Mikasa ya kweli (kufurahisha na kukera)

Gily Gru

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
7,802
20,762
Niaje Wadau wa JamiiForums

1. Jamaa akiwa na demu wake wakiwa wameshikana mikono, mara ikapita njemba nyingine paap kuangalia demu ya jamaa imeshona tako balaaa, si jamaa kaona mwenzake anafaidi, basi akajongea akamminya yule demu wa jamaa tako.

Jamaa akakubaliana na matokeo mana njemba ilikuwa imevimba miraba minne, demu akasuburi jamaa amtemee njema hata mate ila jamaa akauchuna kama hajaona.

Aisee demu eti kwa hasira akamuita njemba amsubirie akamminye vizuri tako. Jamaa kabaki analia tu, anamwambia demu wake si vizuri kugombana na machizi barabarani.

Swali la kizushi:
Wanaume:
Ukiwa uko na demu wako au mke wako, au dada yako afu njemba imepita paap imemminya tako mbele yako, Utafanya nini? Ukiwa mwananume akapita njema badala ya kushika demu akushike tako, utamfanyaje?

Wanawake: Kama wewe mwanamke uko na bwana wako, au kaka yako au mumeo afu ikatokea mwanamke akamshika tako mbele yako. Utafanya nini?

Binafsi: Nikiwa na demu njemba ikapita ikamshika tako mbele yangu, aisee mie sirushi ngumi, niitamfata njema na kumshika tako na yeye.

2. Jamaa yuko na demu wake coco beach, wakiwa wanazura zurura pande za ufukweni, mara wakakutana na beach boys. Basi wakati demu anapita zile njemba zikaanza kuzungumza mara huyu demu hana maajabu, mara demu mweusi kama giza; mara demu si kahamaki na kuanza kurushiana maneno na zile beach boys.

Akaanza kupayuka, "oh mkiendelea kuzungumza bwana angu atawadunda".

Beach boys wakamka, jamaa kuona mabaharia wengi akamkana yule demu akawaambia mabaharia beach boys "mie nimekutana nae beach simjui huyu demu kama anazingua mzingueni tu.

Jamaa akaamsha na demu kwa hasira akaamsha, baadae anamuomba demu msamaha eti kosa la demu ni kugombana na wahuni afu amsakazie kesi yeye.

Swali la kizushi: Ikiwa wewe uko na mwenza afu achokozane na watu kisa upo nae, ungefanyaje?

3: Kuna jamaa kila siku anatoka na mademu waliokuwa na umri mkubwa, sasa watu kitaa wakawa hawamuelewi mana nyendo zake angewafukuzia hata mama zao; baadae machizi wakamuuliza vipiiii mbona unafukuzia mademu vikongwe wakati wadogo chuchu saa sita wengi wa kutosha tu kitaa.

Jamaa akajibu "mimi sina nguvu za kukaza mademu wadogo zimekwisha nina nguvu za kusukuma mavi tu, ndo mana natoka na vikongwe". Ingekuwa wewe jamaa ungemjibu nini?

4. Kuna kapicha hapo chini kinauliza: Mke wako au demu wako na hicho kindama, nani mzuri zaidi?

5. Dogo akiwa amevua shati anataka kwenda kuoga, mara paap anakutana na dingi yake mlangoni; dingi akamwangalia kifuani huku anacheka akamwambia "kwa hivi vichuchu kifuani mwako, akijisahau akilala kwenye banda la nguruwe, vitoto vya nguruwe vitagombea kumnyonya vichuchu wakizani ni mama yao". Ikiwa ni wewe dingi utamfanyaje?

Tupenane visa na mikasa ya kweli (kufurahisha na kukera) ambayo ilishawahi kutokea au inaweza kukumta mtu na kumtia mtu hasira za kumshawishi kutoa uhai kabisa.

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.png
 
Sitaki kabisa watu wakae seat za mbele kwenye nyuzi zangu, nakaa mwenyewe siti ya mbele wakitaka kuwa mbele wakakae kwenye seat zao, wenye mikasa waje. .


Kuna kitabu nimesoma hapa kichwa cha habari Desturi Za Wasuaheli By Dr C Velten


Hiki kitabu kinaelezea kuwa kuna jamii za Tanzania kipindi hicho walikuwa walaji wazuri wa nzige wakiwemo WANYAMWENI na WASUKUMA. Nawaza tu hivi hawa nzige wakija bongo kwenye mighahawa MENU zitasomaje:

Ugali Nzige Roast..............TZS 2500/-
Wali Nzige Roast................TZS 3000/-
Ndizi Nzige Choma............TZS 3000/-
Ugali Nzige Choma.............TZS 3000/-
Wali Nzige Choma................TZS 3000/-

Wauza Supu:
Supu ya Vichwa Nzige...................TZS 1000/-
Supu ya Miguu Nzige....................TZS 2500/-
Supu ya Utumbo Nzige..................TZS 4000/-
Supu ya Kiwiliwili Nzige.................TZS 500?-


wakaangaji samaki:
Fungu moja la NZIGE...................TZS 1000/-
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    167.1 KB · Views: 20
Aisee mi sina kisa mkuu

yess BiShoo haswaaAaa
Nakupa kisa Fundi Bishoo...


