

Baadhi ya vituo hivi, kama kile cha Mbeya, awali vilikuwa vituo binafsi kabla ya Serikali kuvichukua rasmi mwaka 2013, wakati wa Uongozi wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

Kutokana na historia hiyo, sio watumishi wote walioweza kuingizwa serikalini mara moja, wengine waliendelea kuwa watumishi wa mikataba kupitia miradi ya utafiti inayofadhiliwa na wadau wa kimataifa.

Katika Awamu ya Tano, wakati wa ziara ya aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, watumishi hawa wa mikataba waliwasilisha ombi la kuingizwa rasmi serikalini. Waliahidiwa kwamba jambo hilo lingefanyika taratibu kulingana na IKAMA.

Hata hivyo, uongozi wa sasa umeonekana kutokuwa na kipaumbele hicho tena, badala yake, waajiriwa wapya wanaendelea kuchukuliwa huku watumishi wa muda mrefu wa mikataba wakiendelea kutreatiwa kama “vibarua.”
Tofauti ya kimatendo inayoonekana:

• Watumishi walioingizwa serikalini wanapata stahiki kamili — house allowance, transport allowance, na communication allowance.

• Watumishi wa mikataba (Project Staffs), ambao ni Watanzania halisi wanaofanya kazi katika nchi yao, wananyimwa stahiki hizo — hali inayowafanya wajihisi kama wageni kwenye nchi yao wenyewe.

Hadi kufikia tarehe 11/08/2026, ni siku 48 tangu malipo ya mwisho, watumishi wa mikataba hawajalipwa mishahara yao.

Hali hii inaathiri kwa kiasi kikubwa maisha yao na familia zao, wakati wenzao waliopo serikalini wanaendelea kupokea stahiki zao kama kawaida.

Tunaomba mamlaka husika (uongozi wa NIMR, Wizara ya Afya, na wadau wengine wenye dhamana) kuliangalia suala hili kwa jicho la haraka na la kibinadamu.

Watumishi hawa wamekuwa uti wa mgongo wa tafiti muhimu za kitaifa kwa miaka mingi; wanastahili kutendewa haki, heshima, na malipo ya wakati kama Watanzania wenzao waliopo katika mfumo rasmi.
 
Pole sana mdau, hivi hizi hoja huwa zinazingatiwa? kuna namna hapa wahusika wanaweza kuwa tagged?

Lakini kulingana na autafiti wangu, ni ngumu sana serikali kuajiri watumishi wa mkataba moja kwa moja.
Sasa na nyie mnapaswa kuchangamka, wakitoa hizo kazi ombeni, msibweteke tu na huku mnazitakana.

Hili lakuajiri moja kwa moja wameliweza Tanesco na TANROADS tena kwa maeneo machache na huwa inategemea sana nguvu ya Mkurugenzi aliyeko.

Kuna wajamaa wa TBA walikuwa mkataba na wameomba kazi kupita utumishi lakini ajabu wamepangiwa sehemu nyingine. so na nyie kwasababu ,kuna ugumu sana msibakie hapo kusubiria huruma za serikali.

ombeni Kazi kwa mfumo rasmi uliopo.
 
Back
Top Bottom