Mikasa Duniani

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Tangazo la kazi
Kama uko tayari kufanya kazi yoyote
mahala popote -- kuna kazi
imetangazwa -- huko India vijijini --
kazi ya kunyonga watu.
Maafisa wa gereza la Jorhat, karibu
maili mia mbili mashariki mwa Gauhati,
wanatafuta mtu atakayekuwa tayari
kupeleka watu kwenye kinyongeo.
Majaji nchini India aghalabu hutoa
hukumu za kifo. Gazeti la Metro
limesema watu wawili tu
wamenyongwa nchini humo katika kipindi
cha miaka 15 iliyopita.
Myongaji mwenye uzoefu nchini humo Nata
Mullick alikufa mwaka 2009.
Bwana Mullick ambaye mwaka 2004 akiwa
na umri wa miaka themanini na nne, na
akiwa tayari amestaafu, alilazimika kuitwa
kwa dharura ili kumnyonga mtu aliyekuwa
amehukumiwa kifo wakati huo.
Wafanyakazi katika magereza ya karibu na
Jorhat, katika majimbo ya Uttar Pradesh na
West Bengal wameulizwa iwapo wanaitaka
kazi hiyo, lakini hakuna mtu aliyejitokeza
mpaka sasa.
Iwapo hakuna mtu atapatikana kufanya kazi
hiyo, huenda hukumu za kifo zilizotolewa
zikawa mashakani. Kuna watu watau kwa
sasa ambao wamehukumiwa kunyongwa
nchini India.
Panya mla nguruwe
Mfugaji mmoja nchini Australia hakuamini
macho yake alipokuta mifugo yake
ikishambuliwa na panya.
Mfugaji huyo wa kusini mwa Australia John
Gregory aliingia katika banda lake la kufugia
nguruwe na kukuta nguruwe wake mmoja
akiliwa na mamia ya panya waliomvamia,
umeripoti mtandao wa news.com.
"Tatizo la panya limekuwa kubwa mno"
amesema bwana Gregory. Katika kukabiliana
na nguruwe wake kutafunwa na panya,
mfugaji huyo ameamua kuwapaka nguruwe
wake mafuta machafu ya engine-- maarufu
kama oili chafu.
"Hawa panya wameishiwa chakula,
wanawaparamia nguruwe na kuwatafuna"
amesema Gregory na kuongeza "Lakini
hawapendi ladha ya mafuta machafu na
ndio salama yangu" amesema mfugaji huyo.
Amesema sumu ya panya inauzwa bei ghali
na hivyo analazimika kutumia njia kama hizo
za ujanja. "Sisi wakulima tunapenda vitu vya
bei nafuu" amesema Gregory "Wakati
mwingine huwa nachanganya sukari na
simenti, panya wanapenda sukari, wakiila,
ile simenti inaganda tumboni mwao"
amesema Gregory.
Panya ndani ya ndege
Shirika la ndege za Australia lililazimika
kufuta safari yake moja, baada ya
wafanyakazi wa ndege kukuta vitoto vitano
vya panya ndani ya ndege.
Panya hao waligundiliwa muda mfupi tu
kabla ya abiria kuanza kuingia ndani ya
ndege kuanza safari mjini Sydney. Panya hao
walikutwa katika moja ya kabati ndogo
ndani ya ndege hiyo aina ya Boeng 767.
Msemaji wa shirika hilo amesema panya hao
walikamatwa na kuuawa, na ndege hiyo
kusimamisha safari zake kwa muda wa saa
thelathini na sita. Shirika hilo limesema hili ni
jambo lisilo la kawaida, na kuwa hakuna
dalili yoyote ya uharibifu ambayo
umefanywa.
Figo kwa iPad
Kijana mmoja nchini Uchina alikuwa
akitamani sana kupata kifaa kipya cha
mawasiliano aina ya iPad 2 kiasi kwamba
aliamua kuuza figo yake ili anunue kifaa
hicho.
iPad ni kifaa cha kisasa ambacho kinaweza
kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na
kuhifadhi muziki na pia kurambaza kwenye
mtandao.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17
aliyejulikana kwa jina moja tu la Zheng alikiri
kwa mama yake kuwa aliamua kuuza figo
yake baada ya kuona tangazo la mtu
anayetaka kununua figo kwa dola elfu mbli
za kimarekani.
"Nilitamani sana kuwa na iPad 2 lakini
sikuwa na pesa" amesema kijana Zhang
akizungumza na kituo cha televisheni cha
Shenzen, katika jimbo la Guangdong. Kijana
Zheng aliporudi nyumbani mama yake
aligundua mara moja.
"Aliporudi, alikuwa na laptop mpya na iPad
mpya" amesema mama yake, huku
akionesha kidonda ambapo mwanae
alifanyiwa upasuaji kutoa figo. "Nilitaka
kujua alipata wapi pesa za kununua vitu
hivyo vya gharama kubwa, na ndipo akakiri
kuwa ameuza figo yake moja" amesema
mama huyo.
Simu za iPhone na kifaa cha iPad ambazo
hutengenezwa na kampuni ya Apple ni
maarufu sana hasa kwa vijana kuonesha
ufahari wao nchini Uchina.
Jamaa kakatwa nanihii
Mwanamama mmoja nchini Bangladeshi
ameukata--- CUT--- uume wa mwanaume
mmoja-- SHOUT-- na kuupeleka polisi kama
ushahidi kuwa alikuwa akitaka kubakwa.
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC
mwanamama huyo mwenye umri wa miaka
arobaini alifanya hivyo siku ya Jumatatu.
Mwanamama huyo ambaye ameolewa na
ana watoto watatu, amedai kuwa
alishambuliwa wakati akiwa amelala katika
wilaya ya Jhalakathi, karibu kilomita mia
mbili kusini mwa mji mkuu Dhaka.
Maafisa wa polisi wanasema mwanaume
anayetuhumiwa kutaka kumbaka pia ana
miaka arobaini na ana watoto watano.
"Wakati akijaribu kumbaka, mwanamke
huyo alimkata kwa kutumia kisu, halafu
akaifunga kwenye mfuko wa karatasi na
kuileta polisi kama ushahidi" amesema
Abdul Khaer, mkuu wa polisi wa huko.
Kipande hicho kilichokatwa kiliachwa polisi
wakati mshukiwa huyo akitibiwa hospitali.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo anasema
mwanamama huyo alikuwa mpenzi wake,
na alimtaka watoroke wakaishi pamoja.
Bwana huyo amesema alipokataa ombi la
mwanamke huyo, ndipo alishambuliwa.
Mkuu wa polisi Khaer amesema
watamkamata, mara tu atakapopata nafuu.
Daktari wa hospitali anapotibiwa
mtuhumiwa huyo amesema imeshindikana
kuunganisha kipande kilichokatwa.
Na kwa taarifa yako
... Ukifika umri wa miaka 75, utakuwa
umelala kwa takriban miaka 23 kwa jumla...
 
Back
Top Bottom