Katika pita pita zangu pande fulani za uswahilini nimekutana na masela wawili wanabishana leo. Mahojiano yao yalikuwa kama hivi:

Jamaa mrefu: Huyu jamaa ni mrefu kidogo alimuliza mwenziwe swali la kizushi "Hivi ukipewa AKILI na TZS 100 MILLION, utachagua kipi?"

Jamaa Kibonge: Jamaa ambaye alikuwa kibonge wa miraba minne alionekana akifikiri kidogo kisha akajibu "Mie nachagua AKILI". Akamuliza jamaa mrefu, je wewe ukipewa AKILI na TZS 100 MILLION utachagua kipi?

Jamaa mrefu: Huku akiwa ametabasamu akajibu "mie nitachagua TZS 100 MILLION"
Jamaa Kibonge: Yani wewe hujielewi hata kidogo utachaguaje TZS 100 MILLION, unahitaji uwe na AKILI ili uweze kuziendeleza hizo TZS 100 MILLION, utashindwa kuziendeleza.

Jamaa mrefu: Akiwa ametabasamu "Mie nimechagua kitu ambacho sina na nimechagua TZS 100 MILLION, wewe umechagua AKILI kwa kwa sababu unahitaji kuwa na AKILI. .

Jamaa kibonge akaamka akaanza kurusha ngumi, ugomvi ulikuwa mkubwa sana, mie nimekimbia nimekuja huku kukuliza wewe Fundi Bishoo, "Hivi ukipewa AKILI na TZS 100 MILLION, utachagua kipi?". .
 
Kuna watu walikuwa wanabishana juu ya neno KADAMNASI katika sentensi, basi wakajikuta wanaleta kamusi ya Kiswahili kuangalia maana halisi ya neno KADAMNASI, wakakuta maana yake ni "MBELE YA WATU"

Msela: Sentensi yake inatakiwa iwe hivi "Raisi wa Tanzania anahutubia MBELE YA KADAMNASI"
Demu: Hapana hauko sahihi, neno KADAMNASI maana yake ni "MBELE YA", huwezi kutunga sentensi ukasema "MBELE YA KADAMNASI", tayari neno KADAMNASI maana yake ni MBELE YA"

Msela: Wewe ndio utakuwa hujui Kiswahili, Basi nitungie sentensi kutumia neno KADAMNASI
Demu: akafikiri nae akatoa sentense yake "Mbunge wa viti maalumu alipigwa risasi katika KADAMNASI"
Msela: Ina maana Mbunge alipigwa risasi katika mbele ya ? Hapo wewe itakuwa ni kiswahili cha mtwara vijijini, si sawa

Mie niliwaacha wakiwa wanabishana na kutunga sentense zenye neno KADAMNASI, weka sentensi moja yenye neno KADAMNASI, tuwasaidie Msela na Demu. .
 
Gily, naungana na uyo mwamba nipewe hyo milioni mia tu mambo yasiwe mengi aisee.....

yess BiShoo haswaaAaa
 
naungana na uyo mwamba nipewe hyo milioni mia tu mambo yasiwe mengi aisee.....

yess BiShoo haswaaAaa

Alaaa kila mtu anachukua asichokuwa nacho, akili unazo, ndio maana unachukua million 100. .
 
Mkasa mwingine leo 09/02/2020

Kuna mzee mmoja anajikuta ana akili sana, leo kapigwa swali la kizushi: Je, kati ya gunia la pumba kilo mia moja na gunia la machanga kilo mia moja lipi ni zito zaidi?

Mzee si akajibu bhana, "we unajua mchanga wewe ni mzito kweli kweli, tena ukiwa umelowa na maji ni nzito sana, hazibebeki"

Aliyemuliza akamjibu "mie sikuzungumzia mchanga kulowa na maji, Je pumba kilo mia moja zikilowa na maji zinakuwaje???"

Mzee akajibu "sipendi kuulizwa maswali ya kipumbavu, wewe unauliza makofi polisi"



Swali la kizushi : Pumba kilo mia na Mawe kilo mia, ipi nzito zaidi???????????????????????????
 
Mkasa mwingine vijana wanabishana wakiwa wameshiba chakula cha usiku:


Kuna madogo hapa wanaonekana wameshiba sana wanabishana kuhusu CCM na CHADEMA:
Dogo wa CCM: Serikali ya awamu ya tano ni moto, yani wamekuja na kasi ya umeme, maendeleo kila kona, lazima tumpitishe Raisi Magufuli uchaguzi 2020
Dogo wa CHADEMA: Safari hii nakwambia Raisi atatokea upinzani, lazima upinzani ulete mabadiliko, mie naandaa kitambulisho cha kura, kama ni kuku, lazima achinje kuanzia nyumba ya shingo
Dogo wa CCM: Acha ujinga wewe sie lazima kwa maendeleo yaliyopo lazima tuchukue ushindi kwa nguvu
Dogo wa CHADEMA: Afu we dogo waCCM Mpumbavu sana, yani kuliko kuishi na watu kama nyie TANZANIA, bora ningezaliwa MSTIMU marekani. Watu kama nyie mngekuwa China mngechomwa sindano ya sumu mfe tu
Dogo wa CCM: Kwani we nani, ukazaliwe tu mtupunguzie msongamano Bongo, kwanza iuniue unanijua, auliwe nani kwa kuchomwa sindano ya sumu?
Dogo wa CHADEMA: Unauliwa tu kwani we nani? Nani anakujua?Una faida zipi?
Dogo wa CCM: SIO KWA SERIKALI YA MAGU. HEBU NIUE UJUE KAMA SERIKALI INANIJUA AU HAINIJUI? JARIBU UNIUE UONE SERIKALI YA MAFU INANIFAHAMU AU LA. .


Mie nikaona hawa madogo wameshiba na wana masikhara kweli kweli, nikachukua hamsini zangu, ila dogo wa CHADEMA sijui aliua ahakikishe serikali inamjua dogo wa CCM au la teh teh teh. .
 
Leo mkasa unakuja kutokea ndani ya JamiiForums:

Katka nyuzi nyingi unaona kuna baadhi ya watu wana comment hii CHAI, huku wakisubiri wapatiwe maandazi na chapati.
Chai ikiwa ya moto sana watashindwa kunywa na hayo maadazi au chapati wanazozisubiri ziletwe, Waje kwenye huu uzi kuna visosi vya kupoozea hiyo chai ya moto wasije ungua midomo..

Kama wanataka chai na viporo, sambusa, au mayai wasubiri huko huko. . .
indeax.jpg
index.jpg
800px_COLOURBOX1445208.jpg
 
Niko na baba yangu mdogo hapa, ananiambia kuhusu dawa za mbu za coil ambazo zilikuwa zinatumika zamani. Anadai hii haikuwa dawa ya mbu kipindi wakiwa wadogo walikuwa wanazichoma, moshi ukitoka ukiingia puani basi usingizi unakupitia vizuri ili mbu wakiwa wanakung'ate vizuri usisikie maumivu. Mh kuna ukweli??
 

Attachments

  • coil.jpg
    coil.jpg
    21 KB · Views: 10
Njemba lolote kumminya mke wangu tako hapo lazima kinuke, hata kama lina miraba mia, vigae vya chupa, mawe, viti yaani chochote kitamhusu, kichwa chake halali yangu.
 
Pande za kiswazi hivi, Mpemba kaenda nyumbani kwa mgosi, kama kawaida yake kutembea na mke wa mgosi. Akiwa dirishani akaanza kuita na kumshinikiza afungue mlango aje apumzike
Mpemba: Fungua lango nije ndani pumzika
Mke wa mgosi: (Akiwa anazungumza kwa sauti ya kuning'oneza) usije mwenye mali leo yupo njoo kesho. (Akimaanisha mumewe yupo.
Mpemba: Acha masikhara jana ulinambia vinyo na nikakudedeua.

Mgosi si akatokea bhana, ugomvi ulikuwa mzito sana maana mgosi alisikia kila kitu na akiwa kajifunga kanga ya mkewe, nimewaacha amemshikilia mpemba anataka nae KUMDEDEUA. .
 
Njemba lolote kumminya mke wangu tako hapo lazima kinuke, hata kama lina miraba mia, vigae vya chupa, mawe, viti yaani chochote kitamhusu, kichwa chake halali yangu.


Mie lazima nimminye na yeye tako lazima nimrudishie, yeye kaminya na yeye aminywe. Hapo nitaridhika sina haja ya kurusha ngumi wala mawe..

Nimekubali sana mbinu zako ila hujasema utamuuma sikio kama Tyson alivyomuma Evander teh..
 
Kuna wana walikuwa wanabishana kuhusu nyama ya ng'ombe na mbuzi?

Mgogo: Mbuzi wa Dodoma bei chee sana elfu thelathini unapata
Mchaga: Mbuzi wa Kilimanjaro bei sana afu mbuzi na ng'ombe kutoka Kilimanjaro watamu sana aisee nyama choma unaweza kula kilo tatu.
Mgogo: We Dar nzima wananunua mbuzi na ng'ombe wa Dodoma wale wana soko sana
Mchaga: Mbuzi na ng'ombe wsa Kilimanjaro wanakula majani yenye sukari wenu wanakula vumbi na udongo nyama chungu

Nimeshangazwa sana, sikujua kumbe mbuzi nao wana UKABILA. .
 
Back
Top Bottom