Mijini kwa utapeli

Mijini kwa utapeli

Hmaster

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
346
Reaction score
86
Nina uhakika kwa wale waishio mijini na hata katika baadhi ya vijiji aidha wamewahi kutapeliwa au kusikia mkasa wa mtu fulani kutapeliwa au kuibiwa kwa ujanja ujanja flani.
Mimi hapa nina mkasa mmoja ambao ulimtokea mwenzetu mmoja enzi tunapanga nyumba moja maeneo ya flani DSM.
Nyumba tuliyokuwa tunaishi ilikuwa ni kubwa hivyo kuna waliokuwa wamepanga chumba ki1, vi2 na hata vi3, na kwa kweli kila baada ya miezi michache kuna waliokuwa wanahama na hivyo kukaribisha wapangaji wapya kila mara.
Siku moja asubuhi sana kama saa 12 hivi watu wakijiandaa kwa ajili ya kutawanyika katika mihangaiko, alitokea kijana m1 pale maskani kwetu na akamkuta mama mmoja anafagia. Akamsalimia kisha akamuuliza kama jamaa yake aliyepanga chumba cha nje ameshaamka au bado yupo ndani amelala amgongee mlango. Yule mama bila kujua kwmba yule kijana ni tapeli na mwizi akamjibu kuwa jamaa yake ameshaamka na yupo bafuni anaoga. Bafu lilikuwa nyuma na ni mbali kdgo na chumabani hivyo anayeoga alikua hasikii majibizano wala hawaoni. Jamaa akamwambia yule mama ya kwamba kama jamaa anaoga basi yeye atamsubiri chumbani kwake hadi arudi. Yule mama kwa kutokumfahamu yule anayeoga kwa ugeni wake akaamini yule ni rafiki zake. Hakuwa na neno. Lakini ghafla yule jamaa akatoka mle chumbani kwa mwenzie akielekea kule nyuma anapooga mwezie na kuanza kumlaumu kwa sauti ni kwa nini anachelewa kutoka wakati muda unakwenda. Anayeoga kwa kujua ni m1 wa wanaosubiri huduma ya bafu akamjibu yupo karibu kutoka. Jamaa tapeli akarudi kwa yule mama na kumwambia kuwa yeye anatangulia, hivyo jamaa akitoka amwambie ameshindwa kuvumilia na atamkuta mbele kwa mbele. Huyo akasepa!
Kumbe kile kitendo cha kuingia tu mle ndani kwa mwezie akachukua hela kwa wallet pamoja na simu ya mkononi. Jamaa alipotoka tu na kuambiwa kuwa jamaa yake amemsuri ndani na kuamua kuondoka akajua tayari kashaibiwa kwani hakuwa na miadi na mtu asubuhi hiyo. Aliingia ndani kuja tu ni vitu gani vilivyoibwa.
Na wewe ndugu yangu kama una mkasa wowote uliokupata au aliopata kuusikia tueleze wenzio ili tuepuke mitego hii ya mjini. Asante.
:coffee:
 
Mimi unaupata ulemchezo sjui unakuta kuna vitu vimepangwa barabarani vile mabeseni, sjui redio, sjui tv na vingine vingi alafu kuna mchezo wanachezesha, alafu unaskia wanasema elfu tano mara ya kwenza, elfu tano mara ya pili, ile ya mara ya tu nikasema hebu nichungulie Ahhhhhhhaa!! nimeshapigwa mchanga kitambo kiiingiii nikasema doh! Dar es salaamaaa mji wa lawama
 
hii hamishieni hoja mchanganyiko bana, humu ni full malavidavi!
 
niliwahi kupigwa kilo mbili zangu mwaka 2000 kuna jamaa walitaka et kuniuzia dhahabu iko kwenye test tube walipo ondoka kufungua nakuta betrii niliishiwa nguvu kabisa na ilikuwa nauli yangu na shemeji yenu tamaa mbaya
 
Back
Top Bottom