Miji 28 Ifakara sasa kazi kwa saa 24

Miji 28 Ifakara sasa kazi kwa saa 24

Wizara ya Maji

Govt Institution
Joined
Oct 2, 2024
Posts
33
Reaction score
20
Serikali imemtaka mkandarasi wa mradi wa maji wa miji 28 Ifakara kufanya kazi kwa saa 24 ili kufikisha huduma ya maji kwa wananchi mapema.


Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Andrew Mathew (Mb) amesema akikagua mradi huo Oktoba 2, 2026 kuwa uamuzi wa kufanya kazi hivyo utafanikisha kukamilisha mradi kwa wakati.

Mradi unatekelezwa kwa thamani ya Shilingi bilioni 48 ukihusu ujenzi wa kidakio ,mtambo wa kuchakata na kutibu maji,na ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji lenye uwezo wa ujazo wa lita Milioni 4 ambapo kwa sasa utekelezaji umefika asilimia 71 na utahudumia zaidi ya wananchi 80,000.

Amesema kwa muda uliobaki kwa kuzingatia msimu wa mvua unaokuja mkandarasi anatakiwa kupanga ratiba vizuri ili kukamilisha mradi kwa wakati ili wananchi wa Ifakara na maeneo jirani wapate huduma ya majisafi,salama na yenye uhakika.

Mradi huo ni uwekezaji mkubwa wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania .

Mhe Kundo ametembelea eneo la mto Lumeno ambao ulikatika na kuhama uelekeo wake kutokana wingi wa maji yanayopita katika mto huo kipindi wa mvua.

Amemwelekeza Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji, Wizara ya Maji Bw.Robert Sunday kwa kushirikiana wa wataalamu kuhakikisha kazi ya kurudisha kipande cha mto kilichohama katika mkondo wake inafanyika ili kuepuka na madhara yanayoweza kujitokeza .
 

Attachments

  • 1.jpeg
    1.jpeg
    190.9 KB · Views: 4
  • 2.jpeg
    2.jpeg
    179.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom