Mikakati gani itumike kuongeza matumizi ya gesi na kupunguza matumizi ya mkaa

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
DeoLex6X0AElVF-.jpg

A sack of charcoal in Dar es Salaam cost Tzs 70,000, while a bottle of cooking Gas weighing 15 kg is about 45,000 to 50,000 shillings. Tatizo ni nini hasa? Elimu au

Gunia la mkaa linauzwa shillingi 70,000/= za kitanzania katika Jiji la Dar es salaam na mtungi mmoja wa Gas wa 15kg unauzwa shillingi 45,000/= mpaka 50,000/=

Tupange mikakati gani ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuongeza matumizi ya Gas ambayo tunayo ya kutosha ili kupunguza uharibifu wa mazingira kwa vizazi vyetu na vijavyo?

DeoLex3WkAENulf.jpg
 
Bei ya gesi ishuke na mkaa upandishwe bei kimakusudi ili watu wajikite kwenye matumizi ya gesi.
 
Haya maoni yanapelekwa kunakohusika au ni kwa faida ya wasikilizaji. Maoni yangu ni kwamba kwanza kwa wenye vibali vya kukata mkaa walipe kodi nying sana pia kwa gar zitakazokamatwa na mkaa wa magendo zipigwe fain kubwa then washushe bei ya gas. Uku pwan gas elf 60 kubadilisha elf 22. Wakati gunia la mkaa elf 15 .
 
Mkaa uwekewe kodi na upigwe marufuku ukikamatwa na mkaa kifungo na faini na gsei ishuke bei
 
hapo tatizo linakuja mkaa unauzwa Kwa kupima gesi hakuna ya kupima.
Niko la gesi ni 80,000+ jiko la mkaa ni 5000-10'000
mpira wa gas ni 30,000
gas huwezi bandikia maharage ila mkaa unaweza m.
hSerekali kupitia watendaji wa vijiji wangeweka utaratibu wa kugawa mamilo na mitungi Kwa familia na walipe kidogo kidogo hii ndo itakuwa mwarobaini wa kutibu hilo tatizo
 
Nyie mnaongea tu kwa kuangalia vipato vyenu. Unajua initial cost za kutumia gesi? Mnadhani kuna ambae hapendi kutumia gesi?? Kuzuia au kupunguza kutumia mkaa itawezekana tu pale ambapo serikali itagawa mitungi ya gesi bure kia nyumba na vilevile kuweza kuuza gesi ya rejareja mpaka ya shilingi elfu moja. Vinginevyo itabakia siasa tu na matamko yasiyotekelezeka.
 
Back
Top Bottom